Shule ya English Medium imegoma kumuhamisha mwanangu. Hatiani kukosa mtihani wa darasa la nne


Mimi ninashauri baba wa watoto aende kuokoa jahazi.

Mpaka huyu mwanamke analeta jambo mitandaoni maana yake ameshindwa kuwachekecha wahusika ili apate mwafaka.

Baba wa familia ni nguzo ya nyumba
 
Shule za vichochoroni kila mtu anafungua yake[emoji1][emoji1], shule haina akaunt ya bank hatulipagi ada keshi ni mwenfo wakulipia bank napeleka list tu kule.
Mnapoteza pesa zenu bure tu unampeleka mtoto medium school kisa kiingereza ambacho hatukuja kukitumia mm naona kumpeleka mtoto medium ni upungufu wa akili tu na kupoteza pesa tu mpeleke shule za kawaida tu kama ana akili atabaki kuwa na akili na kama ni zoba atabaki hivyohivyo
 
Mimi ni single mother umri wangu ni miaka 34.
Haya maelezo hayahusiani na mada / hayana mchango kwenye mada.
Serikali waki hitaji ni disclose taarifa za hiyo shule pamoja na majina ya huyo madam wanae sema amekimbia na hela pamoja na majina ya uongozi nipo tayari kufanya hivyo.
Pole sana kwa yote uliyopitia.

Ni wazi kuwa unapitia wakati mgumu sana na unastahili msaada wa haraka ili kuwahi deadline (japo hujataja ni tarehe ngapi).

Fanya yafuatayo:

1. Wasiliana na Wizara ya Elimu:
  • Anza kwa kuwasiliana na Wizara ya Elimu. Eleza tatizo lako kwa kina na utoe ushahidi unao nao, kama vile risiti za malipo ya ada na namba za simu za watu husika.
  • Wizara ya Elimu ina mamlaka ya kuchunguza suala hili na kuchukua hatua dhidi ya shule husika. Wanaweza kuagiza shule impe mtoto wako haki yake ya kufanya mtihani wa darasa la nne na kumhamisha kwenye shule mpya.
2. Wasiliana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA):
  • Wasiliana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA)
  • Eleza tatizo lako kwa kina na utoe ushahidi ulio nao. NECTA ina mamlaka ya kuhakikisha kuwa mtoto wako anapata haki yake ya kufanya mtihani wa darasa la nne.
3. Tafuta msaada wa kisheria:
  • Unaweza kutafuta msaada wa kisheria kutoka kwa wakili. Anaweza kukushauri kuhusu hatua za kisheria ambazo unaweza kuchukua dhidi ya shule husika na huyo mwalimu ambaye ulikuwa ukimtumia fedha.
4. Wasiliana na vyombo vya habari:
  • Unaweza kuwasiliana na vyombo vya habari ili kuangazia tatizo lako. Hii inaweza kusaidia kuweka shinikizo kwa shule husika kutatua tatizo lako.
Mambo ya kuzingatia:
  • Kuwa mvumilivu na endelea kufuatilia suala hili. Inaweza kuchukua muda kutatua tatizo hili kikamilifu.
Natumai kuwa hatua hizi zitakusaidia kupata haki kwa mtoto wako.

Nakutakia kila la kheri hili.
 
Ubarikiwe sana mkuu
 

Hela alimpa nani? Huyo mwalimu ndio muhasibu wa shule? Hizo risiti ni halali ? Au ni karatasi zisizo na muhuri? Hayo maandishi yapo kwenye plain paper au ni official writings ?

Shule itamkana huyu kirahisi sana
 
shida ilianzia hapa, ni shule gani inakubali kufanya udalali wa namna hii kwenye ada za shule na usajili wa watoto? unawekaje commission?? ile ni sawa na recruitmnent kwa watoto, unachuja upate vichwa bora ukavifundishe viwe bora zaidi, lakini wao wanazoa zoa tuu kwamba wakiwa watoto wengi ndo analipwa zaidi, ilitakiwa ushtuke hapo, yan mwalimu apokee ada akaziwasilishe shuleni?shule haina akaunti namba ? sijawahi ona.

shida nyingine ni hii, ulipeleka watoto hapo bila kufanya tafiti zakutosha kuhusiana na management ya shule, historia ya shule kitaaluma na hata ikibidi kwenda deep zaidi ya hapa, ukaishia kumsikiliza mwalimu ambae ni jirani yako, mkaanza kupeana ada.

hapa hata mimi ningekua nawaandikia ka memo tu kuwa watapewa risiti, kwa huu ujinga ulio kua unaendelea , hizi pesa natumiwa na mzazi yuko dar, hata mimi ningekula. Kwahiyo mleta mada shida zote ziko na wewe, na hata ukiwahamisha unakojua wewe ukiendelea na ushamba wa namna hii haata hao watoto wakimaliza darasa la 6 au la mwisho watakua hawana akili. Kuna ingredients fulani za umakini katika ufuatiliaji wa mambo ya msingi na yaulazima zimekosakana.

Nawasilisha.
 
Ingawa umeandika mambo mengi lakini wewe ni MZEMBE.Maisha hayahitaji shortcut,hiyo njia uliyokuwa unatumia usitumie tena sehemu nyingine.Nyie ndo mnannua viwanja kwa simu tu masuguru,fukayose,etc oh haina shida wewe tuma tu hela documents zote ntasimamia usiwaze...ndo maana mnapigwa sana.Akili,Akili mtu wangu!
 
Mpaka umeamua kufungua ID mpya ili ku post malalamiko yako, itakuwa ulimtukana sana LIKUD by the way, mtafute akusaidie
 
Siku hizi shule ikiwa na noah na madarasa mawili na choo eti tayari ni English medium

We nae ukute ata kwa afisa elimu uja wahi kwenda una kuja kulia lia direct humu
 
Wakati Mwingine Msikilize Ushauri Kwa Baba Wa Hao Watoto.

Sasa Mkiachana Hamtaki Kumshirikisha Zaidi Ya Kuomba Ada Ya Watoto Na Matumizi Hadi Mambo Yanapoharibika.
 
Fika kwa afisa elimu wa wilaya husika tatizo lako dogo sana
 
Mimi ninashauri baba wa watoto aende kuokoa jahazi.

Mpaka huyu mwanamke analeta jambo mitandaoni maana yake ameshindwa kuwachekecha wahusika ili apate mwafaka.

Baba wa familia ni nguzo ya nyumba
Kuna mambo mengine hapa duniani hayahitaji nguvu; chukulia mfano, labda unahitajika kufanyiwa upasuaji na mtaalamu wa hilo tatizo ni mmoja tu, unafikiri ukitumia nguvu inaweza kuwa suluhisho?
 
suala dogo sana hilo funga safari hadi shuleni kamata mwalimu uliekua unamtumia ada kesi imeisha. masuala ya hela sio ya kuongea kwa simu nenda personally
 
Kuna mambo mengine hapa duniani hayahitaji nguvu; chukulia mfano, labda unahitajika kufanyiwa upasuaji na mtaalamu wa hilo tatizo ni mmoja tu, unafikiri ukitumia nguvu inaweza kuwa suluhisho?
Kwamba baba atatumia nguvu? Au mfano wako una maanisha nini?
 
Aisee
 
Kikubwa kubali kua wewe ndio una makosa. Baada ya hapo lipa ada mtoto ahamishwe kwa utaratibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…