Mhhh ina maana huyu Makamo wako wa Raisi wa awamu ya nne, ule utalamu wa Maswala ya nuklea aliusomea Tanzania? Bila Nyerere kubinafsisha shule za Serikali sizani kama tungekuwa na kina Lipumba.
Tatizo ndugu zangu mnapenda kulalamika huku mkisahau kuwekeza kwenye elimu, Nyerere alizibinafsisha shule nyingi za Kikristo (Pugu,Kigonsera,Tosa ,Ndanda nk) waikristo hawa kulalamika wakaja na mipango wakachangishana, then wakajenga shule zao nyingine ambazo leo hii zinafanya vizuri.
Nyie wenyewe mnatusema "mnapigwa sana kwenye michango.......",ila hizo shule ndio michango ya wakristo na ndio maana kama umewafuatilia Roma au KKKT kama wakitafuta eneo la kujenga kanisa jipya huwaga wanachukua ekari za kutosha, sasa njoo baada ya miaka 10,utaona kuna kanisa,primary, secondary, chuo cha ufundi, kumbi za sherehe ,nursery na hospital nk. Sasa nyinyi ndugu zangu utamaduni huo hamna, kwenye michango wavivu mnaona kama shekhe anafaidi na familia yake.