Shura ya Maimamu Tanzania: Mlinzi Mwanamume wa Rais kuvaa Hijabu na kuingia Msikitini

Maana bila andiko (surah) wakija BAKWATA wakasema PSU walikuwa sahihi kuingiza mwanaume msikitini, hapo utazuka utata.

Ili kusiwe na utata ni lazima mtizamo wa kuunga mkono ama kupinga ujengwe juu ya Quran tukufu ama hadithi inayokubalika kwa wote.
Na wewe uwe unaelewa

Shura ya Maimamu hajasema Qur'an imekataza Wanaume na Wanawake kukaa pamoja bali tatizo ni kukaa kwa kificho ambako unaweza kuwachungulia maungoni bila Wao kujua
 
Takhbiiiirrrr
 
Na wewe uwe unaelewa

Shura ya Maimamu hajasema Qur'an imekataza Wanaume na Wanawake kukaa pamoja bali tatizo ni kukaa kwa kificho ambako unaweza kuwachungulia maungoni bila Wao kujua
Hakuna Aya kama hiyo inayokataza wanawake na wanaume kuswali pamoja bila kutenganishwa
 
Andiko...!??
Kabla ya kuitekeleza ibada ya swala miiongoni mwa mambo inakubidi ujue ni udhu. Kabla ya kujua udhu inakubidi ujue sharti zake. Na ukijua sharti zake inakubidi ujue sunna zake na fardhi zake.

Kwenye Fiqh mlango wa udhu kuna mlango unazungumzia "nawaaqidhul udhui" kwa maana vitenguzi vya udhu/vinavyotengua udhu. Kutengua kwa maana unafanya udhu wako unakuwa tena si halal kwako. Kwa maana hiyo hutoweza kutekeleza ibada ya swala.

Bakwata ni madh-heb ya Shafii.
Kwenye Fiqh madh-heb ya Shafii miongoni mwa vitu au mambo yanayotengua udhu ni kugusana kwa ngozi baina ya mwanaume na mwanamke. Zikigusana ngozi imma za mikono au miguu kwa sababu kwenye uislam mkiswali ni lazima mpange swafu (mstari) na vidole vya miguu vitakutana na kwa kufanya hivyo ngozi zenu zinagusana.

Kwa mujibu wa madh-heb ya Imam Shafii hapo unakuwa hauna udhu. Kama hauna udhu hauna swala. Kwa mantiki hiyo haifai mwanamke na mwanaume kuswali pamoja.

Swali; kama huyo mlinzi ni mwanaume kwa nini kaenda kuwaharibia watu swala zao? Ina maana anafanya mchezo?

Kingine uislam unaheshimu faragha za jinsia mbili tofauti na ndiyo maana wanaume wana sehemu yao na wanawake wana sehemu yao. Ikiwa kama huyo ni mwanaume kivipi anaingilia eneo la wanawake wenye faragha yao?
 
Acha porojo weka aya
 
Akili imetumika ya hali ya juu sana kutoa ujumbe! Maadili lazima yazingatiwe na hakuna uchawa hapo! Hongereni sana!
 
Maana bila andiko (surah) wakija BAKWATA wakasema PSU walikuwa sahihi kuingiza mwanaume msikitini, hapo utazuka utata.

Ili kusiwe na utata ni lazima mtizamo wa kuunga mkono ama kupinga ujengwe juu ya Quran tukufu ama hadithi inayokubalika kwa wote.
Yapo mambo Aya za Qur'an zipo na hadithi zipo ila bado yana utata, na yapo mambo hayana utata wote wanakubaliana. Hili la mwanaume kujichanganya katikati ya wanawake na kuvaa mavazi ya kike hata kwa akili tu ya kawaida ni jambo ambalo halipo sawa.
 
Nimetafuta kama kuna andiko limewekwa linalokataza wanaume kuswali na wanawake sijaona.

Wangeweka hilo andiko bila ya shaka lingeongezea uzito wa habari yenyewe
Kwani Papa aliporuhusu mashoga kubarikiwa vatican aliweka andiko?

Wewe hujui kua wanawake hawachanganyiki na wanaume kwenye misikiti?

Kwahiyo hao watu wa ulinzi wameingia kwa wanawake coz hawajui hilo andiko? Ingekua hawajui kua wanawake hawachanganyiki na wanaume,wasingejificha kwa kuvaa hijabu.
 
Mimi binafsi siyo muislam ila niseme tu kuwa ikiwa kitendo hicho kimefanyika basi ni makosa makubwa mno yaliyofanywa na waliompangia kazi huyo jamaa na hata kumshauri avae nguo za kike.

Huo ni udhalilishaji kwa akina mama wachaMungu walioingia Msikitini kusali.

Kitendo hiko kitapotezewa kwa kuwa tu Rais ni Muislam ila angekuwa Mkristo, sipati picha ingekuaje.

Ikiwa ni kweli basi serikali iwaombe radhi waislamu wote na watu wachukue tahadhari ili watu wasiendelee kujificha kwa mavazi hayo ambayo hayamtambulisha mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…