Siasa, unafiki na usanii: Ufaulu wa kidato cha nne mwaka 2023 umejificha ndani ya divisheni 4

Siasa, unafiki na usanii: Ufaulu wa kidato cha nne mwaka 2023 umejificha ndani ya divisheni 4

Kabisa mkuu. Tukumbuke watoto hawa wengi ni under age (miaka 15, 16 na 17). Serikali ndio inahusika kuua future yao halafu wanaturudishia sisi wazazi tuwapeleke wapi? Serikali hii ina mambo ya kipumbavu sijapata kuona.
Hao wanao maliza chuo kikuu,pia mnarudishiwa vile vile..huwa mnawapeleka wap? Maana ajira hakuna
 
Kwanini serikali isifute shule za kata na kuboresha shule hizi kwa manufaa ya wote?

Hapa sio kuzifuta shule za kata, nikujua nani anahitaji elimu gani?

Sio kila mtoto anahitaji hizi mbilinge za masomo ya namna hii.

Pia waboreshe upatikanajibwa walimu na miundombinu mingine.
 
Ccm ni JANGA
CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.
 
Hao wanao maliza chuo kikuu,pia mnarudishiwa vile vile..huwa mnawapeleka wap? Maana ajira hakuna
Your argument is unfounded. Kwa hiyo kwa sababu hakuna ajira unashauri serikali itoe elimu ya ovyo ili wanafunzi wengi wafaulu kwa ufaulu wa divisheni foo ya serikali?
 
Your argument is unfounded. Kwa hiyo kwa sababu hakuna ajira unashauri serikali itoe elimu ya ovyo ili wanafunzi wengi wafaulu kwa ufaulu wa divisheni foo ya serikali?
Iwe One ama Foo..hizo elimu hazina impact zozote kwenye jamii kwa dunia ya sasa. Elimu za kukariri zimepitwa na wakati. Ndo maana tunahitaji mabadiliko kwenye mfumo wa elimu uendane na mahitaji sahihi
 
Wewe unashauri nini kifanyike kukabiliana na hii hadaa ya serikali?
waongeze walimu mashuleni na usahili wa walimu uwe na interview sio wa makusanyo,mfano ujerumani kazi ya heshima na ngumu kuipata ni ualimu hapo taifa linatakiwa liweke mdhaha kando kabisa.
Waboreshe miumdobinu ya ufundishaji kulingana na technologia, mitaala iwe inapitiwa kila baada ya miak miwili au mitatu.

Pia hapa secondary combi zianzie form Two
art
business
Language
Aplied science
Health science
Enviromental science
Profesional zianzie mbali maana wahenga husema samaki mkunje angali mhbichi.
LAKIN KWENYE UCHAGUZI WA WALIMU WAWEKE MDHAHA KANDO PIA WAWALIPE VIZURI
 
Unadhani serikali hii ya kifisadi iliyojaa wachumiatumbo, chawa na kupe inaweza kutekeleza hili?
 
Iwe One ama Foo..hizo elimu hazina impact zozote kwenye jamii kwa dunia ya sasa. Elimu za kukariri zimepitwa na wakati. Ndo maana tunahitaji mabadiliko kwenye mfumo wa elimu uendane na mahitaji sahihi
Serikali tayari imeanza mchakato wa kuhamia kwenye mtaala wa CBC bila kufundisha walimu (on-job training) na wala hakuna vitendea kazi na mazingila ya kutekeleza mtaala mpya. Hali itakuwa mbaya zaidi kwenye huu mtaala mpya kuliko huu wa kukariri.
 
Ndugu watanzania, tuamke kumekucha! Tuamke tupiganie haki yetu ya msingi ya kupewa elimu bora na sio bora elimu. Leo wakati katibu mtendaji wa NECTA anawasilisha matokeo nimemsikiliza kwa makini sana. Amedai eti ufaulu wa mwaka 2023 umepanda kwa 0.87% ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2022.

Baada ya kusikiliza matokeo yaliyowasilishwa, nimeingia kwenye mtandao kujiridhisha kama alichosema katibu kinaakisi kupanda ufaulu au la. Nimegundua serikali imejificha kwenye kichaka cha siasa ndio maana kila siku mambo yanaenda ovyo lakini watanzania hawajali. Wamekaa kimya kama mabubu kana kwamba kila kitu kiko sawa.

