Siasa za kindugu, umwagaji damu na Ukatoliki nchini Ufilipino

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,775
Reaction score
71,893
UTANGULIZI

Mwaka 2017 Raisi Duterte alianzisha vita kali dhidi ya Madawa ya Kulevya nchini Ufilipino. Aliaua maelfu wa watu aliodai ni watumiaji na wauzaji wa madawa. Alienda hadi mbele ya kadamnasi na kujisifu kwamba wakati ni Meya wa Davao alikuwa anatembea usiku na kupiga watu risasi mwenyewe.

Alisema atamwaga hata damu ili nchi itokomeze kabisa vita vya madawa ya kulevya ili kuifanya nchi iwe salama. Mwaka 2022 Rodrigo Duterte alinukuliwa akisema hivi mbele ya Ummah "I will never, never apologize for the deaths" na kuendelea hivi "Kill me, jail me, I will never apologize". Wakosoaji wanasema kwamba kuua watoto wanaotumia madawa siyo njia sahihi, wale ni wagonjwa, walichokuwa wanahitaji ni msaada wa kisaikolojia na kiafya.

Ujasiri wa Duterte kwenye siasa ulitokana na historia ya familia yake kuwepo kwenye siasa za Ufilipino kwa muda mrefu tangu enzi za baba yake. Mpaka leo hii 2025 siasa za Ufilipino zimevurugika kwasababu Rodrigo Duterte alivyotawala alipenyeza watoto na ndugu kwenye nafasi za kisiasa nchini humo.

Wakati ni Meya wa Davao, alimteua binti yake Sara kuwa mgombea mwenza wa nafasi hiyo. Binti huyo baadaye alirithi kiti cha Umeya wa Davao kutoka baba yake mwaka 2016, pale baba yake alichaguliwa kuwa Raisi wa Ufilipino. Mwaka 2022 Sara Duterte alijiingiza kwenye kinyang'anyiro cha kugombea UMAKAMU WA RAISI wa Ufilipino na katika nafasi hiyo akawa pia WAZIRI WA ELIMU.

Kipindi hicho-hicho wakati Sara anagombea Umakamu wa Raisi na kuwa Waziri wa Elimu, kaka yake Sebastian Duterte akashika nafasi ya Meya wa Davao. Ifahamike kwamba wakati Sara ni Meya wa mji wa Davao, mdogo wake alikuwa Meya Msaidizi. Hivyo dada alipokuwa MAKAMU WA RAISI, kaka akaendelea kuwa KAIMU MEYA mpaka leo hii.

Mwaka 2025 dunia ilishuhudia kituko ambapo Rodrigo Duterte akiwa kama RAISI MSTAAFU alitangaza kugombea tena nafasi ya MEYA WA MJI wa Davao. Familia ya Duterte ikaenda mbali zaidi ambapo wajukuu na watoto wake wakajiingiza kwenye siasa kugombea nafasi za UBUNGE na SERIKALI ZA MITAA nchini Ufilipino.

MAUAJI YA KIKATILI MWAKA 2017
Mwaka 2017, Duterte aliua maelfu ya watu. Wengi waliokuwa upande wake walishangilia mno, ilhali wengi wakiumia na kusema ni uvunjaji wa haki za binadamu. Nakumbuka mwaka 2017 baada ya mauaji kuwa makubwa dunia nzima ilikuwa inamuongelea sana Duterte.

Nakumbuka mwaka 2017 niliwahi kusoma makala ya BBC ikisema kwamba nchi za Afrika zimetishia kujitoa ICC kwasababu Mahakama ya Jinai za Kimataifa (ICC) ilialalamikiwa kwamba inakamata tu viongozi wa nchi za Afrika. Duterte anaua lakini hafanywi chochote na Jumuiya ya Kimataifa. Viongozi wengi walitishia kujitoa ICC na kweli nchi baadhi zilifanikiwa, ikiwemo Burundi.

Mwaka 2017 baada ya muaji ya Raia kuwa mengi, mwanasheria wa Ufilipino Jude Sabio aliandika nakala ya tuhuma (Communication) yeynye kwenda ICC akielezea kwa kina mauaji yanayofanywa nchini humo na utawala wa Duterte. Dunia iliona ushahidi lakini mwaka 2019 Ufilipino walijitoa ICC na ikaonekana dhahiri kabisa kwamba Duterte hawezi kufanywa chochote kile.

