Siasa ni mchezo unaohitaji precision ya hali ya juu katika kuucheza. Godbless Lema kafanya kosa kubwa la kiufundi kama alivyofanya Hezekiah Wenje

Siasa ni mchezo unaohitaji precision ya hali ya juu katika kuucheza. Godbless Lema kafanya kosa kubwa la kiufundi kama alivyofanya Hezekiah Wenje

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
4,249
Reaction score
11,592
Husemwa kuwa, siasa ni mchezo mchafu...

Lakini mimi nasema hivi: Sio kweli, bali siasa ni Sanaa na profesheni halali na ya kawaida kama profesheni zingine katika maisha mfano ualimu, udaktari, unasheria nk. Shida ni kuwa, siasa imebeba watu wachafu kimaadili kwa zaidi ya 95% ndani yake na hawa kwa kiasi Kikubwa ndio wanaodhibiti mifumo ya kisiasa yote. Aidha, katika siasa ndimo shetani Ibilisi alipoweka makao makuu yake na hawa watu walio wachafu wa kimaadili ndani ya siasa ni wafuasi na watumishi wa huyu shetani Ibilisi baba wa uovu wote duniani. Na mtu yeyote safi kimaadili anayepingana na mifumo ya watu hawa, sharti awe consistent, patient, asiyekata tamaa, mwenye nguvu ya Mungu Yahweh ndani yake lakini aliye tayari ku - endure pains and sufferings sometimes kabla ya Mungu kumsaidia kushinda...

Ndiyo, no matter how these evil people powerful are they, lakini kamwe hawajawahi kuandikiwa kuishinda haki na nuru. Haki ndaima huishinda dhuluma na Nuru daima hulishinda Giza...


Tanzania inao watu safi kimaadili, wapenda haki, walio wazi na huru wasiofungwa na vishawishi na mawazo machafu ya watu wachafu wa kimaadili na wanaoweza kuongoza vita ya kupambania HAKI na UHURU wa kweli ktk taifa letu. Mojawapo wa watu hawa ambaye ameshajitanabaisha waziwazi huku akipitia mateso makubwa kwa sababu ya HAKI ni Tundu Mughway Lissu...

====================
KUHUSU GODBLESS LEMA
​
Hakuna shaka kuwa, Godbless Lema anajua kuwa amekikosea chama chake. Ameisaliti HAKI na atavuna alichokipanda very soon...

Inawezekana kabisa kuwa, labda kweli alikuwa na genuine grievances zake dhidi ya wenzake au chama. Hata hivyo, angeanza kwanza kutueleza hizo grievances zake na kwa namna gani zimeshundwa kushughulikiwa na chama kabla ya kutoka kulaumu wenzake ndani ya chama huku naye akiwa sehemu ya uongozi uliofanya maamuzi anayoyalalamikia...

Kwahiyo, shida yake kubwa ni kuwa, ametumia njia isiyo sahihi kuziwasilisha hizo grievances zake na hivyo kuvunja kanuni, sheria na katiba ya chama chake...

Na kwa sababu hii, his offences are punishable according to the Party constitution..
===================​
Hapa aombe tu CHADEMA wasichukue hatua za kumpiga chini. Kinyume chake ni kuwa, if they do, he's gone forever....

Pua hakijawahi kukizidi kichwa. Lema ni pua, CHADEMA ni kichwa. Mtu hawezi kuwa juu ya taasisi...

CCM pamoja na kuwa chama cha wahuni na hayawani wakubwa, lakini hakuna mtu anaweza kufanya kama alivyofanya Godbless Lema dhidi ya CHADEMA na akabaki free akitamba mitaani. Watamkata kichwa haraka sana hata awe very influential kama Dr Emmanuel Nchimbi (the latest example...)

Hata kama Godbless Lema akiamua haraka haraka kutangaza kujivua nafasi zote za uongozi na kujifuta uanachama mwenyewe, then Lema hamtamsikia tena katika ulingo wa siasa...

He's gone, just like Hezekiah Wenje..

Godbless Lema na Hezekiah Wenje pamoja na Mch Peter Msigwa walikosea kusoma alama za nyakati ktk maamuzi yao...

Wenje is down and gone, sijui kama atakujaga kusimama ktk ulingo siasa tena zilizomweka kwenye peak na kisha ku - earn trust kwa umma...

Mch Peter Msigwa kidogo aanguke moja kwa moja na kupotea. Thank God, amekuwa na moyo wa ujasiri kukiri makosa yake hadharani na kurudi tena ulingoni. Bado anasuasua lakini, hopefully atasimama tena...

Tunaye Godbless Lema. Ni Bahati mbaya kuwa, he is falling in the same trap. Na sbb ni moja tu, TAMAA YA PESA NA KUKOSA UVUMILIVU WA KUSUBIRI WAKATI MWAFAKA...

I real feel sorry for Godbless Lema...
 
Lema ni Tapeli mkubwa sana. Ni Tapeli kama akina Halima Mdee. Walikisaliti chama kipindi kinawahitaji. Leo Halima Mdee ni historia.
Ameshindwa kuubeba umaarufu wa kisiasa alionao...

Ni bahati mbaya, umaarufu ndio huo huo adui zake wanautumia kumzika ktk kaburi la kisiasa..

And honestly, Godbless Lema hana lolote akiwa nje ya CHADEMA sawa na Luhaga Mpina asivyokuwa na lolote nje ya CCM...

Hawa wote wawili Luhaga Mpina na Godbless Lema hawana swaga za kisiasa kiasi ambacho wanapojenga hoja zao, basi mtu unatamani kuendelea kuwasikiliza bila kuchoka...

Hebu mtu aniambie, nani huwa anamwelewa Luhaga Mpina huko aliko anapoongea...?

Ndivyo itakavyokuwa kwa Godbless Lema nje ya CHADEMA....
 
Ameshindwa kuubeba umaarufu wa kisiasa alionao...

Ni bahati mbaya, umaarufu ndio huo huo adui zake wanautumia kumzika ktk kaburi la kisiasa..

And honestly, Godbless Lema hana lolote akiwa nje ya CHADEMA sawa na Luhaga Mpina asivyokuwa na lolote nje ya CCM...

Hawa wote wawili Luhaga Mpina na Godbless Lema hawana swaga za kisiasa kiasi ambacho wanapojenga hoja zao, basi mtu unatamani kuendelea kuwasikiliza bila kuchoka...

Hebu mtu aniambie, nani huwa anamwelewa Luhaga Mpina huko aliko anapoongea...?

Ndivyo itakavyokuwa kwa Godbless Lema nje ya CHADEMA....
Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom