Hii ndio shida ya watanzania, wakipata ajira sijui busara inaenda wapi. Kwani hata ukiwa na mamlaka huwezi kuongea na watu vizuri mkaeleweshana mpaka ufoke?
Sasa hata kama hakumfahamu Dr.Kawambwa, alipaswa kuongea nao vizuri tu, na hata kama unampeleka mtu polisi unamueleza kawaida hapa umefanya makosa, na ina bidi twende polisi ukatoe maelezo, au tutakushitaki ili huyu mlalamikaji apate haki yake.
Lakini Duh utafikiri mtu kaingiwa mashetani/majini anapayuka na kelele utadhani mwehu.
Uzee ni mtakuja hata uwe kijana vipi utazeeka tu, sasa kwanini usiwe na busara na hekima unapoongea na wazeee?
Tukiwa kwenye ofisi zetu tuwe na busara na ustaarabu kidogo.