MVUTANO NA KANISA KATOLIKI
Mwaka 2017 wakati mauaji yanaendelea, KANISA KATOLIKI ndiyo walikuwa vinara wa kupambana na serikali ya Duterte. Nchini Ufilipino kuna chombo kiitwacho, CATHOLIC'S BISHOPS CONFERENCE OF THE PHILLIPINES (CBCP) ambalo ndilo BARAZA LA MAASKOFU. Walikemea mauaji na kuandaa waraka mbalimbali ambazo zilisomwa makanisani na kwenye jumuiya kukosoa serikali. Jambo hili lilizua taharuki kubwa mno na Duterte na genge lake wakaamua kupambana na kanisa.

Bahati mbaya sana ni kwamba asilimia 80% ya raia wa Ufilipino ni wakatoliki. KANISA KATOLIKI limekuwepo ndani ya Ufilipino kwa miaka zaidi ya 1000 na ndilo limechangia kuifanya Ufilipino kuwa ndiyo taifa pekee barani Asia lenye Wakristo wengi mno. KANISA KATOLIKI pia litakumbukwa kwamba mwaka 1986 lilisaidia kumtoa madarakani Dikteta Ferdinand Marcos na mwaka 2001 lilisaidia kumtoa madarakani Fisadi Joseph Estrada.

Raisi Duterte baada ya kuona anashambuliwa na KANISA KATOLIKI na kukumbuka kwamba wenzake wawili washawahi kutolewa, aliamua kuanzisha vita ya wazi-wazi anaenda wazi kusema kwamba MAPADRI ni wabaguzi na hawana HAKI ya kumkosoa yeye kwasababu wengi wao ni MASHOGA na WANAZINI NA WANAWAKE.

Raisi Duterte katika kupambana na KANISA KATOLIKI aliamua kwenda kuungana na WALOKOLE a.k.a BORN AGAIN CHRISTIANS ambao walimpigia sana kura anavyoingia. WALOKOLE ni moja kati ya makundi yenye nguvu sana Ufilipino ukizingatia kwamba Ufilipino lilikuwa ni Koloni la Marekani, na ULOKOLE umezaliwa nchini Marekani.

Mapadri walitekwa, kuchafuliwa na kuuwawa, lakini BARAZA LA MAASKOFU (CBCP) walisema hawamuogopi Duterte. Wakaendelea na kutoa WARAKA kwamba hata kama wao wana dhambi, utakatifu wa KANISA hautoki kwa kiongozi binafsi wa kanisa, bali YESU KRISTO. Hii vita iliendelea na Duterte aliondoka madarakani, lakini Baraza likaendelea kuwepo, na baadaye likaanzisha vita mbaya dhidi ya Binti yake na familia yake, vita ambayo imetikisa mno siasa za Ufilipino huku Duterte akiwa amejeruhiwa mno kisiasa na hawezi kupona leo au kesho.

SIASA ZA KIMATAIFA NA SERA HATARI ZA DUTERTE ZILIVYOMPONZA
Ukweli mchungu ni kwamba mataifa makubwa kama Marekani huwa hayajali sana kinachoendelea kwingine kote kama maslahi yao hayajaguswa. Miaka ya 2000's mwanzoni Raisi Yoweri Museveni alivyoingia Congo na kusababisha muaji, Waziri wa Marekani Collin Powell alimtishia sana na kuongelea mambo mengi mabaya ya Uganda na kumpa Museveni muda wa kurekebisha la sivyo wangemshughulikia.

Museveni kama walivyo wanafunzi wengi wa Mzee Nyerere alikuwa na akili za ziada kufahamu kwamba, pale asipogusa maslahi ya Marekani hatafanywa lolote. Ila akijitia kushinda na mababeru lazima ile kwake. Museveni aliamua kuunga mkono VITA DHIDI YA UGAIDI (WAR ON TERROR) waziwazi na kupeleka vikosi vyake nchini Somalia na kwingineko ambako Marekani alitaka. Alizichanga karata zake vizuri sana.

Raisi Rodrigo Duterte hakuwa na akili. Hali akifahamu fika, Ufilipino lilikuwa ni koloni la Marekani yeye alienda kuanzisha uswahiba na Uchina. Wakati wenzake wote wa ukanda wa Pasifiki wakijiunga na Marekani, Australia, Japan na New-Zealand kusaidia "The Pivot To Asia" yeye alijifanya anakosoa na kuleta kauzibe. Marekani walijifanya hawamuoni lakini wakawa wanamvizia tu, na bahati mbaya akajaa kwenye mfumo.

