UTANGULIZI
Mwaka 2017 Raisi Duterte alianzisha vita kali dhidi ya Madawa ya Kulevya nchini Ufilipino. Aliaua maelfu wa watu aliodai ni watumiaji na wauzaji wa madawa. Alienda hadi mbele ya kadamnasi na kujisifu kwamba wakati ni Meya wa Davao alikuwa anatembea usiku na kupiga watu risasi mwenyewe.
Alisema atamwaga hata damu ili nchi itokomeze kabisa vita vya madawa ya kulevya ili kuifanya nchi iwe salama. Mwaka 2022 Rodrigo Duterte alinukuliwa akisema hivi mbele ya Ummah "I will never, never apologize for the deaths" na kuendelea hivi "Kill me, jail me, I will never apologize". Wakosoaji wanasema kwamba kuua watoto wanaotumia madawa siyo njia sahihi, wale ni wagonjwa, walichokuwa wanahitaji ni msaada wa kisaikolojia na kiafya.
Ujasiri wa Duterte kwenye siasa ulitokana na historia ya familia yake kuwepo kwenye siasa za Ufilipino kwa muda mrefu tangu enzi za baba yake. Mpaka leo hii 2025 siasa za Ufilipino zimevurugika kwasababu Rodrigo Duterte alivyotawala alipenyeza watoto na ndugu kwenye nafasi za kisiasa nchini humo.
Wakati ni Meya wa Davao, alimteua binti yake Sara kuwa mgombea mwenza wa nafasi hiyo. Binti huyo baadaye alirithi kiti cha Umeya wa Davao kutoka baba yake mwaka 2016, pale baba yake alichaguliwa kuwa Raisi wa Ufilipino. Mwaka 2022 Sara Duterte alijiingiza kwenye kinyang'anyiro cha kugombea UMAKAMU WA RAISI wa Ufilipino na katika nafasi hiyo akawa pia WAZIRI WA ELIMU.
Kipindi hicho-hicho wakati Sara anagombea Umakamu wa Raisi na kuwa Waziri wa Elimu, kaka yake Sebastian Duterte akashika nafasi ya Meya wa Davao. Ifahamike kwamba wakati Sara ni Meya wa mji wa Davao, mdogo wake alikuwa Meya Msaidizi. Hivyo dada alipokuwa MAKAMU WA RAISI, kaka akaendelea kuwa KAIMU MEYA mpaka leo hii.
Mwaka 2025 dunia ilishuhudia kituko ambapo Rodrigo Duterte akiwa kama RAISI MSTAAFU alitangaza kugombea tena nafasi ya MEYA WA MJI wa Davao. Familia ya Duterte ikaenda mbali zaidi ambapo wajukuu na watoto wake wakajiingiza kwenye siasa kugombea nafasi za UBUNGE na SERIKALI ZA MITAA nchini Ufilipino.
MAUAJI YA KIKATILI MWAKA 2017
Mwaka 2017, Duterte aliua maelfu ya watu. Wengi waliokuwa upande wake walishangilia mno, ilhali wengi wakiumia na kusema ni uvunjaji wa haki za binadamu. Nakumbuka mwaka 2017 baada ya mauaji kuwa makubwa dunia nzima ilikuwa inamuongelea sana Duterte.
Nakumbuka mwaka 2017 niliwahi kusoma makala ya BBC ikisema kwamba nchi za Afrika zimetishia kujitoa ICC kwasababu Mahakama ya Jinai za Kimataifa (ICC) ilialalamikiwa kwamba inakamata tu viongozi wa nchi za Afrika. Duterte anaua lakini hafanywi chochote na Jumuiya ya Kimataifa. Viongozi wengi walitishia kujitoa ICC na kweli nchi baadhi zilifanikiwa, ikiwemo Burundi.
Mwaka 2017 baada ya muaji ya Raia kuwa mengi, mwanasheria wa Ufilipino Jude Sabio aliandika nakala ya tuhuma (Communication) yeynye kwenda ICC akielezea kwa kina mauaji yanayofanywa nchini humo na utawala wa Duterte. Dunia iliona ushahidi lakini mwaka 2019 Ufilipino walijitoa ICC na ikaonekana dhahiri kabisa kwamba Duterte hawezi kufanywa chochote kile.
