Siasa pembeni, Polepole Vs Nape? Nani kichwa

Siasa pembeni, Polepole Vs Nape? Nani kichwa

..huwezi kusema mtu fulani ni " think tank. "

..think tank maana yake ni TAASISI inayofanya utafiti, na kutoa ushauri, kuhusu sera mbalimbali.

..ukiniuliza mimi, kwa hapa Tz, taasisi kama ESRF [ Economic and Social Research Foundation], naweza kuiita think tank / policy institute ya masuala ya sera za uchumi na kijamii.

..kwenye nchi za wenzetu kuna think tanks za masuala mbalimbali kama Foreign Policy, masuala ya ulinzi , masuala ya fedha na uchumi, etc etc.

cc Nguruvi3, Chige, Kiranga, Erythrocyte , MALCOM LUMUMBA
Mkuu JokaKuu, sisi watanzania bado tunaamini kwamba mtu mmoja anaweza kuwa taasisi ndiyo maana huwa inatuwia vigumu sana kung'amua mambo ya msingi kama haya. Hivyo usishangae kabisa, hata kiuongozi sisi bado tuko kwenye awamu ile ambayo mwanafalsafa wa Ujerumani Max Weber aliwahi kusema "A Charismatic Leadership", mambo kama zidumu fikra za mwenyekiti na raisi ana nia njema.

Mtoa mada hajakosea kabisa kwasababu tofauti kabisa na sehemu nyingine duniani ambako sera za kiulinzi hutungwa, hutengenezwa na kuchakatwa na haya matanuri ya fikra (Think Tanks), Tanzania na sehemu nyingi za Afrika sera kubwa za nchi (Strategic Policies) huwa zinatungwa na kuchakatwa na mtu mmoja tu halafu taasisi nyingine za nchi zinafanya kutekeleza. Ndiyo maana kila Raisi akiondoka yanakuja mambo mapya tu, hata kama ya hovyo.

Hivyo unapozungumzia Think Tank unamaanisha diverse intellectual minds (Erudite) working in unison as a corporate creature in churning social, economic, security and political affairs through advanced research. Lengo hapa ni, helping a government or an organisation to make an informed and pragmatic decision. Huku kwetu Humphrey Polepole na Nape Nnauye ni think tanks, siwalaumu kwa nafasi yao kuna chembe ya ukweli,...
 
Mtoa mada unatakiwa kuomba radhi kwa kumkosea H.Polepole.
Kumlinganisha Nape na Polepole ni sawa na kulinganisha mtoto wa CHEKECHEA (NN) na Mwanafunzi wa Form Six(HP)
Ni lini uliwahi kumsikia Nape anatoa Elimu yoyote au ufafanuzi wowote wa kimantiki juu ya jambo lolote lile.
Kwa kifupi, HP shule ipo kichwani lakini NN ni empty set.
 
Mkuu JokaKuu, sisi watanzania bado tunaamini kwamba mtu mmoja anaweza kuwa taasisi ndiyo maana huwa inatuwia vigumu sana kung'amua mambo ya msingi kama haya. Hivyo usishangae kabisa, hata kiuongozi sisi bado tuko kwenye awamu ile ambayo mwanafalsafa wa Ujerumani aliwahi kusema "A Charismatic Leadership", mambo kama zidumu fikra za mwenyekiti na raisi ana nia njema.

Mtoa mada hajakosea kabisa kwasababu tofauti kabisa na sehemu nyingine duniani ambako sera za kiulinzi hutungwa, hutengenezwa na kuchakatwa na haya matanuri ya fikra (Think Tanks), Tanzania na sehemu nyingi za Afrika sera kubwa za nchi (Strategic Policies) huwa zinatungwa na kuchakatwa na mtu mmoja tu halafu taasisi nyingine za nchi zinafanya kutekeleza. Ndiyo maana kila Raisi akiondoka yanakuja mambo mapya tu, hata ya hovyo.

Hivyo unapozungumzia Think Tank unamaanisha diverse intellectual minds (Erudite) working in unison as a corporate creature in churning social, economic, security and political affairs through advanced research. Lengo hapa ni, helping a government or an organisation in making informed and pragmatic decision. Huku kwetu Humphrey Polepole na Nape Nnauye ni think tanks, siwalaumu kwa nafasi yao kuna chembe ya ukweli,...
Umemaliza mkuu MALCOM LUMUMBA .
Kongole sana.
 
..huwezi kusema mtu fulani ni " think tank. "

..think tank maana yake ni TAASISI inayofanya utafiti, na kutoa ushauri, kuhusu sera mbalimbali.

..ukiniuliza mimi, kwa hapa Tz, taasisi kama ESRF [ Economic and Social Research Foundation], naweza kuiita think tank / policy institute ya masuala ya sera za uchumi na kijamii.

..kwenye nchi za wenzetu kuna think tanks za masuala mbalimbali kama Foreign Policy, masuala ya ulinzi , masuala ya fedha na uchumi, etc etc.
Upo sahihi kabisa mkuu , maelezo yako yanajitosheleza

Najiuliza hivi hawa wawili , Nape na Polepole kwanini wanadhaniwa hata kuwa 'thinkers'
Tumeona wote na utendaji wao.

