Siasa za kindugu, umwagaji damu na Ukatoliki nchini Ufilipino

So wakatoliki walivyompings Durtete walikosea,wangemuacha afanye alivyokua anafanya?

Dini zingine hata kama ni minority zilikuwa wapi?

Hueleweki dhamira yako ni nn,hata waliokutuma wanashangaa
Ewaah, hilo ndilo swali ambalo wote tuanze kulijibu hapa.

Je, TEC inampinga Samia kwasababu ya Uislamu na Uzanzibari wake pekee ???

Je, TEC haijawahi kuwapinga viongozi wa Kikristo-Watanganyika ???

Je, Duterte alikuwa sahihi kutumia historia ya zamani kuhukumu vitendo vya leo vya kanisa katika kukemea uovu ???

=================================================================
HAYO MENGINE ya kusemwa nimetumwa NIMEKUSAMEHE.
​
 
Kwa nini usiwe umetumwa?
Magufuli hakuwa mkristo na mkatoliki? Je TEC haikumkosoa?

Kama walimkosoa Magufuli aliyekuwa mkristo na mkatoliki mwenzao hoja yako ya udini inapataje mantiki?

Kubali tu umepuyanga kwenye kuwahusisha TEC na udini. Na hili linafanya hadi werevu kujiuliza nini lengo hasa la uzi wako??
 
Nimesoma ila napata mkaranganyiko kidogo. Kwahiyo kwa mujibu wa mleta uzi ni kuwa kanisa katoliki linakosea sana kukemea maovu yanayofanywa na wahuni wanaojiita ni viongozi huko serikalini?

Kwamba kukemea uovu unaondelea kwasasa ni udini?

Hii inafikirisha sana, kwahiyo kama Kanisa katoliki ni linafanya udini kukemea maovu ya sasa ina maana madhehebu mengine na dini zingine zinasapoti si ndio?


Ndugu zanguni tuwe makini sana na ujenzi wa hoja zetu, unaweza jikuta unaongea vitu ambavyo vina contradict uhalisia na kuleta shida.
 
Nakumbuka uliandika mada kuhusu kutunza Siri,

Haikupita muda, Plepole akatekwa,

Na Leo unaongelea wakatiliki,

Nini kinapikwa huko?
The Bigger Picture is:

Politicians think about the next election. Statesmen think about future generations.

====================================================================
Nguvu kubwa ya Kanisa Katoliki ni taasisi, ni UTAASISI (INSTITUTIONALIZATION). Kwamba wewe utapambana nayo lakini wewe utaondoka ila yenyewe itabaki na watakuja watawala viongozi wengine kabisa. Hivyo ukizingatia hali ilivyo ni busara sana haya mambo yakazungumzwa nyuma ya pazia kuliko kuleta hadharani na kurushiana vijembe, jambo ambalo litazua hisia kali baina ya waumini na wafuasi.

Katika hili busara haijatumika kwasababu, nyuma ya pazia kuna CHURCH-STATE FORUM, ambacho ni chombo kinachotumika kufanya mazungumzo baina ya watawala na viongozi wa kanisa. Nini kimesababisha kushindwa kukaa meza moja na kuyamaliza huko ndani ???

Mzee Nyerere alishawahi kupambana na TEC, akawalima barua ya kutisha kweli.

Mzee Sokione alishawahi kupambana na TEC, akawashika pabaya mno baadhi viongozi wa kanisa hasa kwenye harakati za kupinga uhujumu uchumi. Sokoine alituma jumbe za kutisha kwa Maaskofu.

Mzee Mkapa alishawahi kupambana na TEC, akalumbana nao mno lakini waliyamalizia nyuma ya pazia.

Mzee Kikwte alishawahi kuzozana na TEC, walimshambulia hadharani lakini hakuvuka mpaka kwenda mbele ya kadamnasi kutaka kuchochea na kupata huruma wa kidini.
====================================================================
Hapa nje unaweza kudhani mambo yako vizuri, ila kuna watu wanaenda kuumia vibaya sana katika hili. Naam, tayari wengi washaanza kuumia nyuma ya pazia. Tukiendelea hivi kuna mambo mabaya mno yatatokea na CCM haiwezi kupona hayo majeraha, wala watawala wake hawawezi kupona hayo majeraha.

