Si sahihi kumpa maagizo Waziri Mkuu hadharani, si kila kiongozi anaweza kupewa maagizo hadharani

Anachofanya Makonda ni Kutoa ishara ya Ukubwa wa Cheo chake, na kweli mliokua hamjui cheo cha Makonda sasa mtakua mmeanza elewa bwa mkubwa kapewa Kitengo.
 
Ukiona jambo hilo ndugu Pascal Mayalla kakaa kimya basi ujue kwa mujibu wa taratibu za chama, Mwenezi hajachemka🤣🤣
 

Nilisema hili na ninarudia tena, katika nchi yetu Waziri mkuu hapewi hashima anayostahili kupatiwa kutikana na mamlaka yake. Hii inatokana na wivu wa kiutawala, sina hakika sana kama marais wetu wamekuwa 'wakiwaacha' mawaziri wakuu waheshimiwe.
 
Asante sana mkuu.
 
Naona unateseka tu makonda awezi kukurupuka kabla ajasema walishaonana kwa siri na mawaziri wote na kashaambiwa aongee vipi
 
Chama ndio kimeunda serikali na siyo serikali iliyounda chama,. serikali haiwezi kuwa kubwa kuliko chama hata siku moja.Nenda kasome katiba ujielimishe kidogo maana naona uelewa wako siyo mkubwa sana kwenye haya mambo. Huwezi kuwa Rais kama huna chama cha siasa au hujapendekezwa na chama cha siasa. Kwa hiyo chama kinachokupa ridhaa ya kugombea ni kikubwa kuliko serikali utakayo iunda wewe baada ya kuchaguliwa. Wakati wa uchaguzi chama ndicho hutafuta kura kwa wananchi kwa kunadi ilani yake ambayo ndio hutekelezwa baada ya kupewa ridhaa na wananchi kupitia sanduku la kura. Chama kinaweza iagiza serikali kufanya jambo lolote lile na kuhitaji mrejesho wa utekelezaji wake.
 

View: https://www.instagram.com/reel/CzJfL93IbJU/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Aliyetoa maelekezo sio Makonda ni Chama.

PM akiagiza Huwa hawasemi Majaliwa kaagiza Bali Waziri Mkuu Kwa niaba ya Serikalini nk so Makonda Yuko sahihi kiitifaki.
 
Jiulize kwani kuna vikao vya ccm vimekaa vikatoa hizo kauli anazoeneza Bashite PM Albert?
Kama HAPANA basi fahamu kuwa hayo ni maagizo toka kwa alomteua!
Huyo Majaliwa... achague Moja... Apokee maagizo ayafanyie kazi au abwage manyanga!
Akikomaa watamuongezea Naibu mwingine
 
Wahenga wanasema kulikuwa na 'H' Sita
Tatu zomekufa na Tatu hazifi mpaka kiama
Haya, Huba na Huruma zimekufa
Zilizobaki tatu ni Hila, Hadaa na Husda
 
Hilo li jamaa sijui lina siri gani na mama mpaka halijafunguliwa mashitaka kama Sabaya na badala yake limeteuliwa.
WACHA LIKIGAWE CHAMA
 
Mpole kabisa pamoja na kuwa uwezekano wa dua zako kutimia ni 0p% katiba ya jmt haimpi makamu wa rais hayo meno uyawazayo, kazi kubwa ya makamu wa rais ni kukata utepe tena wa miradi midogo midogo na kukagua bei ya vyakula tandale.
 
Kwani Katibu Mkuu wa CCM yupo wapi,mpaka subordinate wake Makonda ndo ampe Prime Minister Maagizo ? Hapa kuna kitu hakijakaa sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…