Mwanahabari Sebastian Strangio kwenye makala yake iitwayo, "Parsing The Philippines Pivot To China Under Rodrigo Duterte" kwenye moja ya jarida maarufu barani Asia, THE DIPLOMAT, anaandika wazi kusema "He was not a strategic thinker. His foreign policy flowed from his personal likes and dislikes." Akielezea kwa kina kwamba kitendo cha Duterte kuwatukana wazi Wamarekani na kuonesha kuchagua upande fulani kulimgharimu sana.

KUKAMATWA NA MAHAKAMA YA ICC
Mambo yalianza mwaka 2017, mwaka 2019 Ufilipino ikajitoa ICC. Mwaka 2021 baada ya familia ya Duterte kuonekana inaendelea kushikana na Uchina wakati VITA BARIDI mpya baina ya Marekani na Uchina inaendelea wakubwa wa dunia wakaamua kumtumia ujumbe mdogo tu.

ICC ikaruhusu uchunguzi dhidi ya Duterte, kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu (Crimes Against Humanity). Tena kumkomesha wakaanza kufuatilia vitendo vyake vya mauaji tokea miaka ya 90's kupitia genge la kihalifu liitwalo, THE DAVAO DEATH (DDV). Ambapo inasemekana yeye alifahamu kinachofanywa na hili kundi la muaji ya raia akiwa Meya, lakini hakuchukua hatua zozote kuzuia UTEKAJI, UTESWAJI na MAUAJI.

Wameenda mbali mno na kufukua TAARIFA za Human Rights Watch na UN Human Rights Council. Taarifa za miaka mingi sana zikionesha Duterte alikuwa hachukui hatua zozote zile kwasababu alikuwa ni mnufaika wa UTEKAJI, UTESWAJI na MUAJI.

Mwaka 2025, ICC walitoa HATI YA KUKAMATWA (ARREST WARRANT) kwa siri Raisi Duterte na kushirikiana na Interpol. Bahati mbaya sana watu ambao walikuwa washirika wake kisiasa walisaidia kumuangusha na kuhakikisha anakamatwa. Hawajaishia tu hapo, hadi Binti yake Sara ambaye ni WAZIRI WA ELIMU na MAKAMU WA RAISI anaanza kutikiswa na kupewa majina kama "Pro-China" huku BARAZA LA MAASKOFU (CBCP)likisema awajibishwe.

Duterte amekamatwa na ICC, BARAZA LA MAASKOFU (CBCP) wakatoa waraka mwingine kuunga mkono ukamatwaji huo. Bahati mbaya sana inasemekana ICC wameandaa nyaraka nyingine za siri ambazo kuna watu tisa wa karibu wa Duterte wanatakiwa kukamatwa, akiwemo MKUU WA JESHI LA POLISI.

Bahati mbaya sana Sara Duterte ambaye alikuwa MEYA MSAIDIZI kwa Baba yake, amekiri wazi kwamba hata yeye yuko kwenye orodha ya ICC. Alinukuliwa akisema hivi "I’m on the list. Many of us are. There are many of us on the ICC’s list". Mdogo wake wa kiume Sebastian Duterte ambaye ndiye anaratibu makundi ya wahuni alionekana wazi kumtishia Raisi Marcos BongBong hasimu wa baba yake kwamba atakufa kama Nicholas Ramanov na Benitho Mussolini, naye inasemekana kwenye orodha ya ICC yupo.

==========================================================

SIASA inahitaji akili na utaalamu wa hali ya juu. Duterte alikuwa na nguvu sana na aliwashinda kabisa mahasimu wake. Alikuja kukosea alivyoenda Uchina na kutoa kauli za kebehi kwa WAMAREKANI ambao Ufilipino ni koloni lao mpaka sasa (De Facto Colony). Nchi zina uhuru wa kuchagua marafiki, lakini ukweli mchungu ni kwamba WAKUBWA WA DUNIA ni lazi ucheze nao vizuri.