Nimetoa mfano wa UFILIPINO, kama utaweza kung'amua hongera. Ukishindwa ndiyo basi tena...

​
 
Ukinielewa ni sawa, usipotaka kunielewa ni sawa pia. Mimi nimetimiza wajibu wangu na sintadaiwa lolote lile mbele za MUNGU. Binafsi huwa siandiki kufurahisha genge, wala kutoka eneo la mihemko, huwa naandika ambacho nakifahamu vizuri pengine hata wengi wenu hapa hamjawahi kukisikia.

Wewe ni mwanasheria na siku zote nimekuwa nikikukanya sana uache kuleta mihemko kwenye taaluma yako. Huwa natunza kumbukumbu za watu mijadala ninayofanya. Mimi na wewe tulianza kupishana kwenye BANDARI ila muda ukasema. Tukapishana kuhusu LISSU na MIGA ila ukweli unafahamika. Leo hii tunapishana kuhusu TEC na umeamua kwa maksudi kutotaka kunielewa, au aidha hufahamu fika kuhusu historia.

YOTE TISA: Mara zote huwa nasema kwamba MUDA HUSEMA UKWELI.
​
 
Soma tena kwa utulivu na ufahamu.

Usisome mada kwa kuangalia maneno (Semantics) yangu peke yake.

Zingatia na muktadha (Context) wa UFILIPINO ambao ndiyo msingi wa hoja yangu nzima.
===============================================================
Duterte na familia yake walipambana na CBCP.

Duterte akawashambulia sana hadharani.

Duterte kweli alikuwa na ushahidi wa makosa ya kihistoria na binafsi ya viongozi.

Duterte alionekana kushinda vita dhidi ya CBCP, leo hii Duterte yuko wapi na CBCP wako wapi ???
================================================================

KWAMBA hamuoni ya UFILIPINO na TANGANYIKA yanaendana sana tofauti zikiwa ni ndogo sana ????
​
 
Kwetu haijatoka warrant ya siri?
 
Wewe jamaa sometimes sijui huwa UNAKULA visungura.

Yaani huwa UNABONGA sana PUMBA wakati mwingine.

Sijui ni VISUNGURA au PROPAGANDA MASLAHI.

Kwanza Kanisa Katoliki huwa linapata NGUVU kwasababu siku zote linasimama na UMMA bila HOFU wala NJAA.

Ndio maana kwenye MATAMKO yao yote, hakuna tamko ambalo wametoa KUDAI manufaa yao peke yao, mostly huwa ni MASLAHI ya watu wote, hasa UHAI na MALI YA UMMA.

Kusema Katoliki huwa wanajiona wanamiliki serikali ni KULEWA CHIMPUMU.

Wewe unataka watu WAUAWE, waporwe MALI na UHAI, au kutekwa halafu KANISA likae KIMYA. Kwahiyo kwako MAUAJI, UTEKAJI, RUSHWA, DHULMA ni SIASA????


Kama unataka Kanisa katoliki likae kimya acha KUPORA mifumo ya Umma kama BUNGE, Media na VYAMA VYA SIASA.


Umezuia Bunge, Media na vyama vya siasa halafu unataka kila mmoja akae kimya???

Kuhusu wanafunzi wa Nyerere pia UMEPUYANGA, hoja siyo wanafunzi wa Nyerere, hoja ni kuwa WANASIASA wenye akili siku zote wanajua nguvu zao ni wananchi wao, na hata siku moja HAWAKUWAHI KUWAGEUZIA BUNDUKI wananchi wao wenyewe.

Hata leo IRAN ambaye ana mabeef duniani lakini wananchi wake wanaandamana hajawageuzia bunduki watu wake.

Kama umeingia vitani na wananchi wako mwenyewe, usilaumu pale ambapo ukivamiwa kutoka nje hao wanamchi wako hawawezi kupambana upande wako.
 
Ukweli upi unafahamika kuhusu Lissu na MIGA?

