Si sahihi kumpa maagizo Waziri Mkuu hadharani, si kila kiongozi anaweza kupewa maagizo hadharani

Anachokifanya Makonda ndicho haswa alichoteuliwa kukifanya.

Makonda ni mithili ya udongo, unamfinyanga vile unataka awe.

Makonda ni mouthpiece ya waliomteua ili aongee yale wasioweza kuyaongea kwa wanaotakiwa kufikishiwa ujumbe.
Na mimi nimepata hisia kama hii, kwamba ni vigumu Makonda kuanza kusema maneno haya bila kupata ruhusa ya aliyemteua.

Kitaratibu, Samia alitakiwa kuunda upya baraza la mawaziri alipokuwa rais, na ama kumteua upya Majaliwa kuwa Waziri Mkuu, ama kumuondoa na kumuweka mtu mwingine. Samia hakufanya hivyo.

Mpaka leo Samia amekuwa na Waziri Mkuu wa urithi ambaye kwa upande mmoja hajamuondoa kwenye hiyo nafasi, na kwa upande mwingine anaonesha kwamba "huyu si Waziri Mkuu niliyemteua mimi, nimeachiwa tu na Magufuli".

Anamfanyia mpaka hila za kumteulia Makamu Waziri Mkuu akionesha kwamba Majaliwa amepwaya.

Hamkupata message pale?

Waziri Mkuu alishahujumiwa hata kabla ya uteuzi wa Makonda.

Makonda amewekwa kimkakati kumuumbua zaidi tu.

Makonda kasema si yeye anayesema hayo, ni chama. Sasa unafikiri Makonda anaweza kuwa na ujasiri wa kusema haya ni maneno ya chama bila kupata ruhusa ya Samia? Kwa Waziri Mkuu?

CCM wanajivua nguo hadharani. Viongozi hawasikilizani. Maneno ambayo yalitakiwa kutolewa kwenye vikao vya ndani yanaanikwa wazi. Watu (CCM) wamestukia uchaguzi unakuja, wanatafuta mbuzi wa bangusilo kumtoa kafara tayari.
 

Ila wabongo bwana ni bendera fuata upepo. Kwa hivyo hujui shughuli za makamu wa Rais Kikatiba?. Unadhani akina Mpango hawawezi kufanya kazi?. Makonda ni mtu anayependa madaraka na anapenda awe juu ya wote. Umesahau hata akiwa mkuu wa mkoa aliwahi kujiita mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa Tanznaia na akawa anapambana na UKUTA wa CHADEMA kwa kutangaza usafi nchi nzima?. Muogope Sana Makonda sio wa kuchekea.
 
Mama Samiah naye mnafiki, alisahuriwa na TLS ateue Waziri Mkuu Mpya Kama ni awamu mpya akakataa, Sasa hivi anatumia njia ndefu kumtoa, mara huku dotto kule Makonda, kesho sijui atakuja na Nini.
 
Hakuna waziri Muongo,Tapeli,Mnafiki na Anajifanya mstaarabu kama Majaliwa!

Bashite inapaswa akaze hapo hapo!

..uongo, utapeli, na unafiki, wa Majaliwa ni kwa ajili ya kuisadia Ccm.

..Bashite huenda anataka kuwa Waziri Mkuu baada ya Majaliwa.
 
Na mimi nimepata hisia kama hii, kwamba ni vigumu Makonda kuanza kusema maneno haya bila kupata ruhusa ya aliyemteua.
Hasa ikizingatiwa Makonda alishachafuka na kila aina ya scandal kipindi chote alichokuwa ndani ya siasa na alishakubali majaaliwa yake kuwa amekuwa irrelevant pale alipokuwa nje ya teuzi na ndio maana alikaa kimya na hata matumizi yake ya social media ilikuwa ni ku post mambo ya Mungu, kumaanisha ametubu na amerudi kwa Mungu.

Katika aklil ya kawaida ilipaswa arudi akiwa mpole na muungwana, hasa kipindi cha awali cha uteuzi wake aendane na aina ya mtu aliejinasibisha baada ya kuwa kwake nje ya siasa/teuzi.

Haingii akilini mtu ambae alishakuwa na maadui lukuki wa kisiasa aje ghafla na kuanza kutengeneza maadui wapya. Ni wazi ana kila baraka na ulinzi wa aliemueka hapo.

Katika siasa huwa hakuna kauli ya bahati mbaya, kila kauli huwa na dhamira ya aidha kuleta athari fulani ama kufikisha ujumbe fulani.

