Si kila kitabu kwenye Biblia ni kwa ajili ya wakristo wote

Unaleta Udini na uchochezi. Utafutwaaaaaaaa.
 
wewe si hauamini katika uwepo wa Mungu?haya mambo na utata wake tuachie sisi tunaoamini katika uwepo wake!!
Kwa nini?

Wewe una mamlaka gani ya kuniambia mimi cha kufuatilia na cha kuacha?

Kama Mungu hayupo na habari za kuwepo kwake ni uongo unaoumiza watu kuanzia kuogopa moto ambao haupo, kupoteza muda mpaka kutoa sadaka ambazo zinaliwa na watu waroho tu huku watoa sadaka masikini wakiaminishwa zinafanya kazi ya Mungu, habari ya kuumulika na kuuondoa uongo huu ili watu wengi waujue na kuepukana nao kwa nini iachwe kwa wanaoamini Mungu yupo tu?

Wanaoamini Mungu yupo watamulikaje uongo wanaouamini?

Hujajibu swali langu.

Mungu wako alishindwa kufanya watu wandike kitabu kimoja kitakachokuwa na maana ile ile kwa watu wote wa miaka yote bila utata?
 
Huyo padre ana kila sababu kutoendelea kuwa kama Mtumishi maana ufaham wake ni mdogo sana,
Biblia nzima inamsema Yesu kikubwa ni ufahamu wako
 
Huyo padre ana kila sababu kutoendelea kuwa kama Mtumishi maana ufaham wake ni mdogo sana,
Biblia nzima inamsema Yesu kikubwa ni ufahamu wako
 
saafi sana big point
 
yakupasa kujua YESU alikuja kuukomboa ulimwengu wote na siku ya mwisho atahukumu ulimwengu wote. ndani ya YESU kuna UTEULE NA UTAKATIFU na ndio maana wanaomfuata YESU jina sahihi kwao ni wateule, watakatifu au wana wa MUNGU. kusema YESU ni alikuja kwa wanaojiita wakristo tu si sawa.
 
unawezaje kujikita katika mjadala wa kitu ambacho unaamini hakipo???kama unaamini yupo karibu tujadiliane!!wewe unafaa katika mada za wanaoamini Mungu yupo vs Wasioamini katika uwepo wake!!sasa hii mada ni ya wanaoamini ktk uwepo wake
 
Naweza kujikita katika mjadala wa kitu ambacho hakipo kama daktari anayejua kwamba ugonjwa A hauna dawa, halafu akasikia matapeli wanasema wanauza dawa inayoponya ugonjwa huo.

Ingawa dawa haipo, daktari huyu anayejua dawa haipo anaingia katika mjadala kuionesha jamii kwamba kuamini kitu ambacho hakipo kwamba kipo kunaweza kuwa hatari.

Kwa sababu watu ambao wangeweza kujikinga wasipate ugonjwa A wanaweza kupunguza kujikinga wakijua kuna dawa.

Pia watu wanaweza kuibiwa hela na matapeli kwa kuuziwa kitu kinachoitwa dawa ya ugonjwa A wakati si dawa.

Zaidi, uongo ni uongo tu. Mtu anayejua huu ni uongo hahitaji sababu zaidi kuupinga.

Mungu wenu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, utukufu wote na uoendo wote, mnayesema kaumba dunia hii inayowezekana kuwa na mabaya mengi, hayupo.

Dhana ya kuwepo kwake ina contradiction.

Kusema yupo ninsawa na kusema pembetatu yenye pembe nne katika Euclidean geometry.

Au kusema katika base ten math square root ya 2 ni 10.

Contradictions.
 
