Si kila kitabu kwenye Biblia ni kwa ajili ya wakristo wote

Si kila kitabu kwenye Biblia ni kwa ajili ya wakristo wote

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
1,862
Reaction score
2,875
Amani iwe kwenu wapendwa!
Siku ya mwaka mpya nilikutana na Baba yangu mdogo ambaye alisomea upadre hadi level ya ushemasi na kwakweli alibakiza muda mfupi sana kupewa daraja la upadre, isivyo bahati aliacha kuendelea na wito wa upadre na hivyo aliamua kuwa mlei (mwanandoa).

Sasa juzi hiyo tukiwa tunapiga stori kuhusu mambo ya kanisa na kuhusu maandiko ya biblia pamoja na mafundisho aliniambia kitu ambacho sikukitegemea kutoka kwake. Aliniambia watumishi wa Mungu wako wa aina mbili, kwanza wako wale waliosoma BIBLE KNOWLEDGE halafu wako wale waliosoma SCRIPTURES. Nikamuuliza nini utofauti wa watu hawa?. Aliniambia kama umesoma scriptures kama yeye yaani kama mapadre wanavyosoma basi hutakuwa na complications juu ya biblia. Anasema mtu aliyesoma scriptures anafundishwa biblia kwa kina , chimbuko la andiko hilo , sababu za kuandikwa kwake na mazingira yaliyopelekea kuandikwa kwa kitabu hicho. Kwahiyo kuna vitabu viliandikwa kwa ajili ya watu wa jamii moja ya wana wa Israel mfano Walawi kitabu hicho kiliandikwa kwa watu hao, kwasababu maalum na kwa mazingira ya wakati huo. Anasema kuchukulia kitabu hicho na kukikumbatia kwa waamini wa Tanzania wa karne ya 21 si kosa lakini pia si sahihi sana. Anasema si kosa kwasababu huenda liliandikwa kuonya jamii na kuwapa muongozo ambao huenda mpaka leo unahitajika, lakini siyo sahihi kwasababu kwanza hakikulenga jamii au kanisa la sasa.

Alisema yapo mafundisho mengi ambayo wakristo wanafundishwa kutoka kwenye biblia ila hayakuandikwa kwa ajili yao. Anatolea mfano sera ya ujamaa ambao kwa wakati huo ulikuwa sahihi lakini kwasasa au kwa miaka zijazo hazitakuwa sahihi kutokana na kubadilika kwa mazingira na kutokana na kutoweka kwa walengwa. Anasema VITABU KWENYE BIBLIA VINAFAA KWA MAFUNDISHO ILA VITABU VYA AGANO JIPYA NDIVYO VYA LAZIMA KWA MKRISTO YEYOTE YULE KUVISHIKA, KUVIFUATA KWA USAHIHI WAKE NA KUVIISHI. ANASEMA UKISTO NI UFUASI WA YESU KRISTO NA HAKUNA UFUASI WA KRISTO WAKATI WA KITABU CHA MAMBO YA WALAWI. Akaendelea kusema agano jipya ndilo msingi wa imani ya kikristo na ukristo umejengwa juu ya imani ya mitume wa Yesu na manabii.

Mwisho akanimbia wale wachungaji waliosoma bible knowledge wao wamesoma biblia na namna ya kuitafsiri lakini kuna vitu vingi vya msingi hawajasoma wala kufundishwa , yaani kwa kifupi anasema wana uelewa wa kati kwenye maandiko.

Nini maoni yako.
 
Hata mimi naona hivyo.

Ila hata huko kwenye agano jipya kuna vitabu bado havifai kwa wakristo wote. Mfano nyaraka za Paulo....nyingi aliandika kulingana na makabila na tamaduni na mazingira ya wakati huo.
 
Mkuu hizo nyaraka ndizo zimeweka msingi wa kanisa au waraka upi unazungumzia?
 
kila andiko lenye pumzi ya MUNGU lafaa kwa mafundisho na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kuwaongoza,na kwa kuwaadibisha katika haki; ili kila mtu wa MUNGU awe kamili,amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema;
haya mambo yanahitaji sana maombi na ufunuo wa akili sio darasa,ikiwa hayo aliyosema yako sahihi basi Biblia yote haiko sawa,LA HASHA hakika yeye ndio hayuko sahihi kabisa;
Biblia haikuandikwa kwetu ila imeandikwa kwa ajili yetu;
 