Mzee Nyerere alishawahi kusema wazi haiwezekani kushindana na WAKUBWA WA DUNIA kwa nchi masikini kama zetu. Hawa wakubwa utawashinda endapo unafanya siasa zako za ndani kitaalamu na huna makandokando mengi kama Rushwa, Ubadhilifu na Upendeleo. Mfano halisi ni Lee Kuan Yew, Nyerere, Kagame, Jerry Rawlings n.k

Pia fahamu fika kwamba familia zikiwa zinafanya siasa madhara huwa hayaishii kwa wazazi tu, huwa yanaenda hadi kwa watoto. Ndiyo maana wanasiasa wenye akili huwa wanaweka watoto wao mbali kabisa na siasa. Urusi Ramanovs walikufa wote. Iraq, Saddam Hussein aliuwawa na watoto wake. Libya, Ghaddafi na watoto wake waliuwawa sana. Uchina, baada ya Mao kufa walimkamata Mke wake na kumhukumia adhabu ya kifo. Historia imejaa ushahidi mwingi sana.

Pia, siasa za kidini huwa zinaleta mgawanyo wa muda mrefu. Ukishaanza kuzifanya fahamu fika kwamba moto wake hauwezi kuzimika, hasahasa kwa taasisi kubwa zenye ushawishi kama KANISA KATOLIKI. Wataondoka maaskofu msiowapenda au mtawaua kabisa, lakini KANISA limekuwepo hapa kwa miaka zaidi ya 2000. Hii siyo bahati mbaya.

UKWELI USIOPINGIKA: Viongozi wa KANISA KATOLIKI huwa wana matatizo ya UDINI ULIOPITILIZA wa kuamini kwamba hii nchi ni mali yao na wao ndiyo wana haki ya kusema kama MIUNGU-WATU. Hii tabia ndiyo ilisababisha wakatoliki wachinjane na waprotestanti kule ULAYA kwa miaka zaidi ya 30 na kusababisha dola la rumi (The Holy Roman Empire) kuporomoka.

Ukiwasikiliza mapadri wengi kama una akili nzuri na ufahamu mkubwa utafahamu kwamba hata wenyewe hawaelewi kwanini huwa wanatetea mengi wanayoyatetea. Mengine siyo kutetea HAKI bali ni RELIGIOUS IMPULSE, rooted from entitlement and parochial mindset.

HAPA HOJA YA KISOMI NI HII: Ogopa kutoa matamka jumuishi (Generalization), kudai kwasababu wanakupinga wewe basi KATOLIKI NZIMA itakuwa imeoza. Hii ni sawa na kusema UKATOLIKI NI MBAYA kwasababu tu matendo kama THE SPANISH INQUISITIONS au UISLAMU NI MBAYA kwasababu ya Matendo ya Makundi kama BOKO-HARAM au AL QAEDA. Fallacy of Generalization.

Hii hoja aliwahi kujibiwa Prof Jordan Peterson alipojichanganya kutaka kufanya mjadala na Prof Richard Wolff kuhusu Ukomunisti, ambapo Wolff alisema kwamba Jordan Peterson ni mpumbavu kwa kusema Ukomunisti ni falsafa ya hovyo kisa tu mauaji yaliyofanywa na Joseph Stalin kule Siberia.

ILA KUBWA ZAIDI: Ni kujitahidi kumaliza migogoro ya kidini nyuma ya pazia kabla haijafika hadharani. Mbinu ziko nyingi sana za kuweza kutoa tamko zito nyuma ya pazia na mambo yakakaa vizuri tu. Mzee Mkapa aliwahi kuvutana mno na TEC, tena sanaa lakini hayakufika hadharani. Hata Jakaya aliwahi kuvutana nao, lakini yeye Friji Lake Lilikuwa linagandisha, hayakufika hadharani.
================================================================

ENIWEI, tusubiri tuone.....
​
 
Mara zote serikali ovu huwa zinaanguka vibya mno

IMG-20251231-WA0001.jpg
 
UKWELI USIOPINGIKA: Viongozi wa KANISA KATOLIKI huwa wana matatizo ya UDINI ULIOPITILIZA wa kuamini kwamba hii nchi ni mali yao na wao ndiyo wana haki ya kusema kama MIUNGU-WATU. Hii tabia ndiyo ilisababisha wakatoliki wachinjane na waprotestanti kule ULAYA kwa miaka zaidi ya 30 na kusababisha dola la rumi (The Holy Roman Empire) kuporomoka.
Huu ndio ukweli wenyewe ndio maana Ulaya na US walidhibitiwa
 
UKWELI USIOPINGIKA: Viongozi wa KANISA KATOLIKI huwa wana matatizo ya UDINI ULIOPITILIZA wa kuamini kwamba hii nchi ni mali yao na wao ndiyo wana haki ya kusema kama MIUNGU-WATU. Hii tabia ndiyo ilisababisha wakatoliki wachinjane na waprotestanti kule ULAYA kwa miaka zaidi ya 30 na kusababisha dola la rumi (The Holy Roman Empire) kuporomoka.

