NDIYO, TEC wanawasemea watanzania.
Lakini TEC ni moja ya taasisi ambayo imechangia Tanganyika kufika kwenye hii hali mbaya.
Nafahamu mada kama hizi zinaibua hisia kwa waumini, but facts are stubborn things.
SAMIA hatamaliza miaka 5, lakini haya matatizo yataendelea kuwepo na makubwa zaidi.
================================================================================
Tatizo ni pale ambapo wengi tunaamini kwamba SAMIA akishaondoka nchi itajirudi kama zamani.
Samia siyo Ugonjwa (A Disease), bali ni Dalili (Symptoms) za Ugonjwa ambao umekuwepo hapa nchini kwa miaka mingi na Kanisa Katoliki limekuwepo moja ya taasisi zilizochangia huo ugonjwa kuwepo. Utakataa, utaghafilika, utanitukana au utapinga lakini ukweli hauwezi kupindishwa na hata wewe unalifahamu hili vizuri.
Ila kama siku zote nilivyosema, Tanzanians are not ready for this conversation.
Mkuu Baro wewe ni moja kati ya wanachama ninaowaheshimu mno humu jukwaani, na nachelea kusema katika hili basi tujipe muda. Panapo majaliwa ya MWENYEZI MUNGU tutarudi hapa miaka michache ya baadaye kuipitia tena upya hii mada. Kama nitakuwa nilikosea nitakiri ukweli, lakini TUJIPE MUDA.