Wakuu nimevumilia hili lakini naona linazidi.
Siku hizi kuna wimbi kubwa la watu wameona kuandika maudhui ya kukejeli kabila la wasukuma ni ujanja ama ni Content ! Na wengine wasiojielewa huendelea kukoment upumbavu na kuchekelea🇹🇿
Kuna majitu yanafurahia sana hizi kejeli ,kwani wasukuma wamewakosea nini?
Siku hizi kila mfano mbovu mitandaoni wanapakaziwa wasukuma mnaudhi na huo upuuzi sisi ni kabila bora,na hatuhitaji dharau.
Kutweza utu wa wasukuma sio sawa. Watanzania tafadhali tuache kudharauliana kipuuzi.
Kila kundi la watu linastahili kuheshimiwa na kuthaminiwa.
Heshimu tamaduni za watu na maisha yao.
Wasukuma wote tusikubali huu upumbavu,tuukemee mahali popote na tuoneshe umoja na mshikamano.