Shule za siku hizi hatuendi kutoa ujinga kama zamani

Mkuu kama ni kweli....."Elimu ya sasa imeboreka na watu wanapata maarifa....." sasa zuio au katazo la kutumia hayo Maarifa liko wapi? Ni ukweli kwamba zamani hawakuomba ajira(na pengine walibembelezwa) lakini hilo haliwafanyi nyie wa siku hizi ambao mmekuwa ni wengi na shule/vyuo ni vingi mtake kuutumia mfumo huo uliotumika zamani. Tumieni Mfumo wa kisasa- Ajira ni Ushindani.
Kuhusu Mtaji, labda nitumie maneno haya kwa nia njema "Mtaji wa Maskini ni Nguvu zake". Ninaamini kwa vijana-wasomi kukaa na kupendelea zaidi kukaa Mijini, mtakaa sana na huenda mtafika a.k.a kutoboa, mkiwa mmechoka sana.
Msichague Ajira na Mahali wakati huna Ajira Mahali popote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…