MVUTANO NA KANISA KATOLIKI
Mwaka 2017 wakati mauaji yanaendelea, KANISA KATOLIKI ndiyo walikuwa vinara wa kupambana na serikali ya Duterte. Nchini Ufilipino kuna chombo kiitwacho, CATHOLIC'S BISHOPS CONFERENCE OF THE PHILLIPINES (CBCP) ambalo ndilo BARAZA LA MAASKOFU. Walikemea mauaji na kuandaa waraka mbalimbali ambazo zilisomwa makanisani na kwenye jumuiya kukosoa serikali. Jambo hili lilizua taharuki kubwa mno na Duterte na genge lake wakaamua kupambana na kanisa.
Bahati mbaya sana ni kwamba asilimia 80% ya raia wa Ufilipino ni wakatoliki. KANISA KATOLIKI limekuwepo ndani ya Ufilipino kwa miaka zaidi ya 1000 na ndilo limechangia kuifanya Ufilipino kuwa ndiyo taifa pekee barani Asia lenye Wakristo wengi mno. KANISA KATOLIKI pia litakumbukwa kwamba mwaka 1986 lilisaidia kumtoa madarakani Dikteta Ferdinand Marcos na mwaka 2001 lilisaidia kumtoa madarakani Fisadi Joseph Estrada.
Raisi Duterte baada ya kuona anashambuliwa na KANISA KATOLIKI na kukumbuka kwamba wenzake wawili washawahi kutolewa, aliamua kuanzisha vita ya wazi-wazi anaenda wazi kusema kwamba MAPADRI ni wabaguzi na hawana HAKI ya kumkosoa yeye kwasababu wengi wao ni MASHOGA na WANAZINI NA WANAWAKE.
Raisi Duterte katika kupambana na KANISA KATOLIKI aliamua kwenda kuungana na WALOKOLE a.k.a BORN AGAIN CHRISTIANS ambao walimpigia sana kura anavyoingia. WALOKOLE ni moja kati ya makundi yenye nguvu sana Ufilipino ukizingatia kwamba Ufilipino lilikuwa ni Koloni la Marekani, na ULOKOLE umezaliwa nchini Marekani.
Mapadri walitekwa, kuchafuliwa na kuuwawa, lakini BARAZA LA MAASKOFU (CBCP) walisema hawamuogopi Duterte. Wakaendelea na kutoa WARAKA kwamba hata kama wao wana dhambi, utakatifu wa KANISA hautoki kwa kiongozi binafsi wa kanisa, bali YESU KRISTO. Hii vita iliendelea na Duterte aliondoka madarakani, lakini Baraza likaendelea kuwepo, na baadaye likaanzisha vita mbaya dhidi ya Binti yake na familia yake, vita ambayo imetikisa mno siasa za Ufilipino huku Duterte akiwa amejeruhiwa mno kisiasa na hawezi kupona leo au kesho.
SIASA ZA KIMATAIFA NA SERA HATARI ZA DUTERTE ZILIVYOMPONZA
Ukweli mchungu ni kwamba mataifa makubwa kama Marekani huwa hayajali sana kinachoendelea kwingine kote kama maslahi yao hayajaguswa. Miaka ya 2000's mwanzoni Raisi Yoweri Museveni alivyoingia Congo na kusababisha muaji, Waziri wa Marekani Collin Powell alimtishia sana na kuongelea mambo mengi mabaya ya Uganda na kumpa Museveni muda wa kurekebisha la sivyo wangemshughulikia.
Museveni kama walivyo wanafunzi wengi wa Mzee Nyerere alikuwa na akili za ziada kufahamu kwamba, pale asipogusa maslahi ya Marekani hatafanywa lolote. Ila akijitia kushinda na mababeru lazima ile kwake. Museveni aliamua kuunga mkono VITA DHIDI YA UGAIDI (WAR ON TERROR) waziwazi na kupeleka vikosi vyake nchini Somalia na kwingineko ambako Marekani alitaka. Alizichanga karata zake vizuri sana.
