Shule Binafsi ziheshimu likizo za watoto wetu

Kwani wanakulazimisha,unahiari ya kumkataza mwanao, ila nikukumbushe tu, kuna kamsemo ka wahenga kuwa kama elimu ni ghali jaribu ujinga. Kwa nyoongeza kuna mhenga alienda mbali zaidi akauandalia wimbo msemo huo wa mhenga.
Hautaki kuukubali huo ukweli basi andamana watakusikia na watakuelewa kwa faida yako na familia yako na mwanao.
 
Imekuwa ni kawaida kwa watoto wanasoma Shule za Binafsi kuwabebesha watoto mafurushi ya kazi za kufanya wakiwa likizo almaarufu Kama HOLIDAY PACKAGES na wakati mwingine watoto wanaendelea kwenda shuleni wakati wa likizo kwa kile kinachoitwa HOLIDAY COACHING. Sasa hizi ni likizo?

Likizo zingeachwa huru ili watoto wawe huru kuwasaidia wazazi wao kazi za nyumbani au kusafiri kwenda kuwasalimia bibi zao huko vijijini ili wafahamu asili yao na pia kujumuika na ndugu zao wengine.

Tungeomba Serikali ilitazame hili jambo na ikiwezekana itoe mwongozo kuhusiana na jili jambo. Tusiwafanye watoto wetu kuwa kama ndondocha, kuna maarifa mengine ambayo watoto wanayahitaji zaidi ya hesabu, fizikia na jiorafia.

Naomba kuwasilisha.
Tena wanalazimisha na kutaka mzazi ulipie?
Hivi kama mtoto amefundishwa ipasavyo atashindwa vipi kufaulu mtihani taifa la nne, saba au form 2?
 
Ubongo unahitaji mapumziko ili ufanye tafakari na organization of knowledge, madhara yake ndio hawa wasomi wenu wa bongo mnawaita 'hawezi kuconnect dots'. Hakikisha mtoto anapumzika na kusocialize wakati wa likizo sana hawa wa private school wanawaoverload sana kwenye ubongo
 
Kwani wanakulazimisha,unahiari ya kumkataza mwanao, ila nikukumbushe tu, kuna kamsemo ka wahenga kuwa kama elimu ni ghali jaribu ujinga. Kwa nyoongeza kuna mhenga alienda mbali zaidi akauandalia wimbo msemo huo wa mhenga.
Kuna kitu kinaitwa kupumzika au kutuliza akili ndomana walitengeneza kalenda kuwa Kuna muda akili inatakiwa ifikirie vitu vingine ili ukirudi kwenye Jambo la msingi akili inakuwa active na concentration inakuwa Bora zaidi.

Muda huu watoto walitakiwa kupumzika na kufikiria watarudije term ijayo haijalishi n darasa la mtiani au lah,

Hawa walimu Kama sio Giza watoto wangekuwa wanashinda darasani usiku na mchana
 
Ni kweli kabisa.

Hii inatokana na walimu wa shule hizo kuwa wavivu kumaliza syllabus.

Kingine ni kwamba ma director wa shule pia huchelelewa kuwalipa walimmu mishahara au kutowalipa kabisa na hivyo walimu hawafundishi.

Wanakuja kukurupuka mwezi wa 5 umekaribia na ndiyo matokeo yake wanaleta hizi HOLIDAY PACKAGE.

Serikali iingilie kati hili suala maana madirector wanaadhbu mtu asiyetoa HOLIDAY PACKAGE
Huu ni wizi tena ulovuka mipaka form2 eti hawafungi sababu koronna mwaka jana lhawakusoma wanafidia likizo hamna mwaka huu
 
Imekuwa ni kawaida kwa watoto wanasoma Shule za Binafsi kuwabebesha watoto mafurushi ya kazi za kufanya wakiwa likizo almaarufu Kama HOLIDAY PACKAGES na wakati mwingine watoto wanaendelea kwenda shuleni wakati wa likizo kwa kile kinachoitwa HOLIDAY COACHING. Sasa hizi ni likizo?

Likizo zingeachwa huru ili watoto wawe huru kuwasaidia wazazi wao kazi za nyumbani au kusafiri kwenda kuwasalimia bibi zao huko vijijini ili wafahamu asili yao na pia kujumuika na ndugu zao wengine.

Tungeomba Serikali ilitazame hili jambo na ikiwezekana itoe mwongozo kuhusiana na jili jambo. Tusiwafanye watoto wetu kuwa kama ndondocha, kuna maarifa mengine ambayo watoto wanayahitaji zaidi ya hesabu, fizikia na jiorafia.

Naomba kuwasilisha.
Ndo maana mtu akiwa na pesa peleka.mtoto wako International school. Kule hakuna huo ujinga
 
Ni kweli kabisa.

Hii inatokana na walimu wa shule hizo kuwa wavivu kumaliza syllabus.

Kingine ni kwamba ma director wa shule pia huchelelewa kuwalipa walimmu mishahara au kutowalipa kabisa na hivyo walimu hawafundishi.

Wanakuja kukurupuka mwezi wa 5 umekaribia na ndiyo matokeo yake wanaleta hizi HOLIDAY PACKAGE.

Serikali iingilie kati hili suala maana madirector wanaadhbu mtu asiyetoa HOLIDAY PACKAGE
Sio wavivu bali ni Biashara wanafanya,
 
We nae unachokiandika hata hujui sijui umekalilishwa hio misemo.

Nimemuelewa sana mtoa mada likizo ibaki kuwa likizo.
Kwani wanakulazimisha,unahiari ya kumkataza mwanao, ila nikukumbushe tu, kuna kamsemo ka wahenga kuwa kama elimu ni ghali jaribu ujinga. Kwa nyoongeza kuna mhenga alienda mbali zaidi akauandalia wimbo msemo huo wa mhenga.
 
Si unamtoa mtoto huko bwashee.
Utampeleka wapi kila kona ni hivyohivyo, hizo shule zinabore sana, ni ujinga mtupu et mtoto wa shule ya msingi asiende likizo ya maana ati ni masomo ya ziada.
 
Tena wanalazimisha na kutaka mzazi ulipie?
Hivi kama mtoto amefundishwa ipasavyo atashindwa vipi kufaulu mtihani taifa la nne, saba au form 2?
Hizo ni Biashara tu
 
Ubongo unahitaji mapumziko ili ufanye tafakari na organization of knowledge, madhara yake ndio hawa wasomi wenu wa bongo mnawaita 'hawezi kuconnect dots'. Hakikisha mtoto anapumzika na kusocialize wakati wa likizo sana hawa wa private school wanawaoverload sana kwenye ubongo
Mkuu, Elimu ya Bongo isha kiwa Biashara na hakuna kitu kibaya kama kuingiza Biashara kwenye elimu au Afya,
 
Kabisa! naunga mkono hoja.
Inasemekana hizo "home packages" ni za kutengeneza fedha.
Mtoto asipofanya mzazi anatozwa fedha na hiyo fedha wanakwambia ndiyo fidia kwa mwalimu atakayemfundisha masomo ambayo hakufanya.
 
Back
Top Bottom