Ukiwasikiliza mapadri wengi kama una akili nzuri na ufahamu mkubwa utafahamu kwamba hata wenyewe hawaelewi kwanini huwa wanatetea mengi wanayoyatetea. Mengine siyo kutetea HAKI bali ni RELIGIOUS IMPULSE, rooted from entitlement and parochial
​

Umewashutumu viongozi wa Katoliki kwa mambo mazito na makubwa.

Kuthibitisha kama madai yako ni ya kweli au ni ya kizushi, uongo unaweza kutoa ushahidi na mifano ya haya madai yako hapa Tanzania.

Tafadhari toa jina la hao viongozi Wakatoliki, vituo vyao vya kazi hapa Tanzania na walisema hayo mambo unayowashutumu wapi, lini, wakilenga nini, context ku-support na kuthibitisha madai yako, tuwekee ushahidi wa video au text kwenye madai yako namba hapo chini 1-5.

1.Viongozi wa Katoliki huwa wana udini uliopitiliza.

2. Wanaamini hii nchi ni mali yao.

3. Wanajiona wana haki ya kusema kama MIUNGU-WATU.

4.Ukiwasikiliza huwa hawaelewi kwanini wanatetea mengi wanayotetea.

5.Mengine siyo kutetea HAKI bali ni RELIGIOUS IMPULSE, rooted from entitlement and parochial
 
Mada yako na wewe ni dini gani?.Unaeleza alafu unajisahau unaeleeza hisia zako wazi.

Nime kunukuu ukisema wakatoliki hawajui wanacho kitetea.

Watu wanavyotekwa,kufirwa,kubakwa,kuuliwa na kupewa ukilema kwa hiyo Ulitaka wasifu na kuabudu.

Naomba kuuliza dini yako?.

Umetoa mada nzuri ila nimegundua ndio nyie mnaoleta propaganda fulani usipo shtuka unatuchukua.

mfano historia ya rwanda ilikuwa kwa ajili ukabila ila kwa sisi kwenye kusimuliana wanaingiza udini sijui vipi vipi?.Ila wengi walikimbilia makanisani ila ukabila ndio ulikuwa tatizo.

Uganda kipindi cha idd amin napo ni vile vile ukabila .
 
Haki ina upande,
Askofu Desmond Tutu hakuwa mkatoliki lakini aliwapinga makaburu na utawala wao dhalimu kwa msimamo thabiti kabisa.
Askofu Janani Luwumu hakuwa Mkatoliki ila alisimama kidete kumpinga Dikteta Iddi Amini
 
Andiko nzuri lenye angalizo nzuri ana lenye hoja inayopaswa kuangaliwa kwa upeke.

Ila hapo kwenye viongozi wa kanisa kuwa na udini mkuu MALCOM LUMUMBA unapata upinzani kidogo.

Kanisa haswa katoliki limeshapita misimu mingi sana kila pito hubakiwa na funzo.

Fikra na mtazamo wa kanisa kwa miaka 200 iliyo pita haiwezi kuwa sawa na sasa.

Naomba nisiandike mengi lakini ukweli ni sivyo ulivyo bainisha.
 
Umewashutumu viongozi wa Katoliki kwa mambo mazito na makubwa.

Kuthibitisha kama madai yako ni ya kweli au ni ya kizushi, uongo unaweza kutoa ushahidi na mifano ya haya madai yako hapa Tanzania.

Tafadhari toa jina la hao viongozi Wakatoliki, vituo vyao vya kazi hapa Tanzania na walisema hayo mambo unayowashutumu wapi, lini, wakilenga nini, context ku-support na kuthibitisha madai yako, tuwekee ushahidi wa video au text kwenye madai yako namba hapo chini 1-5.

1.Viongozi wa Katoliki huwa wana udini uliopitiliza.

2. Wanaamini hii nchi ni mali yao.

3. Wanajiona wana haki ya kusema kama MIUNGU-WATU.

4.Ukiwasikiliza huwa hawaelewi kwanini wanatetea mengi wanayotetea.