Raisi Rodrigo Duterte hakuwa na akili. Hali akifahamu fika, Ufilipino lilikuwa ni koloni la Marekani yeye alienda kuanzisha uswahiba na Uchina. Wakati wenzake wote wa ukanda wa Pasifiki wakijiunga na Marekani, Australia, Japan na New-Zealand kusaidia "The Pivot To Asia" yeye alijifanya anakosoa na kuleta kauzibe. Marekani walijifanya hawamuoni lakini wakawa wanamvizia tu, na bahati mbaya akajaa kwenye mfumo.
Mwanahabari Sebastian Strangio kwenye makala yake iitwayo, "Parsing The Philippines Pivot To China Under Rodrigo Duterte" kwenye moja ya jarida maarufu barani Asia, THE DIPLOMAT, anaandika wazi kusema "He was not a strategic thinker. His foreign policy flowed from his personal likes and dislikes." Akielezea kwa kina kwamba kitendo cha Duterte kuwatukana wazi Wamarekani na kuonesha kuchagua upande fulani kulimgharimu sana.
KUKAMATWA NA MAHAKAMA YA ICC
Mambo yalianza mwaka 2017, mwaka 2019 Ufilipino ikajitoa ICC. Mwaka 2021 baada ya familia ya Duterte kuonekana inaendelea kushikana na Uchina wakati VITA BARIDI mpya baina ya Marekani na Uchina inaendelea wakubwa wa dunia wakaamua kumtumia ujumbe mdogo tu.
ICC ikaruhusu uchunguzi dhidi ya Duterte, kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu (Crimes Against Humanity). Tena kumkomesha wakaanza kufuatilia vitendo vyake vya mauaji tokea miaka ya 90's kupitia genge la kihalifu liitwalo, THE DAVAO DEATH (DDV). Ambapo inasemekana yeye alifahamu kinachofanywa na hili kundi la muaji ya raia akiwa Meya, lakini hakuchukua hatua zozote kuzuia UTEKAJI, UTESWAJI na MAUAJI.
Wameenda mbali mno na kufukua TAARIFA za Human Rights Watch na UN Human Rights Council. Taarifa za miaka mingi sana zikionesha Duterte alikuwa hachukui hatua zozote zile kwasababu alikuwa ni mnufaika wa UTEKAJI, UTESWAJI na MUAJI.
Mwaka 2025, ICC walitoa HATI YA KUKAMATWA (ARREST WARRANT) kwa siri Raisi Duterte na kushirikiana na Interpol. Bahati mbaya sana watu ambao walikuwa washirika wake kisiasa walisaidia kumuangusha na kuhakikisha anakamatwa. Hawajaishia tu hapo, hadi Binti yake Sara ambaye ni WAZIRI WA ELIMU na MAKAMU WA RAISI anaanza kutikiswa na kupewa majina kama "Pro-China" huku BARAZA LA MAASKOFU (CBCP)likisema awajibishwe.
Duterte amekamatwa na ICC, BARAZA LA MAASKOFU (CBCP) wakatoa waraka mwingine kuunga mkono ukamatwaji huo. Bahati mbaya sana inasemekana ICC wameandaa nyaraka nyingine za siri ambazo kuna watu tisa wa karibu wa Duterte wanatakiwa kukamatwa, akiwemo MKUU WA JESHI LA POLISI.
Bahati mbaya sana Sara Duterte ambaye alikuwa MEYA MSAIDIZI kwa Baba yake, amekiri wazi kwamba hata yeye yuko kwenye orodha ya ICC. Alinukuliwa akisema hivi "I’m on the list. Many of us are. There are many of us on the ICC’s list". Mdogo wake wa kiume Sebastian Duterte ambaye ndiye anaratibu makundi ya wahuni alionekana wazi kumtishia Raisi Marcos BongBong hasimu wa baba yake kwamba atakufa kama Nicholas Ramanov na Benitho Mussolini, naye inasemekana kwenye orodha ya ICC yupo.
