Si halali wala haki kwa Serikali ya CCM kuwatoza wananchi fedha ili kutumia Daraja la Nyerere kwenda Kigamboni, ni ubaguzi

Kulipia daraja ni ujima, daraja limejengwa kwa nguvu za wananchi, kama suala ni kuilipa NSSF serikali ilipe. Hata feri ilitakiwa iwe bure kama Mombasa pale Likoni feri zote bure.
 
Probably Kigamboni is a tourist resort, to be precise Kigamboni is Acapulco of Tanzania.
 
Nina nyumba kigamboni, haya toa hoja sasa
Sawa, utakuwa mojawapo wa watu ambao wakipata wanaona wale wasionacho hawana akili sawasawa. Kutoa elefu 4000 kila siku ili kuvuka daraja si wote tunaoweza. Hapo ni nusu kilo ya nyama na viungo kila siku nalisha familia.
 
NSSF kwanza inarudisha gharama zake... Alafu baada ya hapo itakua bure...

Cc: mahondaw
 
Sawa, utakuwa mojawapo wa watu ambao wakipata wanaona wale wasionacho hawana akili sawasawa. Kutoa elefu 4000 kila siku ili kuvuka daraja si wote tunaoweza. Hapo ni nusu kilo ya nyama na viungo kila siku nalisha familia.
Kama huna kwanini usipande daladala ambapo hutalipia chochote zaidi ya ile nauli tu ya kawaida? Badala yake utumje gari binafsi halafu uje ulalamikie kulipia daraja lililojengwa kwa pensheni za wavuja jasho waliostaafu na ambao wanategemea wewe ulipe na wao ndio walipwe viinua mgongo vyao?
 
Kwa miguu na baiskeli darajani ni bure, kwa daladala wewe unalipa nauli tu, hulipii darajani, kama una gari na umeweza kutenga pesa ya mafuta, basi tenga na 3,000/= ya kuvuka.
Ndio unajidanganya kua kwa daladala hulipi eeh, kiuhalisia nauli ya daladala k/Koo ni 400/= imeongezeka kwa ajili ya daraja kwa hiyo unalipia
 
Hivi una akili za namna gani wewe mzito kiasi hiki kuelewa? Suala hapa sio nani ana uwezo wa kulipa au la - suala ni kwamba madaraja Tanzania ni haki ya huduma kwa wananchi. Kama tunalipa Kigamboni waweke toll kwenye madaraja ypote basi - hata na hizo flyover ili kuwe na usawa - equity, unaelewa maana ya equity lakini?

Na nimesema serikali irudishe fedha za NSSF zilizotumika kujenga kwa kuwa ni jukumu lake kujenga madaraja. Kwa hiyo kusema tunalipa fedha kutumia daraja ili turudishe fedhaza wastaafu sio point ya kuongea.
 
Kwa miguu na baiskeli darajani ni bure, kwa daladala wewe unalipa nauli tu, hulipii darajani, kama una gari na umeweza kutenga pesa ya mafuta, basi tenga na 3,000/= ya kuvuka.

Ndio unajidanganya kua kwa daladala hulipi eeh, kiuhalisia nauli ya daladala k/Koo ni 400/= imeongezeka kwa ajili ya daraja kwa hiyo unalipia
Hawa ndio wale wakilala hoteli ya B&B wanasema hii hoteli nzuri sana wanatoa breakfast bure! Utawajua tu, kutokana na point zao za kijima humu JF.
 
Ufaransa kipindi inatawaliwa na king louis xvi walikua na kodi kama hii iliyofahamika kama bridge tax, hiyo ni moja ya sbb mfalme huyo kupinduliwa
 
Nakumbuka mwanzo wakati wanalizindua, walituambia NSSF itatulipisha pesa miaka miwili ili kurudisha pesa yao ya ujenzi,...sasa ni zaidi ya miaka miwili na hakuna matumaini ya kushusha bei wala kuondoa nauli ya kuvuka.
 
Acha kuzunguka mbuyu, hayo yote tumeshajadili, hatuwezi kugharamia daraja ambalo tayari lipo na linafanya jazi tuache kujenga mapya; unaelewa maana ya vipaumbele?!
 
Ndio unajidanganya kua kwa daladala hulipi eeh, kiuhalisia nauli ya daladala k/Koo ni 400/= imeongezeka kwa ajili ya daraja kwa hiyo unalipia
Hayo malipo yanakuwa absorbed na hayawezi kuwa felt significantly maana kwenye basi wanapanda abiria wengi
 
Nauli 450 kumbuka kila abiria analipa 50 hivyo kubaki nauli 400 ya serikali .

Abiria wanalipia isipokuwa wamefungwa jinsi ya kujua wanalipaje
Kwa miguu na baiskeli darajani ni bure, kwa daladala wewe unalipa nauli tu, hulipii darajani, kama una gari na umeweza kutenga pesa ya mafuta, basi tenga na 3,000/= ya kuvuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…