Si kila kitabu kwenye Biblia ni kwa ajili ya wakristo wote

Si kila kitabu kwenye Biblia ni kwa ajili ya wakristo wote

Me pia nakubaliana na Padre, japo kuna watu wanabisha,biblia imegawanyika 1.Vitabu vya historia 2.Vitabu vya sheria 3.Vitabu vya Nyimbo na Zaburi 4.Vitabu vya Injili
No1.nistory ya imani ilikotoka wala haukuwa ukristo. kuna mambo mabaya mengi yalifanywa na waaminio ambayo hatupaswi kuiga kutoka kwao
No2.Hz zililetwa kutokana na ugumu wa mioyo yao, infact walikuwa hawatii
No3.Zilikuwa nyimbo za kusifu na hekma za watu wale
No4.Ndo wokovu wenyewe ambao Yesu alikuja kutuonyesha
 
"Mtu anayekubali Vipande fulani vya Biblia na kukataa Vingine anatenda kosa kubwa"
Author Simkumbuki

Huenda una maana ya andiko hilo hapo chini Ufu 22:18- 19

Ninamwonya kila mtu anayesikia maneno ya unabii wa kitabu hiki: Ikiwa mtu yeyote ataongeza chochote kwa haya, Mungu atampa mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.

19 Na ikiwa mtu yeyote akitoa sehemu yoyote ya maneno ya kitabu hiki cha unabii, Mungu ataondoa sehemu ya urithi wa mtu huyo katika mti wa uzima na sehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyo habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
 
Mwandishi wa thread amekosa namna nzuri ya uandishi wa Kichwa cha thread yake inasound weird kwamba hayo maandiko hayana manufaa yoyote kwa wakristo jambo ambalo si sawa kwa maana tunajua ya kwamba kila andiko linalopatikana katika biblia lafaa kwa mafundisho ikiwa ni sheria nyimbo nyaraka au zaburi, Mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano yakaandikwa ili kutuonya sisi tuliofikiwa na miisho ya zamani.
 
Mkuu wewe umesoma bible knowledge au scriptures? hapo penye rangi nyekundu mbona jamaa alielezea vzr kama nilivyosema hapo juu? Jamaa anasema si kosa kufundisha watu kuhusu habari za mambo ya walawi lakini vitabu vingi vya agano la kale viliandikwa si kwa wakristo wala watu wote bali yaliandikwa kwa watu maalumu kwenye mazingira na nyakati maalumu. Jamaa anasema HAKUNA UKRISTO BILA YESU, HAKUNA KITU KWENYE UKRISTO ZAIDI YA KUFUATA MAFUNDISHO YA YESU NA MISINGI ILIYOWEKWA NA YESU PAMOJA NA MITUME WAKE. Hakatai watu kusoma biblia nzima ila kuna vitabu siyo relevant kwa wakristo.
we we iman gan 2anzie hapo yawezekana n hbar z kuhadthiwa n hujui lolote nd maan bdo n ucku wa kza kwako ,na km n mkrstu una2mia muda gani walau kw wki kusoma hyo bible yenyewe? n km unasoma je unaielewa? kabla y kuanzisha mjadala
 
Mbona hutoi sadaka za kuteketezwa kama walawi(makuhani? walivyofanya?
Kuna mambo ambayo Kristo aliyatimiza na hilo ulilosema ni mojawapo maana hayo Makuhani walifanya kumuwakilisha Kristo mwenyewe,kwahiyo siwezi kufanya mile ambacho Kristo ametimiza;
 
All in all .... Bible iko weak kumuongoza mwanadamu ....vitu vingi haijavielezea
 
Methali 13:24
"Yeye asiyetumia fimbo hamtaki mwanawe, bali yeye ampendaye humrudi mapema."
Wanasoma, ndio maana wanakula kitimoto na kuoa mke mmoja tu tofauti na Wayahudi
 
Ila wakristo ni wastaarabu sana ...