Serikali inaficha uovu wake wa kuua elimu ya watanzania kwenye siasa za majitaka. Zamani NECTA walikuwa hawatoi matokeo ya jumla na ya kipuuzi kama haya wanayotoa sasa. Walilazmishwa kubadili mfumo kisiasa ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Kwa mfano, siku za nyuma wanafunzi walikuwa wanachaguliwa kuingia kidato cha kwanza kwa kuangalia jumla ya alama ambazo kila mwanafunzi amepata.

Kipindi hicho nafasi za sekondari zilikuwa chache, hivyo ushindani ulikuwa mkubwa. Pia mitihani ilikuwa migumu sana. Kwa mfano, kwa upande wa shule za msingi kulikuwa na mkusanyiko wa masomo matatu tu yaani Lugha, Hisabati na Maarifa, na kila somo lilichukua jumla ya alama 50. Hivyo, jumla ya alama za juu ilikuwa 150.

Haikuwa ajabu mwanafunzi kupata alama 145 akakosa nafasi ya kwenda sekondari. Siku hizi utakuta mwanafunzi kapata alama 11 lakini anachaguliwa kwenda sekondari kwa kisingizio cha kwamba amepata wastani wa D! Hii ni nchi ya ajabu sana. Ndio maana serikali imefanya kila njia kuongeza mafumbo kwenye elimu ili kuficha udhaifu wa kushuka kwa kiwango cha elimu na ufaulu katika nchi hii.

Nikirejea kwenye hoja yangu ya msingi, ukiangalia matokeo ya shule za serikali (shule za kata) ambazo NECTA inasema ufaulu wake umepanda, ni ubatili mtupu. Nimejaribu kuchukua shule chache kama mfano. Hebu tazama hiki kichekesho, ucheke uongeze siku za kuishi:
View attachment 2882622
View attachment 2882624View attachment 2882625View attachment 2882628
Ukihesabu idadi ya wanafunzi walioangukia kwenye ufaulu wa daraja la nne ni zaidi ya 95% ya wanafunzi wote nchi nzima. Kumbe ufauulu ulioongezeka ni wa divisheni foo! Sote tunafahamu kuwa ufaulu wa divisheni foo hauna maana yoyote. Mwanafunzi aliyepata divisheni foo hastahili hata kupewa cheti. Akafanyie nini hicho cheti? Hakina maana yoyote ile.

Hivi serikali sikivu ya CCM mnamdanganya nani na haya matokeo yenu ya mchongo ambayo kila mwaka ufaulu wake unapanda? Haya ndiyo maajabu ya serikali hii ya kusadikika iliyojaa hadaa, usanii na unafiki kila mahali.
Bila kufanya jambo huyu Bibi anaitumbukiza TANGANYIKA shimoni!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Iwe One ama Foo..hizo elimu hazina impact zozote kwenye jamii kwa dunia ya sasa. Elimu za kukariri zimepitwa na wakati. Ndo maana tunahitaji mabadiliko kwenye mfumo wa elimu uendane na mahitaji sahihi
Kama vipi serikali iachane na elimu dunia iwe inatoa elimu akhera tu kama wanavyotaka wavaa shungi akina FaizaFoxy
 
Maisha hayaangalii division one wala 4.

Diamond ana division 4 lkn anawazidi akina Professor Kabudi na prof. Mkenda waliopata division 1.
 
Kuna jamaa niliona kwenye sherehe ya Manara anawatukana waliosoma kwamba yeye ni Zero Ila anawaongoza wenye Degrees Masters na PhD, hizi Si dharau hizi zinazofanya madogo wakaandike matusi kwenye pepa
Huyo atakuwa alikula ndumu sio bure aisee! Watu wana dharau sana.
 
Hao wenye four ni ziro hizo…. Wamedanganywa! Ndio maana siku hizi hawatangazi shule wala wanafunzi waliofanya vizuri au vibaya… wanataka kuficha madudu…
 
Back
Top Bottom