Kadhi Mkuu 1
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 19,687
- 23,689
Huyo baba yako mdogo ndo maana walimtimua hawakumpa upadre.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo Mungu alishindwa kufanya watu wake waandike kitabu kimoja kwa watu wote wa zama zote?
Unaleta Udini na uchochezi. Utafutwaaaaaaaa.Amani iwe kwenu wapendwa!
Siku ya mwaka mpya nilikutana na Baba yangu mdogo ambaye alisomea upadre hadi level ya ushemasi na kwakweli alibakiza muda mfupi sana kupewa daraja la upadre, isivyo bahati aliacha kuendelea na wito wa upadre na hivyo aliamua kuwa mlei (mwanandoa).
Sasa juzi hiyo tukiwa tunapiga stori kuhusu mambo ya kanisa na kuhusu maandiko ya biblia pamoja na mafundisho aliniambia kitu ambacho sikukitegemea kutoka kwake. Aliniambia watumishi wa Mungu wako wa aina mbili, kwanza wako wale waliosoma BIBLE KNOWLEDGE halafu wako wale waliosoma SCRIPTURES. Nikamuuliza nini utofauti wa watu hawa?. Aliniambia kama umesoma scriptures kama yeye yaani kama mapadre wanavyosoma basi hutakuwa na complications juu ya biblia. Anasema mtu aliyesoma scriptures anafundishwa biblia kwa kina , chimbuko la andiko hilo , sababu za kuandikwa kwake na mazingira yaliyopelekea kuandikwa kwa kitabu hicho. Kwahiyo kuna vitabu viliandikwa kwa ajili ya watu wa jamii moja ya wana wa Israel mfano Walawi kitabu hicho kiliandikwa kwa watu hao, kwasababu maalum na kwa mazingira ya wakati huo. Anasema kuchukulia kitabu hicho na kukikumbatia kwa waamini wa Tanzania wa karne ya 21 si kosa lakini pia si sahihi sana. Anasema si kosa kwasababu huenda liliandikwa kuonya jamii na kuwapa muongozo ambao huenda mpaka leo unahitajika, lakini siyo sahihi kwasababu kwanza hakikulenga jamii au kanisa la sasa.
Alisema yapo mafundisho mengi ambayo wakristo wanafundishwa kutoka kwenye biblia ila hayakuandikwa kwa ajili yao. Anatolea mfano sera ya ujamaa ambao kwa wakati huo ulikuwa sahihi lakini kwasasa au kwa miaka zijazo hazitakuwa sahihi kutokana na kubadilika kwa mazingira na kutokana na kutoweka kwa walengwa. Anasema VITABU KWENYE BIBLIA VINAFAA KWA MAFUNDISHO ILA VITABU VYA AGANO JIPYA NDIVYO VYA LAZIMA KWA MKRISTO YEYOTE YULE KUVISHIKA, KUVIFUATA KWA USAHIHI WAKE NA KUVIISHI. ANASEMA UKISTO NI UFUASI WA YESU KRISTO NA HAKUNA UFUASI WA KRISTO WAKATI WA KITABU CHA MAMBO YA WALAWI. Akaendelea kusema agano jipya ndilo msingi wa imani ya kikristo na ukristo umejengwa juu ya imani ya mitume wa Yesu na manabii.
Mwisho akanimbia wale wachungaji waliosoma bible knowledge wao wamesoma biblia na namna ya kuitafsiri lakini kuna vitu vingi vya msingi hawajasoma wala kufundishwa , yaani kwa kifupi anasema wana uelewa wa kati kwenye maandiko.
Nini maoni yako.
Kwa nini?wewe si hauamini katika uwepo wa Mungu?haya mambo na utata wake tuachie sisi tunaoamini katika uwepo wake!!
saafi sana big pointkila andiko lenye pumzi ya MUNGU lafaa kwa mafundisho na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kuwaongoza,na kwa kuwaadibisha katika haki; ili kila mtu wa MUNGU awe kamili,amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema;
haya mambo yanahitaji sana maombi na ufunuo wa akili sio darasa,ikiwa hayo aliyosema yako sahihi basi Biblia yote haiko sawa,LA HASHA hakika yeye ndio hayuko sahihi kabisa;
Biblia haikuandikwa kwetu ila imeandikwa kwa ajili yetu;
yakupasa kujua YESU alikuja kuukomboa ulimwengu wote na siku ya mwisho atahukumu ulimwengu wote. ndani ya YESU kuna UTEULE NA UTAKATIFU na ndio maana wanaomfuata YESU jina sahihi kwao ni wateule, watakatifu au wana wa MUNGU. kusema YESU ni alikuja kwa wanaojiita wakristo tu si sawa.Hata huyo Baba yangu mdogo Shemasi Mlei hakatai agano la kale kutumika , yeye anasema si vitabu vyote kwenye biblia ni relevant kwa wakristo wa leo japo yanaweza kutumika kufundishia. Anasema kuna vitabu viliandikwa kwa jamii fulani ya wana wa Israeli kwa wakati na mazingira hayo. Mfano kwenye biblia hasa agano la kale Mungu aliwaruhusu watu kuoa wanawake wengi wala haikuwa shida, habari za vyakula, habari za talaka, habari za kulipiza kisasi, habari za adhabu za moja kwa moja kutoka kwa Mungu etc. Hizi zilisadifu mazingira ya wakati huo na kwasasa msingi kamili wa Ukristo ni YESU na Mitume. Anasema agano jipya ni standard kwa wakristo wote duniani
Kwa nini?
Wewe una mamlaka gani ya kuniambia mimi cha kufuatilia na cha kuacha?
