Shule za English Medium ni kiwanda cha kuongeza Depression kwa wazazi na watoto. Serikali iboreshe shule za umma

🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
Kuna jambo hapa
 
Hapo kwenye fake life la school ndio hatari. Mtoto anashindishwa shule anasoma weee. Mtoto anafika Shule hafagii darasa wala eneo, anakunywa uji anaoshewa kikombe, anakula chakula anaoshewa sahani, yeye ni kusoma tu. Nyumbani hana muda wa kukaa 11 alfajiri hadi 12 jioni.
 
Kuna familia moja inasomesha watoto 3 International school , ada ni 25 milioni kwa mtoto. Juzijuzi anahaha kuuza kiwanja ili apate milioni 75 alipie watoto ada. Kwa hiyo watoto hadi wamalize shule inaweza kufikia hata billion. Huu ni uwekezaji usio na tija. Soko lenyewe la ajira hapa bongo tunalijua. Hizo sijui milioni 75 kwa mwaka ungenunua hata bond za serikali ungepata faida endelevu, pia watoto wangefaidika na uwekezaji huo lakini wewe umepeleka zote shule mpaka unauza assets. Kazi kweli.
 

Hao wa international school wapo level ya juu sana. Wengi vipato vyao vikubwa vina afford hizo ada.

Mtoto Hawezi kwenda Hopac, Feza international ama IST kwa kutegemea baba au mama mwenye mshahara wa milioni moja ama mbili kwa mwezi.

Pia international schools mtoto hachukuliwi na school bus saa 11 alfajiri na kurudishwa saa 12 jioni. ( shule wanatoka saa saba mchana tu ) Na wala likizo habakishwi shule sababu ya kujiandaa na mtihani

Hoja yangu imeongelea english medium zinazofata sylabus ya necta. Mfano Tusiime, Atlas , etc..

Maana shule hizi wazazi wengi wenye mishahara midogo wamepeleka watoto wao. Huku wanateseka kwa msongo wa mawazo muda wa ada ukifika.
 
Wqchabw Wacha wivu..tafuta hela umpeleke mtoto Academy aje apate kazi DP World! Wallah mwenye elimu ya Kayumba hana future nchi hii zaidi ya kuwa shabiki na chawa wa CCM!
 
Wqchabw
Wacha wivu..tafuta hela umpeleke mtoto Academy aje apate kazi DP World! Wallah mwenye elimu ya Kayumba hana future nchi hii zaidi ya kuwa shabiki na chawa wa CCM!

Wamiliki wa jamiiforums wamesoma kayumba.

Ma CEO wazawa wa mashirika na bank zote Tanzania wamesoma kayumba.

English medium kama Olimpio zipo toka tunapata uhuru mwaka 1961, Arusha school pia ni english medium ya kitambo sana... ila waliosoma hapo hawajafikia nafasi kubwa kama CEO huku wahuni wa kayumba wamezishika hizo nafasi sana tu
 
Kuna wa mishahara wamepeleka International school na wanahaha pia. Ni uwekezaji mbovu. Hii inaongeza stress kwa wazazi pia.
 
Unaamka saa kumi usiku kuandaa mtoto
Saa 11 asubuhi unampeleka barabarani kusubiri bus
Kwenye bag unampa juis na biskuit afu driver anagongea

Saa 9 jion unamsubiri stend tena
Sometimes gari inapita saa 12 kasoro

Akifika home unabid umfanyie tena homework
Aiseee
 
Binti yangu anamaliza form iv mwaka huuu nimemsomesha since vidudu private!! Haki ya Mungu nilikiona Cha mtema Kuni!? Wadogo zake nimesha waalert "ni mwendo wa kidumu na mfagio" sitaki tena ujinga !!!
Nitanunua vitabu na kutafuta walimu wa tuishen


Halafu cha kushangaza akifika chuo kikuu udsm.. anaongozwa na wanafunzi waliosoma kayumba... best students udsm huwa kayumba products enzi wakiwa shule za msingi
 
Naa hao hao ndo wanatuuza kwa DP world kwa rushwa ya suti na whiskey! Nchi hii lazima uielewe kwenda nayo sawa.

Hata hizo shule za academy..kuna waliotoboa na wapo vizuri. Siyo kila mzazi ni lofa. Wengine wamejipanga na wanajielewa. Bottomline stay on your lane mkuu!
 
Kwa mzazi mwenye uwezo ni jambo zuri kuwasomesha Watoto katika shule nzuri, ila kwa Wazazi wenye uwezo mdg si vizuri kulazimisha kusomesha watoto huko

Wanaweza kuwapeleka watoto wao katika shule za kawaida za serikali na wakafanya vizuri tu.
 
Halafu cha kushangaza akifika chuo kikuu udsm.. anaongozwa na wanafunzi waliosoma kayumba... best students udsm huwa kayumba products enzi wakiwa shule za msingi
Kwa sababu siyo rahisi mtu akasoma IST au ISM akaja kufundisha vyuo vyetu vya kibongo. Wanaweza kuwepo ila ni wachache sana.
 
Kwa sababu siyo rahisi mtu akasoma IST au ISM akaja kufundisha vyuo vyetu vya kibongo. Wanaweza kuwepo ila ni wachache sana.

Topic ya shule zilizoongelewa kwenye huu uzi sio shule level ya IST. Huu uzi umeongelea english medium schools level za Tusiime na Atlas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…