Nape : Huyu ni mwasisi wa hujuma dhidi ya vyombo vya habari. Ni wakati akiwa Waziri, Nape alizuia Bunge Live kwa hoja ya gharama. Nape hakujua Tanzania ya leo si ile ya Nnauye
Leo Nape haongelei gharama za TV zinazotumika ''kuongea au kuapisha makatibu kata'' .
Madhara ya sheria alizosimamia ni makubwa hadi leo na itachukua muda sana kuyaondoa

PolePole: Kiongozi mwandamizi wa awamu ya 5 anayeamini katika katiba.Matendo yake ya hayaungi mkono hilo. Mfano, alikuwepo katiba inavunjwa kuhusu mikutano ya hadhara.
Juzi kaulizwa hana jibu anasema ni mila na desturi. Hivi mila na desturi zinaongoza nchi!
Hakutaja kifungu cha Katiba, sheria zitokazonazo, kanuni au kifungu cha mila na desturi kama kipo. Katiba inavunjwa alikuwepo na alishiriki halafu anaamini katika katiba !

Kwasasa ni Mbunge, sheria zilizoundwa kutoka katiba zinavunjwa kwa wale Wabunge 19, yupo kimya akiaminisha umma ni muumini wa katiba.

Polepole alishiriki mchakato wa katiba, alizunguka nchi nzima akisema ya 1977 ni mbovu tunahitaji mpya. Alipoteuliwa akabadilika hataki katiba anataka uchumi.

Juzi kaulizwa kasema katiba inaandikwa na Rais anayeondoka. Haijulikani kaiokota wapi hiyo
Huyu anaingiaje kundi la ''thinker' kama lipo
 
watanzania tunaamini kwamba mtu mmoja anaweza kuwa taasisi ndiyo maana huwa inatuwia vigumu sana kung'amua mambo ya msingi kama haya. Hivyo usishangae kabisa, hata kiuongozi sisi bado tuko kwenye awamu ile ambayo mwanafalsafa wa Ujerumani aliwahi kusema "A Charismatic Leadership", mambo kama zidumu fikra za mwenyekiti na raisi ana nia njema.
Miaka 5 iliyopita imethibitisha kauli yako bila shaka.
Mtoa mada hajakosea kabisa kwasababu tofauti kabisa na sehemu nyingine duniani ambako sera za kiulinzi hutungwa, hutengenezwa na kuchakatwa na haya matanuri ya fikra (Think Tanks), Tanzania na sehemu nyingi za Afrika sera kubwa za nchi (Strategic Policies) huwa zinatungwa na kuchakatwa na mtu mmoja tu halafu taasisi nyingine za nchi zinafanya kutekeleza. Ndiyo maana kila Raisi akiondoka yanakuja mambo mapya tu, hata kama ya hovyo.
Ni chagize kidogo tu. Tulikuwa na sera ya kurekebisha uchumi wakati wa Mkapa. JK akaja na Elimu kwanza kabla ya kuhamia Kilimo kwanza kwa mabdiliko ya Mawaziri wakuu. Baada ya hapo tukawa na Viwanda. Sera zote hizo zimetokea katika miaka 15 hadi 20. Je, kulifanyika tathmini ya kujua mafanikio na mapungufu ya kila sera? Na kwanini kila kiongozi ana sera zake na si sera za Taifa?
Hivi leo tuna sera gani?

Hivyo unapozungumzia Think Tank unamaanisha diverse intellectual minds (Erudite) working in unison as a corporate creature in churning social, economic, security and political affairs through advanced research. Lengo hapa ni, helping a government or an organisation to make an informed and pragmatic decision. Huku kwetu Humphrey Polepole na Nape Nnauye ni think tanks, siwalaumu kwa nafasi yao kuna chembe ya ukweli,...
Ahsante na hiyo ndio maana ya 'Think tank'
 
Mama D, nimempenda bure Polepole! Haiwezekani watu waseme uongo kuhusu JPM na asijitokeze mtu kueleza ukweli. JPM aliisaidia nchi hii kiasi cha kupoteza uhai wake, lakini michadema ya humu na wapuuzi akina Zitto wanaona ndiyo kumkomoa. Naona mwanzo mzuri kwa Polepole hasa aliposema mama alikuwa mshauri mkuu na leo anamkana kama Petro kwa Yesu! Hii haikubaliki na Mpango alivyo mnafiki ananyamaza wakati alikuwa waziri wa mipango na fedha. It’s a shame
[emoji16][emoji16] Kwamba alipoteza uhai kwa sababu ya nchi?[emoji1][emoji1]
 
Ili uwe think tank kwanza lazima uwe una msimamo,huyumbishwi kisiasa hata upepo uvume mkali.
Sasa huyo kibwengo anakosa sifa hiyo, wakat wa JK alikuwa kindaki ndaki kariba mpya, alipopewa v8 akayakana mawazo yake yooote ya awali.
Ni ngumu sana kupata mwanasiasa mwenye msimamo Africa kwa sababu ya njaa
Njaa mbaya Sana.
 
Nawaona tu wote kama wasaka tonge.

Wangekuwa cream wangeambulia hata uteuzi mmojawapo.
 
Back
Top Bottom