Siasa za kutishana hazitoimarisha Amani- Rais Samia

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Posts
4,191
Reaction score
677
Mheshimiwa Rais awaasa kina chadema kuhusu kutumia vitisho ubabe, kejeli na dharau kwa kushinikiza wayatakayo.

Mbowe amevunja sheria anapaswa wajibike kwa mujibu wa sheria

mama anashusha nondo
 
Mbona SSH anaendelea kuongelea kesi hii ya Mbowe ambayo iko mahakamani? Huku kama siyo kuingilia uhuru wa mahakama ni nini?
 
sheria ndio itaamua, kwa mujibu wa kuivunja sheria. mama kasisitiza yy hatovunja sheria
 
That is a Political maturity..... hongera Rais Mama Samia kwa kufahamu na kuzingatia kanuni mojawapo muhimu ya kidemokrasia ambayo viongozi wengi wa Kiafrika wameshindw kuizingatia.
 
Mbona SSH anaendelea kuongelea kesi hii ya Mbowe ambayo iko mahakamani? Huku kama siyo kuingilia uhuru wa mahakama ni nini?
kwani si zitto ndio aloanza kuizungumzia na kumuomba mwenzao aachiwe, yy kamjibu kua sheria ifatwe
 
Mheshimiwa Rais awaasa kina chadema kuhusu kutumia vitisho ubabe, kejeli na dharau kwa kushinikiza wayatakayo.

Mbowe amevunja sheria anapaswa wajibike kwa mujibu wa sheria

mama anashusha nondo
Amesema Mbowe amevunja sheria ama wewe umeongezea?

Kama amesema hivyo, basi tayari ameshamuhukumu na kuingilia muhimili wa mahakama ili ufuate anayoyataka yeye. Kama ni kweli kuongea hayo, huyu ataingia kwenye historia ya kuwa rais wa hovyo kuliko wote hapa Tanzania.

Pia kama ametumia hicho kikao chao kuleta mipasho, badala ya kujikita kwenye agenda walizo nazo kama zilikuwepo, kumeonyesha ni kwa jinsi gani utawala huu tumeingia choo cha kike.

Eti CHADEMA waache vitisho na ubabe? Anajuwa maana ya hayo maneno?

Vitisho na ubabe vinatoka kwenye serikali yake kwa mihimili yote mitatu kushiriki kwenye ukandamizaji wa demokrasia na uvunjaji wa katiba ya nchi.
 
Kama ni mhimili unaojitegemea, hata kama kweli yeye ametamka maneno hayo, bado haiifanye mahakama imsikilize yeye, mahakama ni mhimili mwingine, chombo huru chenye maamuzi yake... hata CDM wamekuwa wakisema mara nyingi kesi ifutwe na Mbowe aachiwe na ni moja pia la sharti lao kuhudhuria hiki kikao cha leo, hatuoni nao kama wanaingilia mhimili wa mahakama...

Inawezekana Mbowe kaonewa au hajaonewa, tusubiri mahakama iamue na maamuzi ya mahakama ndio yatatupa uelekeo wa next step..
 
Mbona SSH anaendelea kuongelea kesi hii ya Mbowe ambayo iko mahakamani? Huku kama siyo kuingilia uhuru wa mahakama ni nini?
zitto kamuomba tu kwa busara na mamlaka aliyonayo aliunganishe taifa. sasa mambo ya ujeuri wa CDM umekujaje tena hapo?
 
Kama ni mhimili unaojitegemea, hata kama kweli yeye ametamka maneno hayo, bado haiifanye mahakama imsikilize yeye, mahakama ni mhimili mwingine, chombo huru chenye maamuzi yake... hata CDM wamekuwa wakisema mara nyingi kesi ifutwe na Mbowe aachiwe na ni moja pia la sharti lao kuhudhuria hiki kikao cha leo, hatuoni nao kama wanaingilia mhimili wa mahakama...

