Siasa, unafiki na usanii: Ufaulu wa kidato cha nne mwaka 2023 umejificha ndani ya divisheni 4

Siasa, unafiki na usanii: Ufaulu wa kidato cha nne mwaka 2023 umejificha ndani ya divisheni 4

Ccm wameingiza siasa kila sehemu, Michezo siasa, dini siasa, elimu siasa, miundombinu siasa, yaani kila sehemu siasa.Nawashangaa vijana wanaopewa 20k ku push agenda ambazo wenywe zinawaumiza na ndugu zao.
 

S4213 MARIAN BOYS' SECONDARY SCHOOL​


DIVISION PERFORMANCE SUMMARY


S4213 MARIAN BOYS' SECONDARY SCHOOL



DIVISION PERFORMANCE SUMMARY


SEX
I
II
III
IV
0
F​
0​
0​
0​
0​
0​
M​
96​
0​
0​
0​
0​
T​
96​
0​
0​
0​
0​


S0248 MARIAN GIRLS' SECONDARY SCHOOL​


DIVISION PERFORMANCE SUMMARY

SEX
I
II
III
IV
0

F​
64​
17​
0​
0​
0​

M​
0​
0​
0​
0​
0​

T​
64​
17​
0​
0​
0​
Kanisa Moja Takatifu La Mitume
 
So, mafundi ni watu wajinga wajinga?
Elewa nilichoandika..Hawa madogo wengi wao hawawezi kurisiti mitihani,Wanamaliza form four na elimu ya kujumlisha maeneo na vipeo..matokeo yao hayaqualify hata kuingia kwenye certificates,ahueni yao ingekuwa at least vyuoni vya ufundi wajifunze skills za kujipatia kipato lakini hata hivyo vyuo ni vichache sana. Wapi nimetaja mafundi ni wajinga?
 
Ulitaka wengi wapate Divisheni One???? Sijakuelewa..
Hiyo ni Statistical Distribution table.. ambayo ni Normal hapo
Hujanielewa bado. Nimesema kwamba ufaulu umejificha kwenye divisheni foo. Kumbuka hata hao maelfu ya wanafunzi wanaopata divisheni foo, huhesabika kwamba wamefaulu wakati kiuhalisia divisheni foo haina maana yoyote.

Hapa ndipo utapeli wa serikali unapoanzia. Wanajua fika kwamba wanafunzi wanaopata divisheni 1 mpaka 3 wakijumlshwa wote hawawezi kufika 20% ya wanafunzi wote. Kwa hiyo, serikali inatumia hilo kundi la divisheni foo kuwahadaa wapigakura kisiasa.
 
Wewe Mzazi mtoto wako amefeli.. unailaumu Serikali...
Weww ulichukua hatua gani kumsaidia huyo mtoto tokea akiwa Form one.. mfdno Kukaa nae na kummsisitiza kuhusu elimu; kumnunulia Vitabu vya ziada; Kumtafutia remedial class
Unabaki kulia lia tu Serikali impe mtoto wako Ufaulu
Mimi nimelipa kodi ili serikali iwanunulie watoto wangu vitabu na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia lakini serikali haijatimiza majukumu yake ipasavyo. Ulitegemea nimfundishe mwanangu mimi mwenyewe wakati nalipa kodi au nifanyeje?
 
Ndugu watanzania, tuamke kumekucha! Tuamke tupiganie haki yetu ya msingi ya kupewa elimu bora na sio bora elimu. Leo wakati katibu mtendaji wa NECTA anawasilisha matokeo nimemsikiliza kwa makini sana. Amedai eti ufaulu wa mwaka 2023 umepanda kwa 0.87% ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2022.

Baada ya kusikiliza matokeo yaliyowasilishwa, nimeingia kwenye mtandao kujiridhisha kama alichosema katibu kinaakisi kupanda ufaulu au la. Nimegundua serikali imejificha kwenye kichaka cha siasa ndio maana kila siku mambo yanaenda ovyo lakini watanzania hawajali. Wamekaa kimya kama mabubu kana kwamba kila kitu kiko sawa.

Serikali inaficha uovu wake wa kuua elimu ya watanzania kwenye siasa za majitaka. Zamani NECTA walikuwa hawatoi matokeo ya jumla na ya kipuuzi kama haya wanayotoa sasa. Walilazmishwa kubadili mfumo kisiasa ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Kwa mfano, siku za nyuma wanafunzi walikuwa wanachaguliwa kuingia kidato cha kwanza kwa kuangalia jumla ya alama ambazo kila mwanafunzi amepata.