5.Mengine siyo kutetea HAKI bali ni RELIGIOUS IMPULSE, rooted from entitlement and parochial
Twenda taratibu kwa ushahidi.

Moja ya sababu kubwa kabisa ya Mzee Nyerere kutaifisha shule za kanisa haikuwa kutoa elimu peke yake, bali uhalisia uliokuwepo kwamba baadhi ya waislamu walitengwa kipindi cha ukolini kwenye kupata elimu. Kuna wasomi wa Tanganyika ili kupata elimu ilikuwa ni lazima wabadili dini na kuwa wakatoliki. Huu ulikuwa ni ubaguzi wa kimfumo (Systematic Discrimination) ambao uliligubika kanisa Katoliki duniani kote.

Ushahidi mwingine ni ule wa wazi, ambapo Ukatoliki uliunga mkono mauaji na unyanyasaji wa jamii zisizo za Kikatoliki duniani kote. Hili lina ukweli mchungu hata Papa Francis aliomba msamaha kwa jamii za WAHINDI WEKUNDU nchini CANADA kwa mamanyanyasao ambayo kanisa liliwafanyia kwenye maisha yao yote hadi kwenye mashule. Hili halikufanywa siku moja ni kwa miaka mingi mno.

Ushahidi upo na kanisa liliomba msamaha mbele ya dunia yote. Halikufanya hivyo kwa WAHINDI WEKUNDU, bali hata kwa WAYAHUDI ambapo Papa alienda mbali na KUWAOSHA MIGUU WAYAHUDI kwa makosa ya kibaguzi ambayo kanisa liliwafanyia kwa miaka zaidi ya elfu moja. Sasa kama kanisa lenyewe linawajibika utasemaje kwamba mimi nawatuhumu bure ???
=====================================================================

HOJA YA KISOMI HAPA NI HII:

MOSI: Je, ni kweli TEC wanamshambulia Samia kwasababu yeye ni Muislamu, Mwanamke na Mzanzibari ???

PILI: Je, ni kweli TEC hawajawahi kuwashambulia viongozi wa Kikristo, Wanaume na Watanganyika ???

TATU: Je, wanachokikema TEC ni kitu haramu au halali kwa serikali kukifanya ???
​
 
Mada yako na wewe ni dini gani?.Unaeleza alafu unajisahau unaeleeza hisia zako wazi.

Nime kunukuu ukisema wakatoliki hawajui wanacho kitetea.

Watu wanavyotekwa,kufirwa,kubakwa,kuuliwa na kupewa ukilema kwa hiyo Ulitaka wasifu na kuabudu.

Naomba kuuliza dini yako?.

Umetoa mada nzuri ila nimegundua ndio nyie mnaoleta propaganda fulani usipo shtuka unatuchukua.

mfano historia ya rwanda ilikuwa kwa ajili ukabila ila kwa sisi kwenye kusimuliana wanaingiza udini sijui vipi vipi?.Ila wengi walikimbilia makanisani ila ukabila ndio ulikuwa tatizo.

Uganda kipindi cha idd amin napo ni vile vile ukabila .
Kama kanisa lenyewe lilikili kuhusika na mauaji ya Rwanda ww ni nani upinge?
 
Mada yako na wewe ni dini gani?.Unaeleza alafu unajisahau unaeleeza hisia zako wazi.

Nime kunukuu ukisema wakatoliki hawajui wanacho kitetea.

Watu wanavyotekwa,kufirwa,kubakwa,kuuliwa na kupewa ukilema kwa hiyo Ulitaka wasifu na kuabudu.

Naomba kuuliza dini yako?.

Umetoa mada nzuri ila nimegundua ndio nyie mnaoleta propaganda fulani usipo shtuka unatuchukua.

mfano historia ya rwanda ilikuwa kwa ajili ukabila ila kwa sisi kwenye kusimuliana wanaingiza udini sijui vipi vipi?.Ila wengi walikimbilia makanisani ila ukabila ndio ulikuwa tatizo.

Uganda kipindi cha idd amin napo ni vile vile ukabila .
​
Ukiamua kutotaka kunielewa ni ruksa tu Mkuu.

Ila hoja zangu zina msingi wa kihistoria na ushahidi wa kisheria ambao uko wazi, dhahiri na hata mamlaka za kanisa zinakiri kuhusu uwepo wake. Katika miaka yake 2000 kanisa katoliki limetenda madhambi mengi sana kwa jamii ambazo sizo za wakatoliki. Limefanya mauaji, utekaji na kutoa miongozi mingi ya kikuhani ambayo imelichafua kanisa mpaka leo hii kulazimisha hadi Mapapa waombe msamaha mbele za dunia nzima.

