Shule zaandikiwa Barua kutoa takwimu za Idadi ya wanafunzi wa Kiislamu shuleni

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Duh...
 
 

Attachments

  • IMG-20240509-WA0085.jpg
    60.7 KB · Views: 9
Tanzania Haina usawa,Kuna gepu kubwa sana Kati ya walionacho na wasionacho.
Ninaamini Kuna jambo linapikwa kupitia udini,na muungano.
Haya mawingu ni mosh utakao chini.
Acha uwake tu.
 
Haya mambo siyo ya kuulizia mbona ni kawaida tu?Takwimu ni muhimu katika maisha ya mwanadamu.
 
Wanafunzi hawa waliopo mashuleni kuanzia primary mpaka secondary hasa katika shule hizi za umma wana utaratibu wanafundishwa masomo ya dini either bibble knowledge au Islamic knowledge, wa shule ya msingi wanafundishwa ijumaa (au siku nyingine yoyote iliyoamuliwa na shule) masomo hayo ya dini, kila dini hutuma walimu wao inaowaamini kwenda kuwafundisha watoto hao masuala yanayohusu dini zao, hawa wa secondary hufundishwa pia masomo hayo ya dini na huyafanyia mpaka mtihani wa taifa masomo hayo yaani bible knowledge na islamic knowledge.

Na ukumbuke hakuna walimu waliograduate bachelor of education in islamic knowledge au bible knowledge isipokuwa walimu wanaowafundisha hawa watoto wanajitolea. Sasa kama kuna michepuo ya dini imeanzishwa, kuna ubaya gani watu wa dini husika kuomba kwenda kuwatambua walimu wenye dini fulani na watoto wa dini fulani ili kuweka pengine kuweka utaratibu wa jinsi ya kuwafundisha na kuwaandaa au pengine kuwaomba tu walimu waliotayari na wenye uwezo wa kufundisha masomo hayo washiriki katika kufundisha?

Mkurugenzi hana kosa alichofanya ni kuruhusu hao watu na kuomba wapewe ushirikiano sidhani kama kuna kosa au shida yoyote.
 
Sijaona ubaya wa hii barua, kwani kuna ubaya gani kujua idadi ya wanafunzi na walimu wa dini ya kiislamu katika shule za msingi na sekondari ili taasisi husika zipate kujua kuwa kuna uwiano wa kutosha au kutahitajika walimu wa ziada ili watoto wa kiislamu wapate mafundisho ya dini yao kwa uhakika. Mimi ningeomba zoezi hilo lifanywe nchi nzima ili taasisi kama Bakwata ipate kutayarisha walimu na masomo yenye tija kwa watoto wa kiislamu, masomo ya dini kwa watoto wa kiislamu yamekuwa ni mtihani kutokana na wanafunzi kutumia muda mwingi kwenye elimu ya sekula, bora vijana wafuatwe hukohuko mashuleni ili wapate somo la dini japo mara moja kwa wiki.
 
Asante Sana Daktari kwa Ufafanuzi muruwa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…