Alipokuwa anazungumza kuhusu wastaafu kutulia alitaja majina ya mwenyekiti, makamo nk yote kwa heshima na nyadhifa zao ila alipotaja jina la Chongolo hakutaja wadhifa wake, alisema Chongolo tu, hii ni ishara kuwa nafasi aliyonayo ni ya kiini macho, ana nguvu kubwa mno ya kuweza ku by pass wengi hata wale wanaopaswa kuwa juu yake.
Haitokuwa ajabu huko mbeleni akimshurtisha Katibu Mkuu wake mbele ya halaiki.

Ieleweke tu kuwa Makonda hakuteuliwa kwa bahati mbaya na hakuna analosema kwa utashi wake, kila kitokacho kinywani mwake ni part and parcel ya kile alichoagizwa afanye kwa kiini macho cha Ukatibu Uenezi.

Makonda ni puppet mzuri wa kuweza kutimiza dhamira za wenye madaraka japo katika hiyo process na yeye hutimiza dhamira zake pia. Tutasikia na kuona mengi.
 
Serikali haijawahi kuwa kubwa zaidi ya chama tawala!
 
Kinachokuja na kufuata, atatoa order kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wake wa chama na kujitetea kuwa ni "maagizo ya Chama Cha Mapinduzi....!!"

Kama kuna abishae, nyie subirini tu mtaona ufyatu wa huyu kichwa maji...

Na tafsiri yake ni kuwa, siku zote mpumbavu huwa haachi asili yake...
Your browser is not able to display this video.


Na kwa sababu kichaa huyu kapewa kisemeo, basi wategemee kumwagiwa upupu wa kila aina na kwa hakika kabisa, Kwa ulimi wake huyu, atachoma na kuteketeza msitu wote..

Na Kwa sababu hii huko CCM watavurugana mpaka watavurugika na kufa na kuzikana wenyewe...!!
 
Maoni na mtazamo wako ni mzuri na tunauheshimu..

Lakini sijaiona mantiki ya kumwita mwenzio ndugu Toxic Concotion "kenge" ulipokuwa unajaribu kum - address maoni yako..

Likely hukumsoma ukamwelewa kwa sababu mantiki ya maoni yake juu ya Paul Makonda haina tofauti sana na ya kwako..
 
Inafikirisha.
 
simlaumu sana maana huwa tunatofautiana upeo wa uelewa wa mambo. Kuna kipindi katika maisha tunajikuta tunatengeneza maadui kwa dhana ya kuwa tumekosewa kutotambua kuwa uelewa wetu duni ndio umetengeneza uadui usiokuwepo.

Kikubwa ni uhai tu haya mengine yanapita. Kuitwa kenge hakubadishi kuwa kwangu binadamu.

Nashukuru kwa concern yako Chief🙏
 
Kwani muheshimiwa Katelephone amemkosea nini Sa100? Mara paap Naibu Waziri Mkuu kawekewa. Haijapoa Makonda kaingia na jumbe za mwanzo kabisa zinamlenga direct WM Majaliwa. Mwanakwetu Majaliwa nini shida na kama unaona mambo hayaendi waachie ukubwa wao wasijekukuchafua kwa skendo za hovyo hao.
 

Ni kweli Makonda anazingua, lakini huyo waziri mkuu anayeingia madarakani kwa njia za kishenzi acha apewe makavu peupe. Fuatilia huyo Majaliwa alikuwa mbunge kwa mara ya pili kwa njia gani. Kama unatumia njia za kishenzi kupata madaraka, usijilize ukipewa maagizo kwa njia za kihuni.
 
Cheo Cha PM Kiko kwa mujibu ya katiba ya JMT.Cheo Cha katibu wa uenezi wa Chama Cha siasa wanakijua wanachama wenyewe na katiba yao.Kwa hiyo PM ni bosi wake anapaswa kuheshiwa kwa sababu kabeba wanacha na wasio wanachama
 
Siamini kuwa umeandika haya- totally out of context
 
Cheo Cha PM Kiko kwa mujibu ya katiba ya JMT.Cheo Cha katibu wa uenezi wa Chama Cha siasa wanakijua wanachama wenyewe na katiba yao.Kwa hiyo PM ni bosi wake anapaswa kuheshiwa kwa sababu kabeba wanacha na wasio wanachama
Mkuu na wewe umesemamo
 
Makonda hana adabu kabisa
 
kwa vile hajaenda kama Gaidi Mbowe mvumilieni tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…