Shukuru Kawambwa kwenye mgogoro wa ardhi na diwani mstaafu, Hassani Usinga. Watishiana kufungana pingu

Ndugu yangu ogopa mtu aliyeambatana na hawara, anaweza fanya lolote kwani anatumia kichwa cha chini kufikiri
 
Raia yeyote ana haki ya kumkamata mtu na kukfikisha kwenye vyombo vya dola na ikibidi nguvu kidogo itumike. Hapo kwenye kupima nguvu kidogo ndo shida tu basi
 
Mleta mada huna adabu.
Prof. Kawambwa ninafahamiana naye.
Hawezi kujiingiza kwenye udalali. Hakua na elimu ya kudesa huyu bwana. Amesoma uhandisi UDSM akasoma PhD yake masuala ya engineering Australia
Hakua na skendo za kipuuzi na si mtu wa kujikweza na mpuuzimpuuzi kama walivyo CCM wengi.
 
Kawambwa na JK ni ndugu kabisa wale! Kijana atajua,hajui! Watampoteza kwa msala watakaompa
 
Nimeludia kuitizama vzr video ya jamaa anavyomshambulia Dk. Kawambwa, kiukweli jamaa alikosea sana na bila shaka atajuta sana kwa ujinga mwamba alioufanya??

Hivi ujasili wa kumfanyia vivyo kiongozi mstaafu aliutoa wapi?

Pia nimpongeze mzee Kawambwa kwa busara kubwa sana alioionesha! Ingekuwa mtu mwingine pale pangechimbika vibaya sana. Mimi mwenyewe sikubali unyonge wa namna hiyo.
 
Kawambwa ni mstaarabu sana sio muongeaji. Naona vijana wanampa jambajamba 😃
Kweli jamaa namkumbuka sana kipindi kile cha Hawamu akiwa waziri Elimu...kuna kamgogoro flan hivi tulikafanyaga akiwa na Naibu waziri wake anaitwa somebody Mrugoo walituzingua sana...Ila huyu Mwamba alikuwaga Mpole sana ata ukikutana nae anaongea poa sana.
 
Philip Mulugo - much know 😃
Alitoa boko Mulugo nakumbuka la kijiografia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…