Shule ya English Medium imegoma kumuhamisha mwanangu. Hatiani kukosa mtihani wa darasa la nne

Tatzo huo mfumo wa kulipa ada kwa mtu binafsi ndo lilipo anzia, solution hapo ni shule ipate haki yake, huyo mwalimu pambana naye indivudual ila shule haihusiki
 
Kweli mkuu, huo ushauri auzingatie inaweza kusaidia
 
Tatizo mnaona usingle maza kama fashion... Hao watoto watakusumbua lwenye malezi hadi uone umuhimu wa kujishusha na kuishi na mume.
 
Msiwe mnapeleka watoto wenu kwenye shule hizo za English Mediums ni ubabaishaji mtupu
kila mtu si ana watoto wake? tusipangiane, wewe peleka wa kwako kayumba huyo akanyee choo cha shimo.
 
Nakupa ushauri kwa ajili ya mustakabali wa mtoto wako na pia usimuathiri kisaikolojia mtoto. Pole sana. Umejieleza kwa kirefu lakini chanzo cha tatizo kinabaki kwako mwenyewe kuamini watu katika mambo ya pesa. Kwani kulikuwa na ugumu gani wa kuchukua namba za akaunti ya shule ukawa unalipa ukiwa huko huko Dar?

Ushauri wangu. Cha kwanza mpaka sasa kubali umepigwa. Tafuta hela sehemu yoyote hata kwa kukopa kama laki sita hivi halafu nenda shuleni hapo mguu kwa mguu ukawalilie wakupe namba za usajili ili mtoto asajiliwe kwanza. Hakika watakupa tu.

Usianze kusema mara oooh sina muda wa kwenda Mwanza wakati hii ni dharura na inatakiwa itatuliwe mapema kwa ajili ya mtoto wako.

Baada ya kupata namba za usajili, sasa anza kufuatilia kuhusu huyo mwalimu ingawa umbali nao utakusababisha ukose nguvu za kufuatilia. Hilo suala inabidi mshirikiane wewe na shule kufuatilia kwa sababu hapo tapeli ni madam na siyo shule. Inawezekana madam alikuwa anaiba hata risiti na mhuri anagonga anawapa watoto wako. Lakini kuiachia shule ikufuatilie suala lako wewe ukiwa Dar haiwezekani tu mana Watanzania tunajuana.
 
Wanasema hawatambui risiti hizo kwa sababu zimetoka kwa huyo mwalimu. Wanataka nilipe milioni moja na laki 2 ndio wamtoe mwanangu kwenye system wamuhamishie kwenye hii shule yake mpya
Hii issue itakuhangaisha sana mkuu kama vipi anzia kwa mkuu wa wilaya ikishindikana huko nenda kwa wazir wa elimu ama Dr Gwajima Nina uhakika huko watakusaidia

Ila huyo mwalimu binafsi ningemtia adabu kwa hicho alichokifanya.
 
Eti mimi ni single mama, kumbe ni sifa.... kulanina.
 
Tatizo mnaona usingle maza kama fashion... Hao watoto watakusumbua lwenye malezi hadi uone umuhimu wa kujishusha na kuishi na mume.
Kwahiyo Kila mwenye mume watoto wake wanalelewa vyema sio? Acha kujisahulisha kama vile unaishi sayar ya mars.
 
Kwanini unataka kutupia lawama kwa hiyo shule ya English medium mzazi, hapa kinachoonekana ni wewe kutapeliwa na huyo mwalimu uliyemuamini. Omba tu hiyo shule wakisaidie kiungwana uwahamishe watoto wako ila wakikaza mzigo unaangukia kwako.

Ni jukumu lako kulipa ada shuleni sio kwa mwalimu wa shule.
 
Kwahiyo Kila mwenye mume watoto wake wanalelewa vyema sio? Acha kujisahulisha kama vile unaishi sayar ya mars.
We unamwa kweli, Sijasema kila mwenye mume mzee, Nimemlenga yeye kutokana story yake inaonesha anapitia hizo changamoto kwa sababu ameamua kuwa singlemaza.
 
