Tetesi: Si shwari, rais Magufuli kutangaza mazito August 31 siku moja kabla ya UKUTA

Tetesi: Si shwari, rais Magufuli kutangaza mazito August 31 siku moja kabla ya UKUTA

Kwa maneno mengine, anatangaza hali ya hatari?

So watanzania tusiende kwenye shughuli zetu za uzalishaji mali?

Tanzania ya viwanda inafikiwa mapema iwezekanavyo.
Huenda akafanya hivyo lakini hana uhalali huo kikatiba kwa hali ilivyo sasa. Na litakuwa ni kosa kubwa kisiasa na kiuchuni kuipeleka nchi kati hali mbaya hivyo. Ni sawa na kujiwekea mwenyewe vikwazo vya kiuchumi.
 
Natabiri UKUTA kuahirishwa hadi hapo itakapotangazwa tena ikiwa ni Ukuta part 2
 
Rais HAYUPO juu ya katiba
Ningemuelewa zaidi kama August hiyo angetangaza kuwa Bunge litarekebisha katiba
Iwe marufuku vyama kukutana baada ya uchaguzi
Zaidi ya hapo ni upuuzi tu atakao ongea
 
Natabiri UKUTA kuahirishwa hadi hapo itakapotangazwa tena ikiwa ni Ukuta part 2
UKUTA haitafanikiwa sababu WATZ wameisha mshtukia Mbowe
Mbowe anaitumia CHADEMA kujiimarisha yy tu na watu wake wa karibu
Lkn sababu za kuandamana ni legit sana
Magufuli ni dikteta uchwara
 
Nyie akina mama wanaume hatuwahitaji.Kaa nyumbani usubiri uone wanaume wanairudisha Demokrasia.
 
CHADEMA wapo serious sana,watu hawajajua haya,maagizo yaliyotolewa kwa viongozi wa chini ni mazito,na wameambiwa aneyeona atashindwa aachie ngazi mapema
 
Siasa uchwara za maji taka kamwe hazitaruhusiwa milele. Mikutano ya siasa safi inayofuata kanuni, taratibu na sheria za nchi hazijawahi kuzuiwa. Wewe ulishaona wapi siasa za kumwita rais aliyechaguliwa na majority, hao minority walioshindwa wanamuita uchwara na kuandamana nchi nzima wakimwita hivyo. Kama si upunguani ni nini? Lazima cha mtema kuni wakionje angalao kidogo ili waone kautamu kake.

Tarehe 1 Sep wanaotaka kuonja hako kautamu kake jitokezeni tu wala haina haja ya kuja kubwabwaya huku Jf sasa hivi. Tarehe 2 tunawasubiri mje mtusimulie hako ka utamu ka mtema kuni.

Kwa Akili yako kidogo machafuko yakitokea wewe utabaki kuwa salama !?.Unafikiri haujulikani !?..
 
YAANI WANATAKA KUIGOMEA TUSIIPATE HAKI YETU YA KIMSINGI YA KIKATIBA...!/
 
Cuf wanajielewa hawataki kuburuzwa kama majizi Chadema wanavyoburuzwa na mfalme Mbowe
 
C wawaache tu wafanye.hakuna haja ya ubabe ubabe
 
Sishabikii lakini ningeliomba Mungu amjalie rais wangu Hekima, maarifa na uvumilivu ka baba wa wote. Ajiulize, atapungua nini kama akiwaruhusu wanasiasa wenzake kufanya hiyo mikutano popote wanapopenda?? Ningelitamani atambue kuwa kuwanyima uhuru huu wa kikatiba sio kuwaminya bali kuwashupaza.
Mtu yeyote anayeshangilia maneno ya ukali anayoyatumia rais kuwajibu wapinzani nadhani anajilisha upepo. Kwetu wanasema; Moto wa mpasuko huleta madhara kwa jirani pia. Weye CCM je unakaa mbinguni au ni hapa hapa duniani patakapotokea hiyo fujo? Risasi haimjui mlengwa, ikikukuta ni bahati mbaya. Watakapokuwa wanakimbizwa huko mitaani, wanaweza kuingia kwako na katika harakati za kuwatoa ukajikuta na weye ccm umeumizwa au kuuawa.
Tusishabikie shari, tutafute amani kwa gharama yeyote tu, Ni kaushauri tu
 
Kweli Chadema Kiboko! Kampeni nyingi zimepita, lakini UKUTA unawakosesha usingizi watawala. Natabiri UKUTA utaahirishwa ili kulinda Maisha ya watu.
 
Habari nilizopata kutoka jikoni zinasema kuwa siku ya August 31 mwaka huu, siku moja kabla ya UKUTA rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kutangaza mambo mazito kwa watanzania.

Inasemekana kuwa rais anatarajiwa kuliweka jeshi la polisi katika tahadhari kubwa huku kukiwa na mazuio kadhaa yatakayo ambatana na tahadhari hiyo kwa jeshi la polisi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi kunatarajiwa kuwa na operesheni nzito ya jeshi la polisi na huenda kukatumika nguvu kubwa zaidi katika kukabiliana na Chadema nchi nzima.

Aidha nimedokezwa kuwa ofisi zote za Chadema nchini zinatarajiwa kuzingirwa na jeshi la polisi siku hiyo ya september moja.

#UKUTA for Democracy!

Ukuta ni jaribio la UHAINI, vijana kataeni kuwa mbuzi wa kafara wa Mbowe na Lowassa
 
Back
Top Bottom