Si busara kumruhusu mtoto aanze kujitegemea wakati hana chochote

Mtoto kwanzia akiwa mdogo mjenge ajue thamani ya pesa ,na jinsi ya kupata kipato na kukitunza , then kama una nia ya kuja kumpa mtaji au kumwacha ajitegemee itakua poa sna , usije ukampa mtaji au kumwacha ajitegemee mtoto ambae haujamfundisha vzuri.
Wewe muhudhuriaji mzuri katika vipindi vyangu,hongera😅
 
Mimi baada ya kuingia kidato cha tano shule ya boarding chumba changu kilipangishwa, ilikua ni alama ya sasa sina makazi ya kudumu nyumbani ilimaanisha natakiwa nianze kujitegemea. Toka wakati huo nilijitegemea rasmi.
Baba yako ni mafia
 
Baba yako ni mafia
Namshukuru kwa kitu alinijengea kwenye akili ya kwamba katika maisha nahitaji kutafuta mali yangu. Toka wakati huo sijawahi lilia shida mtu yoyote bila kujali hali ngumu niliyopitia, Najivunia leo kwa kila nilichonacho ni kwa juhudi zangu binafsi(labda na Mungu), sina haja ya kunyenyekea mtu yeyote bali kuheshimu kila mtu
 
Usingekuwa attention angekuathiri kisaikolojia huo mimi naita ni unyanyasaji
Sasa usi apply hiyo kitu kwa watoto wako eti kwa sababu wewe ilikutokea na ukasurvive
 
Watu watu hata nauli tulinyimwa town tumeingia kwa fuso la viazi tukapokelewa na farasi mweupe tukajikuta getto la masela

Tuka Toka kwa kudra za mwenyezi Kama hatuna ndugu

Tumeingia kitaa tukafanya tuka jurikana tulipo jurikana waka tutafta walipo tutafta hatukuwa tupa tuko nao pamoja

Kwani tunajua ilikuwa nimaisha tuu

Vipi nyie watoto wakishua😄😄😄
 
Usiwafanyie wanao sasa😅😅😅
 
Usingekuwa attention angekuathiri kisaikolojia huo mimi naita ni unyanyasaji.
Well, ila kukosa attention tu tayari ni tatizo la kisaikolojia.
Sasa usi apply hiyo kitu kwa watoto wako eti kwa sababu wewe ilikutokea na ukasurvive
Yaah watoto wangu wataamua wanavyotaka ilimradi isiende kinyume na Taratibu ama sheria ama maadili.
 
Binadamu ni wakuja na kuondoka…kuna baba kumzika mtoto au mtoto kumzika baba…walee wanao wakijua ipo sku watakuwa pekee yao ktk huu mgongo wa dunia
 
Binadamu ni wakuja na kuondoka…kuna baba kumzika mtoto au mtoto kumzika baba…walee wanao wakijua ipo sku watakuwa pekee yao ktk huu mgongo wa dunia
Lakini sio kwakumfukuza ama kumuacha ahangaike mtaani ilihali unaweza kumuongoza mpaka akasimama
 
Unadekeza kijana wa miaka 25 kisa unamuonea huruma? Ikitokea haupo je?
 
Lakini sio kwakumfukuza ama kumuacha ahangaike mtaani ilihali unaweza kumuongoza mpaka akasimama
Hakuna mzazi anaependa mwanae ahangaike mtaani…ila wapo watoto wanaopenda kuwa boy street wakijiita masela
 
Wazazi wa aina hiyo ni wale nusu mtu nusu malaika. Sio hawa waliozaliwa wakati wa ukoloni ama baada.
 
Ni vijana wengi wamekutana na mauti wakiwa kwenye hizo harakati bubu za kujitegemea. Ilihali wazazi wao wako na wanamwaga ugali kila siku jalalani.

Pia yale mambo ya kujilinganisha wazazi wanayo sana. Anataka watoto wake wawe kama wa fulani maana wamesoma shule ya aina moja na wamemaliza chuo pamoja.

Ni shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…