Unaweza ukawa unachoma biblia huku wanakuangalia tu ..

Watasema amechanganyikiwa huyo "tumsamehe hajui atendalo"

Ila sasa kule uchome kitabu cha mud uone
 
Ila wakristo ni wastaarabu sana ...

Unaweza ukawa unachoma biblia huku wanakuangalia tu ..

Watasema amechanganyikiwa huyo "tumsamehe hajui atendalo"

Ila sasa kule uchome kitabu cha mud uone
Hamna uchungu nacho, kila siku mnakibadilisha maandishi
 
Amani iwe kwenu wapendwa!
Siku ya mwaka mpya nilikutana na Baba yangu mdogo ambaye alisomea upadre hadi level ya ushemasi na kwakweli alibakiza muda mfupi sana kupewa daraja la upadre, isivyo bahati aliacha kuendelea na wito wa upadre na hivyo aliamua kuwa mlei (mwanandoa).

Sasa juzi hiyo tukiwa tunapiga stori kuhusu mambo ya kanisa na kuhusu maandiko ya biblia pamoja na mafundisho aliniambia kitu ambacho sikukitegemea kutoka kwake. Aliniambia watumishi wa Mungu wako wa aina mbili, kwanza wako wale waliosoma BIBLE KNOWLEDGE halafu wako wale waliosoma SCRIPTURES. Nikamuuliza nini utofauti wa watu hawa?. Aliniambia kama umesoma scriptures kama yeye yaani kama mapadre wanavyosoma basi hutakuwa na complications juu ya biblia. Anasema mtu aliyesoma scriptures anafundishwa biblia kwa kina , chimbuko la andiko hilo , sababu za kuandikwa kwake na mazingira yaliyopelekea kuandikwa kwa kitabu hicho. Kwahiyo kuna vitabu viliandikwa kwa ajili ya watu wa jamii moja ya wana wa Israel mfano Walawi kitabu hicho kiliandikwa kwa watu hao, kwasababu maalum na kwa mazingira ya wakati huo. Anasema kuchukulia kitabu hicho na kukikumbatia kwa waamini wa Tanzania wa karne ya 21 si kosa lakini pia si sahihi sana. Anasema si kosa kwasababu huenda liliandikwa kuonya jamii na kuwapa muongozo ambao huenda mpaka leo unahitajika, lakini siyo sahihi kwasababu kwanza hakikulenga jamii au kanisa la sasa.

Alisema yapo mafundisho mengi ambayo wakristo wanafundishwa kutoka kwenye biblia ila hayakuandikwa kwa ajili yao. Anatolea mfano sera ya ujamaa ambao kwa wakati huo ulikuwa sahihi lakini kwasasa au kwa miaka zijazo hazitakuwa sahihi kutokana na kubadilika kwa mazingira na kutokana na kutoweka kwa walengwa. Anasema VITABU KWENYE BIBLIA VINAFAA KWA MAFUNDISHO ILA VITABU VYA AGANO JIPYA NDIVYO VYA LAZIMA KWA MKRISTO YEYOTE YULE KUVISHIKA, KUVIFUATA KWA USAHIHI WAKE NA KUVIISHI. ANASEMA UKISTO NI UFUASI WA YESU KRISTO NA HAKUNA UFUASI WA KRISTO WAKATI WA KITABU CHA MAMBO YA WALAWI. Akaendelea kusema agano jipya ndilo msingi wa imani ya kikristo na ukristo umejengwa juu ya imani ya mitume wa Yesu na manabii.

Mwisho akanimbia wale wachungaji waliosoma bible knowledge wao wamesoma biblia na namna ya kuitafsiri lakini kuna vitu vingi vya msingi hawajasoma wala kufundishwa , yaani kwa kifupi anasema wana uelewa wa kati kwenye maandiko.

Nini maoni yako.
Mwamposya sidhani amepitia hata Sunday School
 
Back
Top Bottom