Sio swala yani!
Nafikiri ni wakati wa shule baadhi kuwa converted to English mediums na kupewa facility nzuri walau kila zone iwe na shule hata 3 za hivyo. Kuliko kuwa na mashule mengi ambayo hayana walimu.
Mfano: Tabata kuwe na shule kadhaa za hivyo yani segerea iwepo moja, Kimanga Moja, Kinyerezi Moja, Jeshini moja kule...Pawe na full facilities. Hata wakilipisha ada laki 3 sio kesi ila shule iwe imekamilika watu watalipa.
Mlimani napo ikiwepo moja sio kesi maana wana eneo zuri la kuinvest shule wasome watoto wa ma lecturers. Na wazazi wa Sinza na maeneo jirani kama changanyikeni wapate elimu nzuri tu.