Siasa za Tanzania zinakosa tija kwasababu wanaharakati wa kisiasa wanatumia muda mwingi ku-attack personality badala ya kuwa objective

Siasa za Tanzania zinakosa tija kwasababu wanaharakati wa kisiasa wanatumia muda mwingi ku-attack personality badala ya kuwa objective

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Hili ni tatizo ambalo naona linazidi kukomaa, siasa za wanaharakati wa sasa iwe chama tawala ama wenye mirengo ya upinzani, wamekuwa ni watu wenye hoja za ku attack personality zaidi na kukosoa kila jambo.

Yaani kama ni mwanaCCM anaona harakati zake hazijakamilika bila kumtukana Mbowe au Lissu au arushe kombora la matusi kwa upinzani.

Vivo hivyo kwa wanaharakati wa upinzani, inakuwa ni kama harakati zake hazijakamilika mpaka amtusi kiongozi fulani wa chama tawala.

Mi nadhani kati ya mambo ambayo itabidi watanzania tubadilike kwenye siasa zetu, hili ni mojawapo. Sipendezwi na siasa za ku-attack personality kwasababu matusi huwa hayapanui wigo wa kufikiri wala kuongeza kitu kipya zaidi ya kuibua uhasama.

Ingekuwa wanaharakati wanatumia muda mwingi kujenga hoja ambazo zipo objective pasipo masuala ya kutukanana, huenda hii nchi ingekuwa mbali tofauti na ilipo sasa.

Na hii moja kwa moja, inaenda chini mpaka kwenye mfumo wetu wa elimu, watu wanafika mpaka chuo kikuu lakini wanashinda kutofautisha maana ya kuwa objective kwenye kujenga hoja na kujenga hoja kwa kua attack personality.

Nikifikiria kati ya mwaka 2010 mpaka 2011 pale UDSM kulikuwa na harakati kali sana, ila kusema ukweli zilikuwa ni harakati za mihemko zaidi na kua attack personality.

Ni kama miaka kumi imepita na bado harakati za Tanzania bado hazijabadilika kabisa.

Siasa zetu bado ni za matusi matusi na mihemko hakuna objectivism. Mtu anapanda jukwaani anaongea ushizi mpaka mtu unayemtazama unaona aibu wewe.

Tubadilike
N.Mushi
 
Haya mambo yalikuwepo tangu awamu ya kwanza. Na utaratibu wa walioko madarakani kumchafua na kumzushia mtu yeyote mwenye hoja na mawazo tofauti na bora zaidi.
 
..haya mambo yalikuwepo tangu awamu ya kwanza.

..na utaratibu wa walioko madarakani kumchafua na kumzushia mtu yeyote mwenye hoja na mawazo tofauti na bora zaidi.
Anyway ni siasa za kipumbavu tu, japo zinawanufaisha wenyewe ila hazitufai
 
..haya mambo yalikuwepo tangu awamu ya kwanza.

..na utaratibu wa walioko madarakani kumchafua na kumzushia mtu yeyote mwenye hoja na mawazo tofauti na bora zaidi.
Tatizo kubwa la siasa zetu ni ukosefu wa ideology.

Wanasiasa wote wa CCM na upinzani hawana chochote ambacho wanasimamia wala hawajui wakipate vipi.

Ni ukweli mchungu kwamba siasa zetu bado zinaongozwa kwa hulka ya Rais.

Sasa tatizo ni kwamba vyama vya upinzani wanalitambua hilo ila wanaona kama kulionesha hadharani ni kujishusha.

Baada ya Magu kufariki, Mbowe alisema Never and Never again, na wakaanza harakati za kushinikiza katiba mpya wao kama wao as if wana huo ubavu wa kuzuia chochote au kushinikiza chochote.

CCM pia wao wanaishi kwa hisani ya Rais ambaye ni mwenyekiti wa chama chao, yaani kwa lugha rahisi wanaCCM wanaishi kama machawa wa Rais. Maana ukiwa Rais kupitia CCM ni kama unapewa kila kitu.