Kipindi hicho nafasi za sekondari zilikuwa chache, hivyo ushindani ulikuwa mkubwa. Pia mitihani ilikuwa migumu sana. Kwa mfano, kwa upande wa shule za msingi kulikuwa na mkusanyiko wa masomo matatu tu yaani Lugha, Hisabati na Maarifa, na kila somo lilichukua jumla ya alama 50. Hivyo, jumla ya alama za juu ilikuwa 150.

Haikuwa ajabu mwanafunzi kupata alama 145 akakosa nafasi ya kwenda sekondari. Siku hizi utakuta mwanafunzi kapata alama 11 lakini anachaguliwa kwenda sekondari kwa kisingizio cha kwamba amepata wastani wa D! Hii ni nchi ya ajabu sana. Ndio maana serikali imefanya kila njia kuongeza mafumbo kwenye elimu ili kuficha udhaifu wa kushuka kwa kiwango cha elimu na ufaulu katika nchi hii.

Nikirejea kwenye hoja yangu ya msingi, ukiangalia matokeo ya shule za serikali (shule za kata) ambazo NECTA inasema ufaulu wake umepanda, ni ubatili mtupu. Nimejaribu kuchukua shule chache kama mfano. Hebu tazama hiki kichekesho, ucheke uongeze siku za kuishi:
View attachment 2882622
View attachment 2882624View attachment 2882625View attachment 2882628
Ukihesabu idadi ya wanafunzi walioangukia kwenye ufaulu wa daraja la nne ni zaidi ya 95% ya wanafunzi wote nchi nzima. Kumbe ufauulu ulioongezeka ni wa divisheni foo! Sote tunafahamu kuwa ufaulu wa divisheni foo hauna maana yoyote. Mwanafunzi aliyepata divisheni foo hastahili hata kupewa cheti. Akafanyie nini hicho cheti? Hakina maana yoyote ile.

Hivi serikali sikivu ya CCM mnamdanganya nani na haya matokeo yenu ya mchongo ambayo kila mwaka ufaulu wake unapanda? Haya ndiyo maajabu ya serikali hii ya kusadikika iliyojaa hadaa, usanii na unafiki kila mahali.
""Mwanafunzi aliyepata divisheni foo hastahili hata kupewa cheti. Akafanyie nini hicho cheti? Hakina maana yoyote ile.""""
ww nadhani ni mjinga zaidi
 
1706208582747.png
 
Divisheni foo ina faida gani katika nchi hii? Buku saba zimekuharibu ubongo.
Unataka kila mtu awe na one halfu iweje? udhani inchi ilio jaa wezi hivi ones zitasaidia??
Haya mtu kapata one kaenda kusoma sociology, wa four karnda certficate na diploma ya Clinical medicine,mechanics au hot culture sasa hapa nan bora???

shida iliopo vyuo vikuu theory ni nyingi kuliko practicals, Vyuo havina vifaa kabisa atleast kwa afya wanajitaidi na upande wakilimo SUA

IZO VISION HAPO HAO WATU WANATEGEMEANA SANA
 

S4213 MARIAN BOYS' SECONDARY SCHOOL​


DIVISION PERFORMANCE SUMMARY


S4213 MARIAN BOYS' SECONDARY SCHOOL



DIVISION PERFORMANCE SUMMARY


SEX
I
II
III
IV
0
F​
0​
0​
0​
0​
0​
M​
96​
0​
0​
0​
0​
T​
96​
0​
0​
0​
0​


S0248 MARIAN GIRLS' SECONDARY SCHOOL​


DIVISION PERFORMANCE SUMMARY

SEX
I
II
III
IV
0

F​
64​
17​
0​
0​
0​

M​
0​
0​
0​
0​
0​

T​
64​
17​
0​
0​
0​
Hayo matokeo ya marian na boys girls umeyatoa wapi mkuu?


Screenshot_20240125_220053_Chrome.jpg


Screenshot_20240125_215852_Chrome.jpg
 
Unataka kila mtu awe na one halfu iweje? udhani inchi ilio jaa wezi hivi ones zitasaidia??
Haya mtu kapata one kaenda kusoma sociology, wa four karnda certficate na diploma ya Clinical medicine,mechanics au hot culture sasa hapa nan bora???

shida iliopo vyuo vikuu theory ni nyingi kuliko practicals, Vyuo havina vifaa kabisa atleast kwa afya wanajitaidi na upande wakilimo SUA

IZO VISION HAPO HAO WATU WANATEGEMEANA SANA
Wewe unashauri nini kifanyike kukabiliana na hii hadaa ya serikali?
 
Back
Top Bottom