Shuleni kwa mwanangu wanatozwa Tsh. 300 ya usafi kwa mwezi, kwa shule nzima ni pesa nyingi

Shuleni kwa mwanangu wanatozwa Tsh. 300 ya usafi kwa mwezi, kwa shule nzima ni pesa nyingi

Mimi mwanangu akiniambia walimu wanataka wachangiwe Tsh 10,000/= kwa mwezi kwa ajili ya chai, nitatoa bila kinyongo. Walimu wanafanya kazi ya maana sana. Ni nzito na nyeti kuliko hata ya ubunge lakini malipo yao ni duni sana.
Watuibie kwa akili na adabu sasa.Siyo wanakurupuka na kucharaza hovyo watoto wasiowapelekea franga.
 
Namfahamu hali yake kupitia andiko 😂😂😂😂😂
Make 300 kwa mwaka ni 3600
Likizo march, june, sept december hapo unatoa 1200, inabaki 2400

😂😂😂😂😂 Dah
Unaonaje ukimrushia sh 7,200/= malipo ya miaka mitatu?

Mtoto yupo la tano, atahitaji sh 7,200/= tu kuukamilisha mchango wa usafi kwa kipindi chote cha miaka mitatu iliyosalia.
 
Ila jamaniiii
Sh 300 ndo imekufanya uandike uzi
Ambayo hii 300 inakusaidia nini wewe?
Kama wanafunzi wapo 1200 maanake ni kama 720000 hivi makusanyo
Hapo kuna wafanya usafi labda 5 kila mmoja analipwa 140,000

Mahesabu madogo tu mbona
 
Mtoto ananiambia shuleni wanadai 300 ya usafi kwa mwezi. Darasani wako wanalipa shule nzima sasa hii hela kwa shule nzima jamani

Darasa lao lina wanafunzi 350, darasa la tano kuna darasa la saba wapo 400

Yaani ukipiga hesabu hela wanayopata kwa usafi ni kubwa aiseeeeeeeee sijajua kama afisa elimu anajua haya
Akafanye usafi Ili usitozwe
 
Sasa kutoa Tsh. 300 kwa mwezi kwa ajili ya usafi imekuwa nongwa. Umasikini ni mbaya, naomba Mungu aniepushie mbali na roho za umasikini.
Nimewaza tu shule ina wanafunzi 2000×300=600,000 wafanya usafi wako 3=200,000 kila mmoja bado mtu anaamini walimu wanamuibia
 
Mtoto ananiambia shuleni wanadai 300 ya usafi kwa mwezi. Darasani wako wanalipa shule nzima sasa hii hela kwa shule nzima jamani

Darasa lao lina wanafunzi 350, darasa la tano kuna darasa la saba wapo 400

Yaani ukipiga hesabu hela wanayopata kwa usafi ni kubwa aiseeeeeeeee sijajua kama afisa elimu anajua haya
Shule ipo wilaya gani?
 
Kwanza kama mzazi unatakiwa ujitafakari, watoto 350 darasa moja je uelewa kwa hao wanafunzi utakuwaje?

Kiukweli hapo hakuna nafasi ya mwalimu kuhakikisha kila mwanafunzi kamuelewa sawa sawa, hiyo shule haifai mkuu

Kingine acha kujiuliza mara mbili mbili juu ya shilingi mia tatu, sisi wengine tunaambiwa tulipe registration fee laki mbili huku ungeweza kweli??
 
Back
Top Bottom