Inawezekana Mbowe kaonewa au hajaonewa, tusubiri mahakama iamue na maamuzi ya mahakama ndio yatatupa uelekeo wa next step..
Mahakama hizo ambazo majaji na jaji mkuu wanateuliwa na huyo huyo anayesema Mbowe kavunja sheria unategemea nini?

Hivi haufahamu ni kwanini katiba mpya ni muhimu ili kuondokana na ujinga huu?

Ikiwa kuna mtu yeyote ambaye yuko “above the law”, hiyo siyo katiba ya wananchi.

Kwenye katiba makini ya wananchi, “no one is above the law”.

Hapo muhimili wa mahakama utakuwa huru kweli kweli.
 
Mheshimiwa Rais awaasa kina chadema kuhusu kutumia vitisho ubabe, kejeli na dharau kwa kushinikiza wayatakayo.

Mbowe amevunja sheria anapaswa wajibike kwa mujibu wa sheria

mama anashusha nondo
Mama anajisahau kuwa serikali yake ndyo serikali ya vitisho na ubabe!

Hao CHADEMA wasio na jeshi lolote wakitegemea wananchi waoga kuwaunga mkono wana vitisho na ubabe gani??

Je, CHADEMA walishawah kupora uchaguzi Kama CCM alivyofanya 2019 serikali za mitaa??
Vipi kuhusu uchafuzi mkuu 2020, mbabe na mporaji na mtishaji alikua Nani??

Mama ananyoosha kidole kwa CHADEMA huku vidole vyote vitano vikimrudia yeye!!
 
Mbona SSH anaendelea kuongelea kesi hii ya Mbowe ambayo iko mahakamani? Huku kama siyo kuingilia uhuru wa mahakama ni nini?
Inashangaza Maza kuing'ang'ania hiyo kesi .... mpaka sasa serikali imeshindwa kujenga kesi ambayo inaonyesha huo ugaidi. Ni Mahakama tu ndiyo inayoibeba serikali ...... nafikiri anachuki ya kususiwa na CDM....!!
 
Mahakama hizo ambazo majaji na jaji mkuu wanateuliwa na huyo huyo anayesema Mbowe kavunja sheria unategemea nini? Hivi haufahamu ni kwanini katiba mpya ni muhimu ili kuondokana na ujinga huu?

Ikiwa kuna mtu yeyote ambaye yuko “above the law”, hiyo siyo katiba ya wananchi.

Kwenye katiba makini, “no one is above the law”. Hapo muhimili wa mahakama utakuwa huru kweli kweli.

hiyo hiyo katiba ndio inatuambia Mahakama ni mhimili unaojitegemea na hauingiliwi na mtu..

Jaji kuwa mteuliwa hakumfanyi kushindwa kuamua, kwani jaji anaweza kutenguliwa ujaji?.. hapa ni utashi binafsi wa jaji mhusika kuamua kufuata sheria au kusikiliza mamlaka...
Hata hiyo katiba mpya ikiwepo bado jaji anaweza tu kuamua kuweka weledi pembeni na akaamua kwa utashi wake na tusimfanye kitu... KENYA WANA KATIBA MPYA LAKINI KILA SIKU TUNASHUHUDIA HIYO MIGOGORO YA KISHERIA NA WATU KUISIGINA KATIBA...

Hakuna Mahala Katiba hii tunayotumia imesema Rais yuko juu ya sheria....mihimili iko mitatu na yote inajitegemea.....Katiba inasimamiwa na watu, watu wasipostaarabika wataivunja tu hata iweje..
 
Mbona SSH anaendelea kuongelea kesi hii ya Mbowe ambayo iko mahakamani? Huku kama siyo kuingilia uhuru wa mahakama ni nini?
Mbona nyie kila siku mnatoa maneno kuhusu mbowe na press je hamuoni mnaingilia mahakama?
 
Back
Top Bottom