Kama Mungu hayupo na habari za kuwepo kwake ni uongo unaoumiza watu kuanzia kuogopa moto ambao haupo, kupoteza muda mpaka kutoa sadaka ambazo zinaliwa na watu waroho tu huku watoa sadaka masikini wakiaminishwa zinafanya kazi ya Mungu, habari ya kuumulika na kuuondoa uongo huu ili watu wengi waujue na kuepukana nao kwa nini iachwe kwa wanaoamini Mungu yupo tu?
Wanaoamini Mungu yupo watamulikaje uongo wanaouamini?
Hujajibu swali langu.
Mungu wako alishindwa kufanya watu wandike kitabu kimoja kitakachokuwa na maana ile ile kwa watu wote wa miaka yote bila utata?
Naweza kujikita katika mjadala wa kitu ambacho hakipo kama daktari anayejua kwamba ugonjwa A hauna dawa, halafu akasikia matapeli wanasema wanauza dawa inayoponya ugonjwa huo.unawezaje kujikita katika mjadala wa kitu ambacho unaamini hakipo???kama unaamini yupo karibu tujadiliane!!wewe unafaa katika mada za wanaoamini Mungu yupo vs Wasioamini katika uwepo wake!!sasa hii mada ni ya wanaoamini ktk uwepo wake
Unaposoma Biblia, unatakiwa kujua ujumbe huo uliandikwa kwa nani na kwa nini uliandikwa pia ulikusudiwa kutoa somo gani kwa wakati huo na mwisho unatakiwa ujihoji kwetu sisi tunapata fundisho gani. Kwa kweli hata agano jipya liliandikwa kwa jamii ya wakati huo kutokana na hali iliyo kuwepo mfano nyaraka za Paulo ambapo analiandikia kanisaalmu ama mtu mmoja kulingana na hali iliyo kuwepo cha msingi kwetu ni kuchukua jumbe hizo zote za Biblia bila kujali ni agano gani na lujiuliza kwetu sisi tunajifunza nn. Maana kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundishoMkuu wewe umesoma bible knowledge au scriptures? hapo penye rangi nyekundu mbona jamaa alielezea vzr kama nilivyosema hapo juu? Jamaa anasema si kosa kufundisha watu kuhusu habari za mambo ya walawi lakini vitabu vingi vya agano la kale viliandikwa si kwa wakristo wala watu wote bali yaliandikwa kwa watu maalumu kwenye mazingira na nyakati maalumu. Jamaa anasema HAKUNA UKRISTO BILA YESU, HAKUNA KITU KWENYE UKRISTO ZAIDI YA KUFUATA MAFUNDISHO YA YESU NA MISINGI ILIYOWEKWA NA YESU PAMOJA NA MITUME WAKE. Hakatai watu kusoma biblia nzima ila kuna vitabu siyo relevant kwa wakristo.
Mkuu wewe umesoma bible knowledge au scriptures? hapo penye rangi nyekundu mbona jamaa alielezea vzr kama nilivyosema hapo juu? Jamaa anasema si kosa kufundisha watu kuhusu habari za mambo ya walawi lakini vitabu vingi vya agano la kale viliandikwa si kwa wakristo wala watu wote bali yaliandikwa kwa watu maalumu kwenye mazingira na nyakati maalumu. Jamaa anasema HAKUNA UKRISTO BILA YESU, HAKUNA KITU KWENYE UKRISTO ZAIDI YA KUFUATA MAFUNDISHO YA YESU NA MISINGI ILIYOWEKWA NA YESU PAMOJA NA MITUME WAKE. Hakatai watu kusoma biblia nzima ila kuna vitabu siyo relevant kwa wakristo.
Hata kama haamini katika uwepo wa mungu,bado ana haki ya kuhoji kuhusu huyo mungu.wewe si hauamini katika uwepo wa Mungu?haya mambo na utata wake tuachie sisi tunaoamini katika uwepo wake!!
Na mpaka sasa hajanijibu.Hata kama haamini katika uwepo wa mungu,bado ana haki ya kuhoji kuhusu huyo mungu.
Unachotakiwa wewe ni kumpa majibu kwa swali alilouliza.
Uenda kupitia majibu yako yasiyo na mashaka wala kujipinga akaamua kubadili msimamo na kumuamini mungu.
Huyo baba yako mdogo ndo maana walimtimua hawakumpa upadre.
Unaleta Udini na uchochezi. Utafutwaaaaaaaa.
Huyo padre ana kila sababu kutoendelea kuwa kama Mtumishi maana ufaham wake ni mdogo sana,
Biblia nzima inamsema Yesu kikubwa ni ufahamu wako
yakupasa kujua YESU alikuja kuukomboa ulimwengu wote na siku ya mwisho atahukumu ulimwengu wote. ndani ya YESU kuna UTEULE NA UTAKATIFU na ndio maana wanaomfuata YESU jina sahihi kwao ni wateule, watakatifu au wana wa MUNGU. kusema YESU ni alikuja kwa wanaojiita wakristo tu si sawa.
Hata kama haamini katika uwepo wa mungu,bado ana haki ya kuhoji kuhusu huyo mungu.
Unachotakiwa wewe ni kumpa majibu kwa swali alilouliza.
Uenda kupitia majibu yako yasiyo na mashaka wala kujipinga akaamua kubadili msimamo na kumuamini mungu.
Uelekeo wake ni upi?mkuu,jamaa ana tatizo akikuta mada za kiroho zenye muelekeo flani anazipindisha na kuzisukumia katika muelekeo wake
Na kamwe usimjibu atakavyo.ndio maana simjibu atakavyo
Kwanini kuuliza kwake iwe ni kuvuruga mada na si kutaka kujua tu?Ni mvurugaji mada kama wavurugaji wengine