Nyongeza. Wala usinielewe vibaya ukadhani naijua hiyo shule, ila nataka mtoto wako akae sawa kwanza halafu mengine yatafuata mana umesema juzi juzi mtoto alikuwa analia anakuuliza itakuwaje.

Niulize. Kwani hiyo shule imekataa kumsajili huyo mtoto kufanya mtihani wa darasa la nne?

Ni kweli, sheria inakataza mwanafunzi kuzuiwa kufanya mtihani kwa sababu ya ada.

Sasa ifahamike, huyo mtoto hajahama bali anasomeka anasoma hiyo shule ya medium huko Mwanza.

Hivi mama mtoto ukiendelea kuleta ubishi kwamba haujatapeliwa na madam, halafu muda ukafika hiyo shule ikamsajili huko Mwanza na yeye anasoma za Kiswahili huko Dar utafanyaje? Sheria ipo wazi inasema asizuiwe kufanya mtihani.

Nenda kawalilie hiyo shule uwape hata hela kidogo, kubali hasara tu.

Huyo mkuu wa wilaya yeye atataka dhuluma kwa shule?
 
Mtafute pia malisa GJ kwenye mitandao akusaidie kupaza sauti
 
Hii issue itakuhangaisha sana mkuu kama vipi anzia kwa mkuu wa wilaya ikishindikana huko nenda kwa wazir wa elimu ama Dr Gwajima Nina uhakika huko watakusaidia

Ila huyo mwalimu binafsi ningemtia adabu kwa hicho alichokifanya.
Kesi ya milioni moja kupelekana kwa mkuu wa wilaya ni upotevu wa muda tu hata Mkuu wa wilaya hatokubali kuhangaika na ujinga wa hivo, yeye akubali kala hasara amtafute huyo mwalimu haata kwa kumtrack kama mwizi wa simu japo kuwa nako ataliwa hela na polisi ila akimpata atamkanda vizuri mtuhumiwa wake
 
Nenda karipot police huyo mkuu wa shule na mkurugenz wakamatwe wawekwe lockup halafu nenda kwenye dawati la jamii, jinsia wanawake na wazee watakusaidia
 
Nenda karipot police huyo mkuu wa shule na mkurugenz wakamatwe wawekwe lockup halafu nenda kwenye dawati la jamii, jinsia wanawake na wazee watakusaidia
Mnaingiza siasa kwenye logic,
Hapo kazingua mwenyewe, atafute hela alipenada kisha aanze kumtafuta mwalimu jirani yake,
Shule haikuhusika na chochote ni yeye ndio alileta huo ushost,
 
Ukiachana na hayo yote unayopitia,,Kwanza nikupe pole na pia jipe moyo Kwa kuwa kila mmoja anapitia changamoto zake tena nyingine NI kubwa kuliko hiyo yako,,umejaaliwa utashi kaa fikiri kwa kina tatua hiyo changamoto yako hilo ndilo la msingi Haswa kwenye maisha ni wewe kwanza kama ilivyo Kwa wengine NI wao Kwanza,,Nje ya Mada tunaweza wasiliana zaidi kama hutojali Mama wawili??
 
Ada inatakiwa ilipwe kwenye akaunti ya shule unampaje mwalimu tu fika. Hizo risiti zinatengenezwa, mihuri inafojiwa, signature zinafojiwa yaani kwa kifupi unaweza kuta hizo risiti ni fake japo zina nembo na kila kitu cha shule.
Uzembe ni wako Ada huwa hailipwi kienyeji enyeji kwa kumuamini mtu.
Naweza sema huo mzigo ni wako na umefanya kosa kubwa sana.

Pesa huwa inalipwa kwenye account ya shule tu! Hata kama ni mkuu wa shule kakuambia pesa uwe unamtumia ni Kosa kubwa sana usije rudia tena.
 
Pole Sana , Ila watz na wachangiaji ni Kama huwa hawana kitu kichawani MTU anaomba ushauri then wewe unamlaumu .


MTU akileta lalamiko lake tujikite katika kutatua tatizo na sio kulalamika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…