Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Punguza chuki maisha hayapo hivyo ..Kwenye hizo shule ulizotaja,nyingi Zina watoto wengi wa Kiislamu ambao wanaweka mbele Elim akhera kuliko Elim Dunia,mwisho wa siku ndio haya.......watapata thawabu na Allah
Mzee wangu said mohamed njoo uone wajukuu wako wanavyopotea
Hawo wote ni zero tu na ukijumlisha wote wenye zero na foo, wanafika 96% ya wanafunzi wote. Waliopata 1 mpaka 3 ni asilimia 4% tu. Hii nchi ina mambo ya kipumbavu sana aisee!
hao "waroma" a.k.a T.E.C wamepigaje hapo👆👆👆Hayo matokeo ya marian na boys girls umeyatoa wapi mkuu?
View attachment 2882790
View attachment 2882788
Zile shule wanafunzi ni wa dini/madhehebu mchanganyiko mkuuhao "waroma" a.k.a T.E.C wamepigaje hapo👆👆👆
wamiliki mkuu 😂😂wako serious kwenye hii kitu💪🇹🇿👍Zile shule wanafunzi ni wa dini/madhehebu mchanganyiko mkuu
Hilo ni jambo lingine sasawamiliki mkuu 😂😂wako serious kwenye hii kitu💪🇹🇿👍
Tatizo lilianza 2012 baada ya waislamu kuandamana kumkataa Ndalichako kuwa anawaonea kwenye EFKKuingiza siasa kwenye elimu ni kuliua taifa
wapewe maua yao..🌹🌷⚘🌻Hilo ni jambo lingine sasa
Yeah maua wawepe, sema wanafunzi wazuri na wenyewe wanarahisisha kaziwapewe maua yao..🌹🌷⚘🌻
💪🇹🇿👍wapewe maua yao..🌹🌷⚘🌻Yeah maua wawepe, sema wanafunzi wazuri na wenyewe wanarahisisha kazi
Halafu unawapeleka wapi hao wote?Ulitaka wengi wapate Divisheni One???? Sijakuelewa..
Hiyo ni Statistical Distribution table.. ambayo ni Normal hapo
Papaya liloozaWewe Mzazi mtoto wako amefeli.. unailaumu Serikali...
Weww ulichukua hatua gani kumsaidia huyo mtoto tokea akiwa Form one.. mfdno Kukaa nae na kummsisitiza kuhusu elimu; kumnunulia Vitabu vya ziada; Kumtafutia remedial class
Unabaki kulia lia tu Serikali impe mtoto wako Ufaulu
Hili nalo neno mkuu. Upewe maua yako.Ukiachilia mbali Mapungufu ya Serikali yetu katika Sekta ya Elimu.WAZAZI PIA WANAMAKOSA MAKUBWA SANA,KI VP?
Wazazi wengi wanaamini mtoto kwenda shule na kurudi ndiyo kusoma.Mtoto kutoka asubuhi na kurudi mchana ndiyo kusoma uku wakiamini mwishoni atafaulu (HAPANA NA SIO KWELI).Ili mtoto afaulu ni lazima apate muda wake binafsi wakujisomea yeye kama yeye.
KUFAULU KUNA STAGES TATU
1:Kutafuta materials(Vitabu,Past papers,Quiz papers)kuhakikisha notes zote za masomo unazo.
Mzazi unatakiwa kuhakikisha mwanao ana vitabu vyote vya masomo anayosoma shuleni.Nenda shuleni kwao uliza mtoto wangu ansoma masomo gani, Je shule ina vitabu vya kutosha mtoto wako anaweza akapata kama hamna nenda kanunue au omba kitabu ukatoe copy,kule karume wanauza vitabu vya copy bei rahisi.Mtafutie tuition ya ziada mwanao,Mtafutie Reviews za mitihani iliyopita ya miaka ya nyuma kwa maana maswali ni yale yale yanajirudia.
2:Kuhamisha materials hayo kutoka kwenye vitabu kwenda kichawani.
Hapa ndipo kwenye mtihani na ugumu na wazazi wengi wanafeli hapa,mzazi ni lazima uhakikishe mtoto wako anasoma kila siku,kila atakaporudi shule ni lazima ajisomee alichofundishwa shule ni lazima uhakikishe mtoto wako ana ratiba ya kujisomea na anaifata ratiba (sio ratiba imfate yeye).Ni ratiba uhakikishe mtoto wako halali bila ya kujisomea isipite siku bila ya kujisomea, Mtoto kwenda shule na kurudi sio kusoma
3:Kuhamisha materials kutoka kichwani kwenda kwenye mtihani.
Mzazi kaa na mwanao chukua kitabu muulize maswali kwa utani tu kujua kama anakumbuka,au unaweza ukamwambia nifundishe ulichosoma bila kuangalia kwa kitabu kwa utani tu uku mnafurahi.Hapa mtoto hawezi kusahu
Siku zote anza kujipigania wewe mwenyewe usisubiri mtu mwengine akufikirie na akupiganie.