==========================================================
SIASA inahitaji akili na utaalamu wa hali ya juu. Duterte alikuwa na nguvu sana na aliwashinda kabisa mahasimu wake. Alikuja kukosea alivyoenda Uchina na kutoa kauli za kebehi kwa WAMAREKANI ambao Ufilipino ni koloni lao mpaka sasa (De Facto Colony). Nchi zina uhuru wa kuchagua marafiki, lakini ukweli mchungu ni kwamba WAKUBWA WA DUNIA ni lazi ucheze nao vizuri.
Mzee Nyerere alishawahi kusema wazi haiwezekani kushindana na WAKUBWA WA DUNIA kwa nchi masikini kama zetu. Hawa wakubwa utawashinda endapo unafanya siasa zako za ndani kitaalamu na huna makandokando mengi kama Rushwa, Ubadhilifu na Upendeleo. Mfano halisi ni Lee Kuan Yew, Nyerere, Kagame, Jerry Rawlings n.k
Pia fahamu fika kwamba familia zikiwa zinafanya siasa madhara huwa hayaishii kwa wazazi tu, huwa yanaenda hadi kwa watoto. Ndiyo maana wanasiasa wenye akili huwa wanaweka watoto wao mbali kabisa na siasa. Urusi Ramanovs walikufa wote. Iraq, Saddam Hussein aliuwawa na watoto wake. Libya, Ghaddafi na watoto wake waliuwawa sana. Uchina, baada ya Mao kufa walimkamata Mke wake na kumhukumia adhabu ya kifo. Historia imejaa ushahidi mwingi sana.
Pia, siasa za kidini huwa zinaleta mgawanyo wa muda mrefu. Ukishaanza kuzifanya fahamu fika kwamba moto wake hauwezi kuzimika, hasahasa kwa taasisi kubwa zenye ushawishi kama KANISA KATOLIKI. Wataondoka maaskofu msiowapenda au mtawaua kabisa, lakini KANISA limekuwepo hapa kwa miaka zaidi ya 2000. Hii siyo bahati mbaya.
UKWELI USIOPINGIKA: Viongozi wa KANISA KATOLIKI huwa wana matatizo ya UDINI ULIOPITILIZA wa kuamini kwamba hii nchi ni mali yao na wao ndiyo wana haki ya kusema kama MIUNGU-WATU. Hii tabia ndiyo ilisababisha wakatoliki wachinjane na waprotestanti kule ULAYA kwa miaka zaidi ya 30 na kusababisha dola la rumi (The Holy Roman Empire) kuporomoka.
Ukiwasikiliza mapadri wengi kama una akili nzuri na ufahamu mkubwa utafahamu kwamba hata wenyewe hawaelewi kwanini huwa wanatetea mengi wanayoyatetea. Mengine siyo kutetea HAKI bali ni RELIGIOUS IMPULSE, rooted from entitlement and parochial mindset.
HAPA HOJA YA KISOMI NI HII: Ogopa kutoa matamka jumuishi (Generalization), kudai kwasababu wanakupinga wewe basi KATOLIKI NZIMA itakuwa imeoza. Hii ni sawa na kusema UKATOLIKI NI MBAYA kwasababu tu matendo kama THE SPANISH INQUISITIONS au UISLAMU NI MBAYA kwasababu ya Matendo ya Makundi kama BOKO-HARAM au AL QAEDA. Fallacy of Generalization.
Hii hoja aliwahi kujibiwa Prof Jordan Peterson alipojichanganya kutaka kufanya mjadala na Prof Richard Wolff kuhusu Ukomunisti, ambapo Wolff alisema kwamba Jordan Peterson ni mpumbavu kwa kusema Ukomunisti ni falsafa ya hovyo kisa tu mauaji yaliyofanywa na Joseph Stalin kule Siberia.
ILA KUBWA ZAIDI: Ni kujitahidi kumaliza migogoro ya kidini nyuma ya pazia kabla haijafika hadharani. Mbinu ziko nyingi sana za kuweza kutoa tamko zito nyuma ya pazia na mambo yakakaa vizuri tu. Mzee Mkapa aliwahi kuvutana mno na TEC, tena sanaa lakini hayakufika hadharani. Hata Jakaya aliwahi kuvutana nao, lakini yeye Friji Lake Lilikuwa linagandisha, hayakufika hadharani.
================================================================
ENIWEI, tusubiri tuone.....