A
Anonymous
Guest
Miaka ya hivi karibuni kumekua na tabia imeibuka na imeota mizizi ya kuwanyima wanafunzi haki yao ya kupumzika wakati wa likizo.Shule nyingi zimekua haziwapi likizo wanafunzi mpka mwezi wa 12.
Hii ina maana wanafunzi wanasoma mwaka mzima bila kupumzika.Tabia hii ilianza kwa shule binafsi hasa kwa wanafunzi wanaosoma madara ya mitihani kama darasa la nne, la saba, kidato cha pili, nne na sita ila kwa sasa tabia imeota mizizi ni kwamba karibia madarasa yote hawafungi na sio shule za binafsi tu mpaka za serikali.
Kiutaratibu Kamishina wa elimu ndio mwenye jukumu la kupanga siku za masomo (kalenda ya masomo)cha ajabu kalenda hyo haifatwi na shule za binafsi wala za serikali.
Nimekuwa najiuliza, hii nchi waliopewa dhamana wapo wapi kufatilia? Kazi ya kamishna wa elimu ni ipi? Au yeye kazi yake ni kupanga kalenda ya masomo kisha anaendelea na hamsini zake?Nakumbuka waziri wa Elimu Bwana Adolf Mkenda alipiga marufuku jambo ili la wanafunzi kubakia shuleni wakati wa likizo lakini cha ajabu tabia hii imeenda hata kwa shule za serikali.
Likizo zimewekwa kwa ajili ya wanafunzi kupumzika na kujifunza ujuzi mwingine tofauti na wanaopata shuleni.Likizo ndio muda wa wanafunzi kubadili mazingira pia. Enzi zetu likizo ndio ulikua muda wa kwenda kusalimia kijijini au kwenda kusoma tution kwa wale ambao shule zao zina upungufu wa walimu hii pia ilitupa exposure ya kukutana na watu kutoka maeneo tofauti na kubadilisha a materials jambo amablo leo hii haliwezekani sababu wanafunzi wanabakishwa mashuleni.
Kalenda ya masomo ya shule zetu inayotolewa na kamishina wa elimu hakuna anayeizingatia ni kama kila mkoa/halmashauri/shule ina utaratibu wake.kila shule ina muda wake wa kuingia na kutoka shuleni.
Siku hizi imekua kawaida kwa mwanafunzi wa darasa la kwanza na pili kuingia shuleni saa mbili na kutoka saa kumi na moja jioni wakati kwa kanuni wanatakiwa kumaliza masomo saa nane mchana.
Kuna shule moja Mwanza(Nyamanoro sekondari) wanafunzi wa kidato cha nne wanaingia saa moja asubui na kutoka saa mbili usiku na hii ni shule ya kutwa, unajiuliza hawa watoto wanasoma kitu gani masaa yote haya? Vipi usalama wa wanafunzi hawa kutosha shuleni saa mbili usiku kurudi majumbani kwao?
Mwezi huu wa sita ni likizo ya siku 30 lakini tembelea shule nyingi hapa nchini utakuta watoto bado wanaendelea kwenda mashuleni kama kawaida,kamishina wa elimu yu wapi?
Natoa wito kwa serikali hasa Kamishina wa elimu,waziri wa elimu nk wafatilie ili jambo na kuwapa wanafunzi haki yao ya kupumzika na kufata kalenda ya masomo kama inavopangwa tofauti na hapo tunawaharibu hawa watoto kisaikolojia kwa kujiaminisha kwamba tunataongeza ufaulu wa mitihani kwa kuwabakiza mashuleni mwaka mzima.