Siasa pembeni, Polepole Vs Nape? Nani kichwa

Mkuu JokaKuu, sisi watanzania bado tunaamini kwamba mtu mmoja anaweza kuwa taasisi ndiyo maana huwa inatuwia vigumu sana kung'amua mambo ya msingi kama haya. Hivyo usishangae kabisa, hata kiuongozi sisi bado tuko kwenye awamu ile ambayo mwanafalsafa wa Ujerumani Max Weber aliwahi kusema "A Charismatic Leadership", mambo kama zidumu fikra za mwenyekiti na raisi ana nia njema.

Mtoa mada hajakosea kabisa kwasababu tofauti kabisa na sehemu nyingine duniani ambako sera za kiulinzi hutungwa, hutengenezwa na kuchakatwa na haya matanuri ya fikra (Think Tanks), Tanzania na sehemu nyingi za Afrika sera kubwa za nchi (Strategic Policies) huwa zinatungwa na kuchakatwa na mtu mmoja tu halafu taasisi nyingine za nchi zinafanya kutekeleza. Ndiyo maana kila Raisi akiondoka yanakuja mambo mapya tu, hata kama ya hovyo.

Hivyo unapozungumzia Think Tank unamaanisha diverse intellectual minds (Erudite) working in unison as a corporate creature in churning social, economic, security and political affairs through advanced research. Lengo hapa ni, helping a government or an organisation to make an informed and pragmatic decision. Huku kwetu Humphrey Polepole na Nape Nnauye ni think tanks, siwalaumu kwa nafasi yao kuna chembe ya ukweli,...
 
Mtoa mada unatakiwa kuomba radhi kwa kumkosea H.Polepole.
Kumlinganisha Nape na Polepole ni sawa na kulinganisha mtoto wa CHEKECHEA (NN) na Mwanafunzi wa Form Six(HP)
Ni lini uliwahi kumsikia Nape anatoa Elimu yoyote au ufafanuzi wowote wa kimantiki juu ya jambo lolote lile.
Kwa kifupi, HP shule ipo kichwani lakini NN ni empty set.
 
Umemaliza mkuu MALCOM LUMUMBA .
Kongole sana.
 
Upo sahihi kabisa mkuu , maelezo yako yanajitosheleza

Najiuliza hivi hawa wawili , Nape na Polepole kwanini wanadhaniwa hata kuwa 'thinkers'
Tumeona wote na utendaji wao.

Nape : Huyu ni mwasisi wa hujuma dhidi ya vyombo vya habari. Ni wakati akiwa Waziri, Nape alizuia Bunge Live kwa hoja ya gharama. Nape hakujua Tanzania ya leo si ile ya Nnauye
Leo Nape haongelei gharama za TV zinazotumika ''kuongea au kuapisha makatibu kata'' .
Madhara ya sheria alizosimamia ni makubwa hadi leo na itachukua muda sana kuyaondoa

PolePole: Kiongozi mwandamizi wa awamu ya 5 anayeamini katika katiba.Matendo yake ya hayaungi mkono hilo. Mfano, alikuwepo katiba inavunjwa kuhusu mikutano ya hadhara.
Juzi kaulizwa hana jibu anasema ni mila na desturi. Hivi mila na desturi zinaongoza nchi!
Hakutaja kifungu cha Katiba, sheria zitokazonazo, kanuni au kifungu cha mila na desturi kama kipo. Katiba inavunjwa alikuwepo na alishiriki halafu anaamini katika katiba !

Kwasasa ni Mbunge, sheria zilizoundwa kutoka katiba zinavunjwa kwa wale Wabunge 19, yupo kimya akiaminisha umma ni muumini wa katiba.

Polepole alishiriki mchakato wa katiba, alizunguka nchi nzima akisema ya 1977 ni mbovu tunahitaji mpya. Alipoteuliwa akabadilika hataki katiba anataka uchumi.

Juzi kaulizwa kasema katiba inaandikwa na Rais anayeondoka. Haijulikani kaiokota wapi hiyo
Huyu anaingiaje kundi la ''thinker' kama lipo
 
Miaka 5 iliyopita imethibitisha kauli yako bila shaka.
Ni chagize kidogo tu. Tulikuwa na sera ya kurekebisha uchumi wakati wa Mkapa. JK akaja na Elimu kwanza kabla ya kuhamia Kilimo kwanza kwa mabdiliko ya Mawaziri wakuu. Baada ya hapo tukawa na Viwanda. Sera zote hizo zimetokea katika miaka 15 hadi 20. Je, kulifanyika tathmini ya kujua mafanikio na mapungufu ya kila sera? Na kwanini kila kiongozi ana sera zake na si sera za Taifa?
Hivi leo tuna sera gani?

Ahsante na hiyo ndio maana ya 'Think tank'
 
[emoji16][emoji16] Kwamba alipoteza uhai kwa sababu ya nchi?[emoji1][emoji1]
 
Njaa mbaya Sana.
 
Soon watachukua card .....jeuri yake tutaiona
 
Nawaona tu wote kama wasaka tonge.

Wangekuwa cream wangeambulia hata uteuzi mmojawapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…