MASWALI YA MSINGI HAPA NI HAYA:

MOSI: Je, ni kweli kanisa katoliki halikuwahi kutenda mabaya dhidi ya watu ???

PILI: Je, ni kweli kanisa katoliki halikuwahi kuunga mkono vitendo dhalimu vya watawala wakatoliki ambao walinyanyasa watu ???

TATU: Je, ni sahihi kusema kanisa katoliki halina uhalali wowote kukemea maovu kwasababu ya vitendo hivi vya kihistoria ???

NNE: Je, ni sahihi kusema kanisa katoliki lote ni taasisi ovu kisa matendo ya viongozi wake wachache tu ndani ya Kanisa ??? (Hapa zingatia muktadha wa Rwanda 1994)

TANO: Je, ni sahihi kusema kanisa katoliki linafanya mabaya tu ilhali tunakataa kusema mazuri yake pia ambayo lilifanya kama kusaidia harakati za ukombozi barani Afria na America kwa kusomesha maelfu ya wasomi ???

SITA: Je, Kanisa Katoliki linampinga Samia kwasababu ya Uislamu wake tu ???

SABA: Je, Kanisa Katoliki halijawahi kuwapinga viongozi wa Kikristo ???

NANE: Je, uovu unapofanyika dhidi ya raia, ni sahihi Kanisa Katoliki kunyamaza na kufumba macho kuwafurahisha watawala ilhali lina uzoefu wa miaka zaidi ya 2000 ya kuona nini huwa madhara ya kutokemea uovu ???

SABA: Je, ni kweli kwamba hapa Tanzania viongozi wa Kanisa Katoliki hawajawahi kufanya makosa na kutetewa na watu kwasababu tu ni viongozi wa kanisa ??? (Unakumbuka sakata la fedha za TEGETA ESCROW, MKOMBOZI BANK, RUGEMALILA, KADINALI PENGO na FATHER KILAINI ???)
​
 
Andiko nzuri lenye angalizo nzuri ana lenye hoja inayopaswa kuangaliwa kwa upeke.

Ila hapo kwenye viongozi wa kanisa kuwa na udini mkuu MALCOM LUMUMBA unapata upinzani kidogo.

Kanisa haswa katoliki limeshapita misimu mingi sana kila pito hubakiwa na funzo.

Fikra na mtazamo wa kanisa kwa miaka 200 iliyo pita haiwezi kuwa sawa na sasa.

Naomba nisiandike mengi lakini ukweli ni sivyo ulivyo bainisha.
Uko sahihi kabisa. Kanisa Katoliki linakemea sana uovu kipindi hiki kwasababu huko nyuma limeshawahi kushirikiana na watawala waovu jambo lililopelekea kanisa kutaka kupoteza mwelekeo na kusababisha mauaji ya mamilioni. Hivyo kanisa katoliki linapoona dhuluma inafanyika huwa linang'aka sana kwasababu linafahamu fika mambo huanza kidogo-kidogo.

Haya yote sikuyaweka kwenye mada yangu na nikategemea A PUSH-BACK ili niyaweke kadiri ya mjadala utakavyokuwa unaendelea. Ndiyo maana nauliza maswali ambayo majibu yake bado sijapewa. Je, ni sahihi kisomi kulihukumu kanisa kwa makosa ambayo lilifanya miaka ya nyuma ???

Je, makosa ya kanisa ya miaka ya nyuma yanalinyima kanisa uhalali wa kukemea maovu ya leo yanayotenda na watawala dhalimu ???

Je, ni sahihi kukosoa kanisa katoliki ambalo ni taasisi inayobadilisha watu na viongozi kila baada ya vizazi kadhaa. Je, ni sahihi kuhukumu hii taasisi kama mtu binafsi (As an Individual Person) ???
=====================================================================

MADA kama hizi huwa ni ngumu sana kwa WAKRISTO na WAISLAMU. Wengi huwa wanakosa OBJECTIVITY, hivyo huishia kukosoa au kuunga mkono kwasabababu binafsi za kidini bila kutafuta Middle-Ground.

Nafurahi sana kuona wewe umeelewa dhana zima la mada yangu.

HERI YA MWAKA MPYA MKUU.........
​
 
Back
Top Bottom