Unaposoma Biblia, unatakiwa kujua ujumbe huo uliandikwa kwa nani na kwa nini uliandikwa pia ulikusudiwa kutoa somo gani kwa wakati huo na mwisho unatakiwa ujihoji kwetu sisi tunapata fundisho gani. Kwa kweli hata agano jipya liliandikwa kwa jamii ya wakati huo kutokana na hali iliyo kuwepo mfano nyaraka za Paulo ambapo analiandikia kanisaalmu ama mtu mmoja kulingana na hali iliyo kuwepo cha msingi kwetu ni kuchukua jumbe hizo zote za Biblia bila kujali ni agano gani na lujiuliza kwetu sisi tunajifunza nn. Maana kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho
 
wewe si hauamini katika uwepo wa Mungu?haya mambo na utata wake tuachie sisi tunaoamini katika uwepo wake!!
Hata kama haamini katika uwepo wa mungu,bado ana haki ya kuhoji kuhusu huyo mungu.

Unachotakiwa wewe ni kumpa majibu kwa swali alilouliza.

Uenda kupitia majibu yako yasiyo na mashaka wala kujipinga akaamua kubadili msimamo na kumuamini mungu.
 
Na mpaka sasa hajanijibu.

Anaamini Mungu yupo.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote, ujuzi wote, utukufu wote. Aliyeumba ulimwengu huu unaoruhusu mabaya mengi. Matetemeko ya ardhi. Magonjwa. Vita etc.

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya?

Mungu huyu alishindwa kufanya watu waandike kitabu ambacho kitaeleweka bila utata kwa watu wote, muda wote?

Hajajibu maswali.
 
Huyo baba yako mdogo ndo maana walimtimua hawakumpa upadre.

Wapi nimesema walimtimua? nimesema aliacha mwenyewe. Halafu ungetuambia kosa lake kwenye hayo mazungumuzo yetu siyo kumhukumu tu bila sababu
 
Huyo padre ana kila sababu kutoendelea kuwa kama Mtumishi maana ufaham wake ni mdogo sana,
Biblia nzima inamsema Yesu kikubwa ni ufahamu wako

Mkuu huyo kasoma SCRIPTURES katika ukweli na uhalisi wake, kasoma historia ya biblia na mazingira ya uandishi wake. Anajua anachokisema, tena anatushangaa sana tunavyohangaika na habari nyingine
 
Mkuu hiyo habari za Yesu kuja kwa ajili wa wakrito nani kasema?
 
Hata kama haamini katika uwepo wa mungu,bado ana haki ya kuhoji kuhusu huyo mungu.

Unachotakiwa wewe ni kumpa majibu kwa swali alilouliza.

Uenda kupitia majibu yako yasiyo na mashaka wala kujipinga akaamua kubadili msimamo na kumuamini mungu.

mkuu,jamaa ana tatizo akikuta mada za kiroho zenye muelekeo flani anazipindisha na kuzisukumia katika muelekeo wake,ndio maana simjibu atakavyo!Ni mvurugaji mada kama wavurugaji wengine wanaotumia mbinu ya kuingizia mada juu ya mada.Ni hilo tu!Unadhani sipo sahihi mpaka hapa??
 
kama ndivyo basi Yesu Kristo angekuja na amri mpya za Mungu kwa sababu zile za agano la kale ziliwahusu waisrael tu tena wakiwa safarini na ningetegemea baada ya kuwa wamefika basi wangepewa amri mpya kwa sababu safaria ilikuwa imeisha. Huyo shemasi mlei hapo hayuko sahihi hata kidogo, haya mambo hayahitaji shule pekee bali zaidi Roho wa Mungu kukuongoza
 
mkuu,jamaa ana tatizo akikuta mada za kiroho zenye muelekeo flani anazipindisha na kuzisukumia katika muelekeo wake
Uelekeo wake ni upi?

Kwanini kuzipindisha na kuzisukumia mada kwenye uelekeo wake kuwe na tatizo?

ndio maana simjibu atakavyo
Na kamwe usimjibu atakavyo.

Mjibu kwa kadri ya ukweli wa mambo ulivyo.
Ni mvurugaji mada kama wavurugaji wengine
Kwanini kuuliza kwake iwe ni kuvuruga mada na si kutaka kujua tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…