KERO Shule ya Sekondari Kisungu-Dar, Wanafunzi wanapewa adhabu ya kuleta tofali za kujenga uzio

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Inaweza kuwa ni sawa, je ni mfumo rasmi kuwa adhabu iwe hiyo??
Kwani jukumu la kujenga uzio wa shule ni la wazazi/wanafunzi au Serikali yenyewe??
 
Ulitaka wapewe adhabu ipi
Nchi hii ukikutanana na watu kumi , nane WAJINGA… watoto wakichapwa shida , wakipigishwa mazoezi changamoto, wakirudishwa nyumbani malalamiko sijui wanataka wafanyweje? Mwanafunzi akichelewa analeta tofali na uzio wanaona unajengwa lakini bado wanalalamika …wanataka nini sijui ?
 
Inaweza kuwa ni sawa, je ni mfumo rasmi kuwa adhabu iwe hiyo??
Kwani jukumu la kujenga uzio wa shule ni la wazazi/wanafunzi au Serikali yenyewe??
Adhabu nyingine zote wanafunzi wanakufa bora hiyo mzazi atamuamsha mwanaye awahi atake asitake
 
Nchi hii ukikutanana na watu kumi , nane WAJINGA… watoto wakichapwa shida , wakipigishwa mazoezi changamoto, wakirudishwa nyumbani malalamiko sijui wanataka wafanyweje? Mwanafunzi akichelewa analeta tofali na uzio wanaona unajengwa lakini bado wanalalamika …wanataka nini sijui ?

Nchi hii mnakutana wajinga wengi kisha mnadhani kwa sababu ni wengi basi mpo sahihi. Ninyi walimu mkichelewa huwa mnapeleka nini kama adhabu? Ndo maana kuna wakati Mkuu wa Mkoa/Wilaya mmoja aliamua kuwachapa viboko sababu hamna akili ninyi walimu. Kama wanafunzi wenu tu mlivyo.
 
Wanafunzi wetu ni watoto wenu …and that makes three of us…
 
Huu ni umbeya TU
yaani uliposema ulienda kuuliza wazazi wengine
 
Halafu baadae wanasema wametumia shilingi kadhaa kujenga shule, hii haikubariki mwanafunzi anapaswa kupewa adhabu zinazostahili na sio kuleta pesa za kujenga tofali.
Nilisoma kipindi ambacho tunaambiwa tulime binafsi sikuwahi kulima ndio maana shule za private wanafunzi wanafanya vizuri hizo shule unakuta walimu wa masomo mengi hawapo.
 
Back
Top Bottom