Shule za English Medium ni kiwanda cha kuongeza Depression kwa wazazi na watoto. Serikali iboreshe shule za umma

Sahihi
 
Tatizo kubwa ni wazazi kuliko shule tajwa.

wazazi wa sasa umagharibi ni mwingi sana.

watoto wa sasa hawafanyishwi kazi kabisa wanakosa stadi muhimu za maisha na nidhamu njema kutoka kwa wazazi.

Mtoto wa kike kila kitu anafanyiwa na housegirl
Mtoto wa kiume kila kitu anafanyiwa na housegirl

Mzee wangu alikua anatukorogesha zege, tunabebeshwa zege, na kweli unajifunza vingi na sio kuwa tegemezi.

Hata kama mzazi una kipato kizuri usimuendekeze mtoto, wewe na kipato chako huna mkataba na muumba, maarifa bora na elimu kwa watoto wako ndio jambo kubwa kuliko vyote, unaweza kuwaachia vipato vikapotea vyote chaap kwasababu hawakupata maarifa sahihi.

Maarifa sahihi sio tu kufaulu mtihani darasani bali nidhamu katika mbinu zote za maisha.

Ni heri anaepata sifuri mwenye nidhamu kuliko mwenye A++ asiyejitambua.
 
Sahihi 100%
 
Hili sasa ndilo janga la kitaifa kabisa. Na ukumbuke shule za bongo watoto wanasoma ili wapate ajira na hatimaye wapate pesa za kuendeshea maisha. Hii ni sawa na betting ambapo unaweka stake kubwa iliu pate mamilion matokeo yake mkeka unachanika unakuachia stress tupu!

Hii familia inachezea hela kwa kweli. And by the time watoto wanahitimu nafasi za kazi zitakuwa zimeisha kabisa hapa nchini. Hata zile ambazo bado zina magap kadhaa, hayo magepu yatakuwa yameziba moja kwa moja. Hizo hela angewekeza kwa ajili ya ajili ya watoto, wangekuja kumshukuru baadaye.

Shule za mamilioni zinawafaa wanasiasa na mafisadi kwa kuwa wao wanapata hela kiubwete; sio walalahoi na wavuja jasho.
 
Wengi wao wanaongea broken za kutosha lakini kwa kuwa wazazi ni limbukeni wakisikia mwalimu anaongea English wanadhani ni msomi kumbe kanjanja tu. Mimi niliwashtukia siku nyingi. Nimewahi kuona mwanangu kapewa homework ya kukariri marais wa nchi za Afrika lakini nilipopekua kwenye syllabus sikuona topic au subtopic ya aina hiyo. Wengi wa walimu hawa wanafundisha mambo wanayoyajua wenyewe bila kufuata syllabus. Mitihani ikikaribia wanaanza kuwakaririsha wanafunzi majibu. Wanafunzi wa shule za medium uelewa wao unaishia kwenye kujibu maswali na kuongea broken English walizofundishwa na walimu wao. Hawana kingine zaidi ya hicho.
 
Hapo kwenye PS nakazia. Niliwahi kutembelea chuoni nikakuta mwanafunzi anacheza nikaja hapa JF nikafungua uzi kulaumu matumizi mabaya ya muda na fedha za wazazi wake. Watu walininanga sana:
 
Mimi km Bandokitita niseme tu kuwa kwa aina ya walimu wanaofundisha shule za Uma ni bora km unajiweza peleka mwanao English medium. Huwezi kuamini walimu shule za uma hasa Sekondari wanalalamika kila siku kuwa wanapelekewa watoto wasiojua kusoma, kuandika, na kuhesabu, wakati wao 80% hawawezi kutumia lugha ya kfundushia (English language) kwa ufasaha. Muda mwingine unaweza kuwaza hivi hawa walimu waliokotwa wapi. Hilo liko wazi hata Waziri wa elimu Dr Mkenda alisema anajua kuna walimu hawawezi hata lugha ya kufundushia(English language), na wapo wenye uwezo mdogo ktk kufundisha. Hili alikili mwenyewe kwa kinywa chake. Ndo maan wadau wanasisitiza walimu nao wae wanapewa interview kabla ya kuajiriwa.

Hivi mnakumbuka kipindi Cha hayati Benjamini kuna watu waliingia ualimu kwa kutumia vyeti vya watu na feki. Hadi mabamedi walienda vyuoni kusomea ualimu na wakaajiliwa. Heko mwendazake uliwapuruni kwelikweli.

Hivi mnakumbuka enzi za utawala wa mheshimiwa wa Msoga. Kulikuwa na kozi ya miez 3 a.k.a voda faster, waliomaliza form 6 walipiga na kwenda kufundisha, ingawa hawa walipewa sharti la kujiendekeza.

Ktk utawaka wa huyo huyo wa Msoga, walimu wa shule za msingi (form 4) walijiendeleza kwa fujo kwa kusovu past papers za form 6 na walipopata credit (Yani E, E) walienda diploma na waliporudi wakapelekwa secondari badala ya kurudi primary. Wengine baada ya vyuo vikuu kuota km uyoga walipopata D, D kwenye matokeo yao ya form 6 walienda vyuo vikuu na walipomaliza walipelekwa Sekondari badala ya kurudi primary. Hawa waliotoka primary wakiwa either na diploma/degree ndo wengi wao ni wabovu wa kupindukia.