Nilikuuliza swali hujanijibu hadi Leo? Kwa kufuta retention licences Tanzania hatukushtakiwa? Hatujalipa matrilioni ya fedha kutokana na kushtakiwa kufuta leseni za utafutaji na uchimbaji madini?

Una changamoto kubwa ya kuwa mjuaji kupitiliza na kutokubali ukweli pale unapokosea. Kwenye suala la kushtakiwa kuhusu kufuta leseni za madini hadi sasa tumelipa zaidi ya trilioni 2 pesa za walipakodi na bado kuna makesi mengine yapo Mahakamani. Kwa nini unakataa kuelewa hoja ya Lissu?

Kuhusu TEC nimekupinga kwa hoja na wewe kama una hoja nipinge kwa hoja. Umedai TEC ni wadini na wao ndo wanajiona wana haki ya kuongoza hii nchi.

Swali langu kwako ipo wapi mantiki ya hoja yako ukizingatia TEC walimpinga na kumkosoa waziwazi Magufuli aliyekuwa mkristo na mkatoliki mwenzao?
 
Uingereza wao ni Anglikana ndo maana inaitwa Church of England....Marekani huko ni waprotestant...jifunzee kwanza
Uingereza walikuwa wanazozana na wakatoliki lakini kuanzia 1939 ikabidi waanze kushirikiana nao kwenye mambo ya kiutawala hasa ukizingatia wao ndiyo walikuwa na taarifa sahihi kuhusu Ulaya kipindi chote cha WW2. Walikuwa wakatoliki hawaajiriwi kabisa MI6 na MI5, baadaye baada ya watu kukomaa akili mambo yakabadilika sana.

Marekani moja ya chanzo cha Civil War 1861-1864, ilikuwa ni mvutano baina ya Ukatoliki na Uprotestanti. Kennedy ndiye Raisi wa kwanza Mkatoliki nchini Marekani, kiufupi walikuwa hawataki Mkatoliki atawale. Baadaye baada ya watu kukomaa akili mambo mengi yamebadilika Maraisi wakatoliki wamekuwepo.
=================================================================

TURUDI MADANI: Wewe unadhani nini utakuwa mwisho wa CCM vs TEC Rift ???
​
 
Ukweli upi unafahamika?

Lissu ni Mwanasiasa na Taarifa za mikataba huwa ni siri. Lazima huwa kuna trial and error ya taarifa hasa kwenye nchi hii ambayo tumeshapigwa vibaya sana kwenye mikataba.

Alichofanya Lissu alikuwa sahihi, maana mikataba yenyewe hatuioni.

Mwisho wa siku, Lissu ndio mbaya, ni Kilema leo ila kina SINGASINGA, ANGELA KIZIGHA na ZEE LA MILIONI kwa DAKIKA linakunywa WINE IKULU.
Leo hii tunapishana kuhusu TEC na umeamua kwa maksudi kutotaka kunielewa, au aidha hufahamu fika kuhusu historia.
​
Unapishana na TEC kuhusu kipi?

Ni kipi cha TEC usichokubaliana nacho.

Weka wazi.
YOTE TISA: Mara zote huwa nasema kwamba MUDA HUSEMA UKWELI. ​
Kwa huu upumbavu unaoandika, utakuwa upumbavu zaidi kusubiri ukweli kwenye hilo.
 
Ndio maana nikasema kuna kitu unakijua kuhusu mpango mkubwa wa kushufhulika wakatiliki na wakristo kwa ujumla wao nikihusianisha na ulichoandika kumhusu Pole Pole na akashufhulikiwa kwa haraka.

Anyway, nijuavyo Mimi,


Christians huwa hawapigani pekeao, Mungu wao ni mpiganaji nzuri tu , na mara nyingi amewahi kuvaa mavazi ya kivita na kuongoza mapambano front na akashinda yote na kuwashindia watu wake.

Wana wa Israel na wanafunzi wa YESU ni mfano nzuri sana.

Tusubiri.
 
TEC imefanya makosa mengi sana tangu kuanzishwa kwake.

