Si kila kitabu kwenye Biblia ni kwa ajili ya wakristo wote

Labda hana majibu sahihi.
 
Mi muislam hainihusu ngoja nikae pembeni mchambane wenyewe
 
Amen.... Huyo ni ROHOMTAKATIFU amekufunulia siri hii
 
Kwa mtazamo wake huo lazima angeacha wito.
 
Hata mimi naona hivyo.

Ila hata huko kwenye agano jipya kuna vitabu bado havifai kwa wakristo wote. Mfano nyaraka za Paulo....nyingi aliandika kulingana na makabila na tamaduni na mazingira ya wakati huo.
Mnapotoshwa
 
Hata mimi naona hivyo.

Ila hata huko kwenye agano jipya kuna vitabu bado havifai kwa wakristo wote. Mfano nyaraka za Paulo....nyingi aliandika kulingana na makabila na tamaduni na mazingira ya wakati huo.
Kikubwa ni kuacha dhambi , ukiacha dhati utachagua kitabu cha kusoma
 
Aisee mbona ambapo tuna IQ ndogo na akili average hatutakaa tukanyage mbinguni..

Mbinguni wataenda watu wenye akili,wenye uweze wa kusoma biblia kwa akili fulani mahususi na uelewa fulani hivi special..Sisi wengine tusiokua na akili hizo imekula kwetu..

Na kama hatuna hela ya kununua na kusoma biblia tutaenda motoni milele

Na kama tumezaliwa Siberia huko au Uchina huko wasiojua nini kitu Yesu Kristo,tutaenda motoni milele,wakati hata sikua na uwezo wa kuchagua kuzaliwa huko,nilijikuta tu nimezaliwa huko bila uamuzi wangu binafsi

Etc

Etc

Etc

Huyu mungu wa wakristo ni baguzi la kutupwa,na wakristu wote ni watu wa ajabu hawafai kukaa hapa duniani kabisa...
 
Yesu alikuja kutimiza torati na sio kuiondoa usipotoshe ndugu nakukaribisha tujifunze kwa unyeyekevu huku tukiomba Roho mtakatifu atufundishe neno lake
 
Yaaap anaye tafsiri biblia kwa kigezo cha roho mt. Huwa wanatafsiri kwa mizuka.....hisia....kiasi kwamba hadi muumini anaingiwa na Yale maneno Na anasema ni roho wa Mungu.....kumbe mchungaji ameweza kugusa roho yako kwa sauti za hisia na ameweza Kuhusanisha biblia na matqtizo yako.
.

.

.ndoa....

Vyuma kukaza....


Uchawi..
.


Kukosa kazi.....

Madeni.......


Elimu.

Hapa ndo utaona watu wanavyo anguka.


Lakn mapadre wapo tofauti sana.
Anafanya uelewe sio Kuku umiza kihisi
 
Kwa uhalisia nadhani huyo jamaa hana upadre wowote.
Kwanini nasema Hivyo?
Bible Knowledge ni Ufahamu Wa Biblia
Scripture ni Maandiko.
Biblia ni mkusanyiko wa maandiko fulani..............
Sasa itakuwa ajabu leo Bible knowledge na Scripture vikawa masomo mawili tofauti.

Pia Hiyo Bible Knowledge sio Somo la Wachungaji Ni somo kama masomo mengine tu kama History/Mathematics Biology/Islamic Studies etc
Mimi Nimesoma Shule za Kidini(Za Wakristo)
Bible Knowledge kwa Kidato cha kwanza na Pili NI Lazima Kusoma Sio Option (Kwa Shule za Kikristo)
NIlipofika Advance nikasoma Divinity
Na Wachungaji hawana somo hilo zaidi zaidi unakutana nalo katika madarasa ya Wainjilisti nalo haliwi zito kama vile shule za Sekondari.
Mtoa Uzi Next Time Uwe makini acha kuleta Mikanganyiko Hapa.
Unajua Mada kama hizi inakupasa uwe hata wewe unaifahamu kwa upana zaidi mbali na masimulizi tu unayopatiwa huko lakini uweze kupata namna ya kuileza na kutetea ili usilete maswali zaidi kwa wasomaji.
Si vema kuleta hoja ambayo huna ujuzi nayo na kisha ikaleta ukakasi na mambo tofauti kwa wasomaji

Naambatanisha Ni Uzi Huu hapa ukibonyeza ukaone masomo yanayotambuliwa Na Serikali Ambayo Ni Ya Dini pamoja na ambayo Sio Ya Dini BONYEZA HAPA
 
Sasa kile cha makabila yetu kiko wapi? Kile cha utamaduni wetu kiko wapi? Mtoa mada anadhani mtu wake ndiye peke aliyesoma maandiko kwa kina. Anapotofautisha scriptures yaani maandiko na Bible Knowledge yaani elimu ya Biblia ana maana gani? Wanaosoma Bible Knowledge ama Theology au Teolojia (Elimu ya Mungu) na fani zingine husika hurejea maandiko ya Biblia. Maandiko ndiyo rejea kuu (Primary Source). Bible Knowlege ni hatua ya mwanzo katika sayansi ya kutafsiri Maandiko (Hermeneutics). Ili kupata kiini ama kina cha habari na tafsiri bora unafanya biblical exegesis yaani uchanganuzi wa kina wenye kuhusisha mambo mengi yakiwemo historia ya kifungu, walengwa, maana ya asili ya mwandishi na mazingira ya wakati huo; ndipo unafanya matumizi ya ujumbe uliomo katika zama za sasa, walengwa wa sasa katika lugha ya wahusika na desturi zao za sasa. Biblia ni kwa ajili ya vizazi vyote ina tafsiri moja bali matumizi (application) nyingi. Mfano kut 18:19 Yethro ampa Musa sifa za kuweka wakuu wa watu wamsaidie kazi. Sifa hizo zinafanana na sifa za Mzee wa Kanisa katika Tito 1:5-9 na sifa za Askofu katika 1 Tim 3:1-5. Leo Januari 2018 twaweza pia kutumia baadhi ya sifa kama inavyotuhusu. Mfano mzuri ni kuwa kiongozi asiwe mwenye kupenda pesa ama mwenye kutafuta mapato ya aibu. Tutaitumia sifa hiyo leo pia maana inahusika.Taz Kut 18:21, 1Tim 3:7 na Tit 1:3
 
Pengine huyu ndugu yako aliyekuwa anasomea upadri angemalizia masomo yake ndio angeweza kukupa picha kamili.. Biblia iko wazi kuwa kila neno lenye pumzi ya Mungu la faa kwa mafundisho, kuonya na kuelekeza..Hakuna namna unayoweza kuisoma na kuielewa biblia bila msaada wa Roho Mtakatifu ambaye ndiye mwalimu wa kweli akuongoze, vimginevyo pamoja na hoja yake bado hakuna jambo lolote linalomshinda Mungu kutumia kitabu chochote katika Biblia kutimiza makusudi yake kwetu.
 
Mbona hutoi sadaka za kuteketezwa kama walawi(makuhani? walivyofanya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…