Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Hili ni tatizo ambalo naona linazidi kukomaa, siasa za wanaharakati wa sasa iwe chama tawala ama wenye mirengo ya upinzani, wamekuwa ni watu wenye hoja za ku attack personality zaidi na kukosoa kila jambo.
Yaani kama ni mwanaCCM anaona harakati zake hazijakamilika bila kumtukana Mbowe au Lissu au arushe kombora la matusi kwa upinzani.
Vivo hivyo kwa wanaharakati wa upinzani, inakuwa ni kama harakati zake hazijakamilika mpaka amtusi kiongozi fulani wa chama tawala.
Mi nadhani kati ya mambo ambayo itabidi watanzania tubadilike kwenye siasa zetu, hili ni mojawapo. Sipendezwi na siasa za ku-attack personality kwasababu matusi huwa hayapanui wigo wa kufikiri wala kuongeza kitu kipya zaidi ya kuibua uhasama.
Ingekuwa wanaharakati wanatumia muda mwingi kujenga hoja ambazo zipo objective pasipo masuala ya kutukanana, huenda hii nchi ingekuwa mbali tofauti na ilipo sasa.
Na hii moja kwa moja, inaenda chini mpaka kwenye mfumo wetu wa elimu, watu wanafika mpaka chuo kikuu lakini wanashinda kutofautisha maana ya kuwa objective kwenye kujenga hoja na kujenga hoja kwa kua attack personality.
Nikifikiria kati ya mwaka 2010 mpaka 2011 pale UDSM kulikuwa na harakati kali sana, ila kusema ukweli zilikuwa ni harakati za mihemko zaidi na kua attack personality.
Ni kama miaka kumi imepita na bado harakati za Tanzania bado hazijabadilika kabisa.
Siasa zetu bado ni za matusi matusi na mihemko hakuna objectivism. Mtu anapanda jukwaani anaongea ushizi mpaka mtu unayemtazama unaona aibu wewe.
Tubadilike
N.Mushi