Siasa za ushawishi zimekuwa ngumu, wananchi pia hawajaona utayari wa kupambania siasa kwasababu hawaoni maslahi yoyote kwao.

Wanaharakati wenyewe wamekata tamaa na kibaya zaidi hawajui wanatafuta nini.

Serikali ikifanya A wanataka B, ikifanya B wanataka A ni ilimradi hawaungi mkono upande wa serikali.

Na ikitokea wameumizwa, suluhisho ni kutukana maana huwezi kupambana na mwenye nguvu.

Ili kujenga siasa za hoja na fikra jambo la kwanza na muhimu ni kuwa na ideology.

Ukitegemea matukio na trends kila siku utakuwa na agenda mpya.
Jana ulikuwa na katiba mpya, leo una bei ya petrol na miamala ya simu. Kesho sijui utakuja na ipi ?
 
Hustoria inaongea wazi,hakujawahi kuwepo maendeleo na siasa kwa wakati mmoja.

So wacha tuendelee kupiga danadana hapa maendeleo baadae kwanza.
 
Alianzisha Magufuri siasa za kuattack watu badala ya matukio hivyo huo ugonjwa utachukuwa muda mrefu labda ccm wakubali kuwa Tanzania kuna mfumo wa Vyama vingi na si mfumo maslahi tulionao sasa.
 
Usemacho ni kweli kabisa,Nchi yetu imekaa chuki Sana lakini Ukiangalia kwa makini ni kokosekana kwa HAKI.Kuna kundi kwenywe jamii yetu Ina haki wakati kundi kundi linguine Halima haki.Hivo basi lazima Hali iwe hivo .Siku Kila mwananchi akipata haki haya mambo yatapungua.Haki,Haki,Haki.
 
Tatizo kubwa la siasa zetu ni ukosefu wa ideology.

Wanasiasa wote wa CCM na upinzani hawana chochote ambacho wanasimamia wala hawajui wakipate vipi...
Nimepata hapo kwenye ideology mkuu, nadhani vyama vya upinzani vingekua vinaibiri ideology zao mara kwa mara(kama zipo) na wananchi wakajua hwa wakiingia serikali itakua 1 2 3. Kuliko kuamka na trending news kila kukicha.

Mwisho wa siku wanachama wengi hasa wapya wanakua wapo tu hata hawajui wanachokiamini.
 
Wauchu na waroho wa madaraka, wanaona haki ipo upande wao pekee...
 
Nimepata hapo kwenye ideology mkuu, nadhani vyama vya upinzani vingekua vinaibiri ideology zao mara kwa mara(kama zipo) na wananchi wakajua hwa wakiingia serikali itakua 1 2 3. Kuliko kuamka na trending news kila kukicha.

Mwisho wa siku wanachama wengi hasa wapya wanakua wapo tu hata hawajui wanachokiamini.
Ideology si ndio hiyo katiba mpya.
 
Ideology si ndio hiyo katiba mpya.
Ideology ya katiba wamekuja nayo baada ya kudhulumiwa uchaguzi, vitu vingi wanavofanya CHADEMA n matokeo ya matukio fulan yalofanywa na CCM na mwenyekiti wake.

lkn wao kama chama wanakosa jambo na falsafa ya kusimamia ambayo inaleta uniqueness ya chama chao. Chama lazima kiwe kina mrengo, kiwe inakitu cha kusimamia regardless ya hali ya chama tawala.
 
Lakini mwisho wa siku mwanzo wa kuja na ideology ungekuepo tu. Hata isingekua kipindi hiki wangekuja nayo kipindi cha nyuma napo sababu ingepatikana kama ilivopatikana ya sasa hv.
Cha msingi wananchi hatutakiwi kua na upande kwa sababu nchi ni yetu. Tunatakiwa tusikilize kila upande na kuchambua kilicho bora. Kama katiba ni jambo la msingi. Hiyo ni fact na huwezi kuiondoa. Hata kama imesemwa na adui
 
Back
Top Bottom