Siasa, unafiki na usanii: Ufaulu wa kidato cha nne mwaka 2023 umejificha ndani ya divisheni 4

Hao wenye four ni ziro hizo…. Wamedanganywa! Ndio maana siku hizi hawatangazi shule wala wanafunzi waliofanya vizuri au vibaya… wanataka kuficha madudu…
Hawo wote ni zero tu na ukijumlisha wote wenye zero na foo, wanafika 96% ya wanafunzi wote. Waliopata 1 mpaka 3 ni asilimia 4% tu. Hii nchi ina mambo ya kipumbavu sana aisee!
 
Hizo div 4 zilikuwa zero hapo wameona aibu tu.na hizo division zero ni zero nyingine

Aibu kubwa kwa mbagala Kule hakuna wasomaji hata kidogo.

Watu Hadi saa Moja usiku wanasubiri gari za kurudi nyumban sasa hapo watajisomea muda gani.?
 
Hakuna mtoto wa diwani, mbunge, na vigogo wengine anasoma kwenye hizi shule zaidi ya watoto wa masikini
 
Hao waliofaulu kwa daraja la nne (division four) kwa mujibu wa serikali ya CCM ni vema wangepewa fursa ya kurudia mitihani baada ta miezi sita.

Hata kwenye maisha tunajifunza kwa kuteleza mara kadhaa.

Kuwaketa mtaani hao failures kwa kigezo kuwa wamefaulu ni kuandaa bomu.

NB: Hicho ndio kizazi kitakachoiangusha CCM.
 
Ahsante kwa kuliongelea hili swala,wakati naangalia haya matokeo nilimwambia jamaa yangu hawa serekali wanamdanganya nani,kuna shule ina fo 230 bila zero,ikabidi tucheke tu
Hapo serikali ya CCM inasema shule yote wamefaulu [emoji23]
 
Kuna jamaa niliona kwenye sherehe ya Manara anawatukana waliosoma kwamba yeye ni Zero Ila anawaongoza wenye Degrees Masters na PhD, hizi Si dharau hizi zinazofanya madogo wakaandike matusi kwenye pepa
Kwan uongo? Serikali ndo inataka hivi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wee wizo ulipata ngapii?
Mimi nina maakili balaa, nilitusua DIVISHENI ONE kali sana.

Usinifananishe na hawa MAZEZETA WA KITANGANYIKA wenye MAZIRO 🙈

Wizo ntakubonda balaa, 🥴
 
Kwan uongo? Serikali ndo inataka hivi.
Kwa hio ndio inaona ni Jambo zuri wasomi kutukanwa mitandaoni? Jamaa anatukana kabisa ooh we unasema unaenda kusoma Mwanza ooh we unaenda kusoma Uganda unarudi unakuta huna kazi huna Ajira Mimi ndio nakuongaza Kiko wapi? Kwa hio kusoma hakuna maana
 
Serikali tayari imeanza mchakato wa kuhamia kwenye mtaala wa CBC bila kufundisha walimu (on-job training) na wala hakuna vitendea kazi na mazingila ya kutekeleza mtaala mpya. Hali itakuwa mbaya zaidi kwenye huu mtaala mpya kuliko huu wa kukariri.
Kabisa Mkuu yaani ukiwa Mjini Dar es Salaam unaweza kudhani inawezekana lakini huko vijijini huu mtaala mpya hauwezekani kabisa yaani.
 
Kwenye hizo shule ulizotaja,nyingi Zina watoto wengi wa Kiislamu ambao wanaweka mbele Elim akhera kuliko Elim Dunia,mwisho wa siku ndio haya.......watapata thawabu na Allah

Mzee wangu said mohamed njoo uone wajukuu wako wanavyopotea
 
Ccm ndo chanzo

Vya bure toka lini vikawa na ubora?

Je watoto wao wanasoma hizo shule za kata?

Hilo kundi la waliopata division 4 na 0 nakuhakikishia tayari lishaondolewa ufahamu ko kulipelekesha utakavyo ni rahisi, target ya ccm.

Sio muda mrefu tu, kulikuwa na uchaguzi wa ccm chipukizi mlijionea wenyewe majina ni yale yale. Means hata ukimaliza chuo uhakika wa ajira huna hata greengard ana uhakika wa ajira kuliko msomi



ccm inajua mchezo inaoufanya kila sehem kumekuwa ni siasa tu!
 
Kwenye hizo shule ulizotaja,nyingi Zina watoto wengi wa Kiislamu ambao wanaweka mbele Elim akhera kuliko Elim Dunia,mwisho wa siku ndio haya.......watapata thawabu na Allah

Mzee wangu said mohamed njoo uone wajukuu wako wanavyopotea
Una uhakika mkuu? Ngoja tumuite bi mkubwa FaizaFoxy aje kuthibitisha.
 
Una uhakika mkuu? Ngoja tumuite bi mkubwa FaizaFoxy aje kuthibitisha.
Mbagala wanafunzi 65% ni Muslims

Tuangoma wanafunzi 70% ni Muslims

Abdallah Ulega wanafunzi 89% ni Muslims

Na bado hujagusa sehemu za Chake chake,Wete,Mjini Magharibi au Kaskazini Unguja..........huko hali ni mbaya sana kwa Watanzania wenzetu
 
Mbagala wanafunzi 65% ni Muslims

Tuangoma wanafunzi 70% ni Muslims

Abdallah Ulega wanafunzi 89% ni Muslims

Na bado hujagusa sehemu za Chake chake,Wete,Mjini Magharibi au Kaskazini Unguja..........huko hali ni mbaya sana kwa Watanzania wenzetu
Tusubiri wenyewe waje mkuu. Ukiwaambia kama jambo hili wanakuwa wakali sana. Hawataki kuambiwa ukweli.
 
Mkuu asante kwa hii nyongeza. Sasa kila kitu kiko uchi....serikali ipo uchi, NECTA ipo uchi na CCM ipo uchi. Usanii wa serikali kupika matokeo unaanzia kidato cha pili. Hebu tazama upishi huu ambao NECTA imefanya kwenye maatokeo ya kidato cha pili:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…