Mkuu wewe umesoma bible knowledge au scriptures? hapo penye rangi nyekundu mbona jamaa alielezea vzr kama nilivyosema hapo juu? Jamaa anasema si kosa kufundisha watu kuhusu habari za mambo ya walawi lakini vitabu vingi vya agano la kale viliandikwa si kwa wakristo wala watu wote bali yaliandikwa kwa watu maalumu kwenye mazingira na nyakati maalumu. Jamaa anasema HAKUNA UKRISTO BILA YESU, HAKUNA KITU KWENYE UKRISTO ZAIDI YA KUFUATA MAFUNDISHO YA YESU NA MISINGI ILIYOWEKWA NA YESU PAMOJA NA MITUME WAKE. Hakatai watu kusoma biblia nzima ila kuna vitabu siyo relevant kwa wakristo.
 
Kuijua biblia haihitaji wasomi wa bible knowledge wala scriptures Ila inahitaji uongozi wa Roho mtakatifu tu na hapa hats biblia yenyewe inajishuhudia;
Najua neno hili tu,huhu Yesu alikuwepo tokea agano la kale na ndio alitoa maelekezo yote yale hivo ukisema wakristo tunatumia mafundisho ya Yesu lazima usikatae agano la kale wala kulibagua kama ulivoandika amesema;
 
Pia nakukumbusha neno 'kila andiko' litafakari utajua maana yake vizuri;
 
agano la kale kimsingi lilileta sheria na yakupasa kujua bila sheria hakuna dhambi. agano jipya limeleta uwokovu kwa njia ya NEEMA KATIKA YESU KRISTO. TORATI YOTE NA MANABII UKAMILISHO WAKE NI YESU KRISTO. AGANO LA KALE LILILETA SHERIA, LAKINI TUNAONA HAKUNA ALIYEWEZA KUOKOLEWA KWA MATENDO YA SHERIA MAANA WOTE WALITENDA DHAMBI NA KUVUNJA SHERIA. NAMNA PEKEE YA KUMKOMBOA MWANADAMU ILIBAKI KUWA NEEMA KATIKA YESU KRISTO. YESU ALIKUWEPO KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA DUNIA SO KILA UNACHOKIONA KATIKA BIBILIA NI KWA WATU WOTE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO. ACHA KUSOMA BIBILIA KAMA KITABU CHA HISTORIA
 
Kwa hiyo Mungu alishindwa kufanya watu wake waandike kitabu kimoja kwa watu wote wa zama zote?
 
"Mtu anayekubali Vipande fulani vya Biblia na kukataa Vingine anatenda kosa kubwa"
Author Simkumbuki

Si kweli hata kidogo, mazingira yalimfanya Mungu atoe sheria na taratibu kwa wana wa Israel kwa wakati huo tu na hakulenga jamii nzima ya dunia wala karne nyingi zilizokuwa zinakuja. Hapa ndipo kuna umuhimu wa kusoma scriptures. Mfano habari ya talaka, habari za kufunga, habari za kutoa sadaka za kuteketeza, habari za vyakula etc. Haya ni mafundisho na maandiko kamili ya biblia lakini zilihusu jamii ya wana wa Israeli kwa wakati na mazingira yale ndiyo maana baadaye Yesu Kristo anakuja kuyarekebisha.
 
Kuijua biblia haihitaji wasomi wa bible knowledge wala scriptures Ila inahitaji uongozi wa Roho mtakatifu tu na hapa hats biblia yenyewe inajishuhudia;
Najua neno hili tu,huhu Yesu alikuwepo tokea agano la kale na ndio alitoa maelekezo yote yale hivo ukisema wakristo tunatumia mafundisho ya Yesu lazima usikatae agano la kale wala kulibagua kama ulivoandika amesema;

Hata huyo Baba yangu mdogo Shemasi Mlei hakatai agano la kale kutumika , yeye anasema si vitabu vyote kwenye biblia ni relevant kwa wakristo wa leo japo yanaweza kutumika kufundishia. Anasema kuna vitabu viliandikwa kwa jamii fulani ya wana wa Israeli kwa wakati na mazingira hayo. Mfano kwenye biblia hasa agano la kale Mungu aliwaruhusu watu kuoa wanawake wengi wala haikuwa shida, habari za vyakula, habari za talaka, habari za kulipiza kisasi, habari za adhabu za moja kwa moja kutoka kwa Mungu etc. Hizi zilisadifu mazingira ya wakati huo na kwasasa msingi kamili wa Ukristo ni YESU na Mitume. Anasema agano jipya ni standard kwa wakristo wote duniani
 
Back
Top Bottom