Mtu unawaza, inakuaje mtu asome kizimamoto kwa kosovu tu maswali kwa miezi kadhaa afaulu na kuwa mwalimu bora. Elimu ingekuwa rahisi hivyo watu wasingekuwa wanaingia darasani kupoteza muda wa miak 2 kwa ajili ya form 5-6.

Haya yote ndo yanafanya shule za uma zinaonekana mbovu. Mimi nawapenda sn walimu na siku zote nimekuwa mtetez wao sababu walinitoa ujinga na wanaendelea kutufundishia watoto wetu lakini hili la kupeleka mtoto English medium naliunga mkono. Serikalini huko hasa hizi za kata yanahitajiika maombi mwalimu.
 
Mkuu umeongea ukweli 101%.....siongezi kitu 💪 💪
 
Nakazia 100%. Kule kijijini kwetu kulikuwa na kijana mmoja aliyekuwa anajifanya msomi ilhali yupo sekondari tu. Akirudi nyumbani alikuwa hawasaidii wazazi kulima wala kuchunga ng'ombe. Mwisho wa siku alipata sifuri akarudi kijijini kulima na kuchunga ng'ombe......kazi alizokuwa hazipendi mwanzo.

Halafu nidhamu inasaidia kwenye masomo pia. Ukiwa huna nidhamu hata masomo hutayachukulia serious. Mwisho wake utapata zero na kurudi nyumbani kusumbua wazazi.
 
Umeandika sana il suluhusisho hapo ni kuacha kuzaa watoto wengi zama zimebadilika stress mnazitafuta wenyewe.. mtu anahangaika kuzaa watoto sijui wanne n.k wote wanini ikiwa huna pa kuwapeleka na kuwahudumia vyema? Stress zinaanzia hapo
 

Your browser is not able to display this video.
 
Hivi watoto kama hawa wanapenyaje kuingia sekondari kama sio kwa sababu ya mitihani ya kubet? Ipo haja ya kuangalia namna nzuri ya kutunga mitihani. Nashauri utaratibu wa zamani urudishwe ambapo kila mtahiniwa awe anajaza majibu yeye mwenyewe badala ya kuchagua. Hili likifanyika, wanafunzi wasiojua kusoma watajichekecha wenyewe. Ni afadhali kuwa na wanafunzi wachache darasani kuliko kujisifia kisiasa kuingiza wanafunzi wengi sekondari kwa kuwatungia mitihani ya kubet.

Tunaharibu kizazi cha sasa na cha baadaye kwa makusudi finyu ya kisiasa kwa maslahi ya watu wachache. Na hili ni lengo mahsusi la wanasiasa kuharibu elimu ya watoto wa wakulima ili watoto wao waje wawe watawala wa baadaye. Jambo hili tumeanza kulishuhudia kwa mifano hai. Tazama familia za Karume, Kikwete, Makamba, Mwinyi, nk zinavyozidi kujikita kwenye utawala utagundua ajenda yao imeanza kuzaa matunda.

Asante kwa kunielewa.
 
Hili nalo mkalifanyie kazi.
 
Yaan mtoto ajifunze shida? Kama mzazi anaweza mpa mtoto furaha basi apewe.
 
Waliopita olympio na diamond wengi wako na future nzuri jaribu kufatilia ...hao unaowataja wew ni kwakuwa 98% shule za govt ni za Swahili kwaiyo hesabu ya kawaida TU hata watu wake wata outshine wa hizo shule za olympio na diamond....ila hao hao wachache waliosoma Olympio na diamond Wana posess businesses international level & hata locally huko mitaa ya upanga, ukienda mashirika ya kimataifa wamejaa ,ukienda Dubai , USA ndo usiseme ..Yani Leo hii marekani ukisema uitishe alumni ya olympio na diamond unajaza kijiji
 
English Medium hizi hizi za kumilikiwa na Mr. And Mrs Mugetta, mtaala wa Necta, walimu wanakimbia kila siku kwa kutolipwa mishahara ndio niwalipe milioni hao kwa mwaka aisee nitakuwa na kichaa ama nini
Hao uliowataja wanamiliki shule gani
 
Mkuu ongea kwa sauti ya chini. Dunia haijawahi kuwa sawa
ni swala la kila mtu kutumia akili yake ya kuzaliwa.
Ni kwamba nenda jiji lolote lenye wafanya biashara hapa tz,fanya utafiti kwa wenye
maduka makubwa ya zana za kilimo,spare za magari, nguo n.k
uliza ni wangapi walisoma hizo ''ingilishi midiam'' utakuta wengi ni wale waliojifunza kupambana
toka utotoni wakitokea kayumba,wengine hata form four hawakufika walienda migodini n.k
Wengine kayumba imetufundisha maisha. English medium tuwaachie wanaopelekwa kazini kwa vimemo.
ukijichanganya kuiga,utalalamika mpaka Yesu anarudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…