Mimi bado najiuliza niende shule au sio...lol... kwa sasa kila linalofundishwa shuleni lipo mkononi mwa mtu ,, so why go to school???
Usidanganye.Acha watoto waende shule.Ila tulie na waalimu.Ninajua bila mwalimu huwezi kwenda popote kwani mwalimu ndiye wa kwanza kutoa kutu kwenye akili zetu.
Nilikuwa mara nyingi sana nilikataa katu nilipoambiwa kuna wanafunzi wamejiunga kidato cha kwanza bila kujua kusoma na kuandika.Hili nimelithibitisha kwa mwanafunzi wa darasa la sita bila kujua kusoma na kuhesabu.
Mwanafunzi wa darasa la sita hata kukopi kilichoandikwa na mwalimu ubaoni hawezi, kuhesabu mpaka 100 ni tatizo.Mwandiko ndio basi tena.
Lakini nilisikitika nilipofuatilia zaidi nikagundua kuwa.
1, Hakuna mwalimu anayesaidia mwanafunzi aweze kuandika mwandiko unaoweza kusomeka au namna ya kuumba herufi.
2. Watoto wanafanya hesabu, wanaweka majibu yasiyosahihi, mwalimu anamwekea alama ya vema kuwa kapata kumbe kakosa.(Inawezekana sio waalimu wote ila hawa wanadhalilisha fani ya ualimu.)
3.Mwanafunzi wa darasa la sita hajui orodha kabisa, hata ile rahisi ya 1x1 hajui.Lakini kafika darasa la sita.Hebu nisaidieni,huyu kafikaje darasa la sita.Mtihani wa darasa la nne vipi.
Maoni yangu.
Wazazi chunguzeni madaftari ya watoto wenu kwa kina ili kuwasaidia.Hasa hawa wa madarasa ya awali ya shule zetu za kawaida kabla hawajafika mbali wakiwa hawajitambui.La pigana kufa na kupona mtoto aende kwenye shule za Yes na No.
Waalimu,tunajua wakati mwingine darasa lina watoto zaidi ya 100.ni shughuli kuwamanage. Jiweke kwenye nafasi ya mtoto wako kuwa miongoni mwa hao 100 ili uweze kuwasaidia.
Wakaguzi wa shule wako wapi?????????
Nitaendelea.........