Shule za siku hizi hatuendi kutoa ujinga kama zamani

Shule za siku hizi hatuendi kutoa ujinga kama zamani

Yan wazee wa zamani kujiona vyao ndio bora hamjambo

Elimu ya sasa imeboreka na watu wanapata maarifa sema tatizo ni ushindani uliopo kwenye ajira ndo unatesa vijana

Zamani hamkuwa na elimu bora ila mliajiriwa kwa sababu mlikuwa wachache na ndo mana mlikuwa hamuombi ajira,

Halafu kuhusu kujiajiri mitaji bado changamoto kwa tulio wengi, najua utakuja na u motivation speaker kuwa tuanze tulipo + bla bla ila bila mtaji wa pesa hatutaboa na ninyi wazee hamkutuwekea hata akiba ya 5M tuanzie maisha tunabaki kuwa saidia fundi
Mkuu kama ni kweli....."Elimu ya sasa imeboreka na watu wanapata maarifa....." sasa zuio au katazo la kutumia hayo Maarifa liko wapi? Ni ukweli kwamba zamani hawakuomba ajira(na pengine walibembelezwa) lakini hilo haliwafanyi nyie wa siku hizi ambao mmekuwa ni wengi na shule/vyuo ni vingi mtake kuutumia mfumo huo uliotumika zamani. Tumieni Mfumo wa kisasa- Ajira ni Ushindani.
Kuhusu Mtaji, labda nitumie maneno haya kwa nia njema "Mtaji wa Maskini ni Nguvu zake". Ninaamini kwa vijana-wasomi kukaa na kupendelea zaidi kukaa Mijini, mtakaa sana na huenda mtafika a.k.a kutoboa, mkiwa mmechoka sana.
Msichague Ajira na Mahali wakati huna Ajira Mahali popote.
 
Back
Top Bottom