Hata wakati Mwinyi anakuwa Raisi kuna baadhi ya viongozi walimfuata Nyerere kusema kwamba huyu mbona ni Muislamu. Nyerere akasema mimi mbona Mkristo nimetawala miaka zaidi ya 20 hamkuniuliza ???

Ushawahi kutokea mvutano mkali TEC na MUSLIMS hapa Tanzania kuhusu , Mzee Nyerere akasema hawezi kuwaonea haya Wakristo kwenye baadhi ya mambo na kuwakemea vilivyo. Mbona haya hamtaki kuyasema, au ndiyo SELECTIVE OUTRAGE ???
================================================================
Kuhusu LISSU, waliofungua kesi dhidi ya Tanzania kule LCIA walikuwa ni Acacia ambao hawakuwa wamepewa Certificate of Compliance na serikali ya Tanzania. Hivyo kesi ilitolewa LCIA na Barrick ambaye alisaini CONCESSIONS na Tanzania akaingia kwenye mjadala na serikali. Mbona hili liko wazi na limeandikwa sana hapa duniani, kwamba Acacia walikuwa hawana Locus Standi kufungua kesi LCIA wala kudai fidia MIGA. Au kuna jambo ambalo unalifahamu hatulifahamu ulitaje hapa ???
​
 
Kuna kitu kinapikwa,

Padre Kitima aongezewe ulinzi na waombaji tuongeze bidii kuomba.
 
Haki ina upande,
Askofu Desmond Tutu hakuwa mkatoliki lakini aliwapinga makaburu na utawala wao kwa msimamo thabiti kabisa.
Askofu Janani Luwumu hakuwa Mkatoliki ila alisimama kidete kumpinga Dikteta Iddi Amini
Mimi siyo Mkatoliki.

Ukweli ni kuwa, wanasiasa NGURUWE wamezima kila sauti ya umma (BUNGE, MEDIA, WANAZUONI, VYAMA VYA SIASA, BAKWATA, etc)

Sote, tumeona yaliyomtokea GWAJIMA. Tuliona yaliyomtokea KAKOBE, NIWEMUGIZI, KITIMA????

HIzi kelele kuhusu TEC , ni kwasababu wameshindwa KUWADHIBITI kwa MASLAHI yao na kuwaweka MFUKONI.


Kazi inayofanywa na TEC kama hawataki TEC waseme BASI waache mifunMmo ya UMMA kama BUNGE, MAHAKAMA, MEDIA, VYAMA VYA SIASA na WANAZUONI wafanye kazi??


Huwezi kuzima KILA sauti.

Huwezi KUUA, KUTEKA, KUFIRA, watu halafu kila mwenye akili timamu AKAKAA KIMYA, kwa kusingizia hizo ni SIASA na anayekwambia acha anataka MASLAHI.

Huo ni UTAAAHIRA.
 
Umenipa tuhuma nzito sana.

Japo niseme tu: TEC-BAKWATA-CCM Coalition ndiyo zimesaidia na kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa nchi yenye amani kwa vizazi vinne. Hawa wakipishana na kutopata A Common Ground, sisi hapa nje tunaweza kushangilia lakini taifa linadidimia. Tofauti na mivutano imekuwepo sana, na haiwezi kuacha kuwepo ila tunavumiliana.

Tanzania ni nchi ambayo raia wake wanaaamini sana dini kuliko chochote kile. Haya yanayofanyika kipindi hiki yataleta madhara makubwa. Samia kacheza vibaya karata zake na kukataa kuwajibika na kujirekebisha. Mwisho wa hili ni nini haswaaa ???? Unadhani kuua au kuteka Mapadri na Wakatoliki kutasaidia ???

MWISHO KABISA: Unadhani huu mgogoro utaishaje kwa Tanzania yote, ukizingatia hizi taasisi kama TEC na BAKWATA ni nguzo muhimu kwenye utawala na usalama wa Tanganyika kwa ujumla ??? AU unadhani kwamba TEC na BAKWATA wakigawana mbao wewe na mimi tutakaa hapa kuandika hivi tunavyoandika ???
​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…