Sifurahishwi na dhihaka zinazofanywa dhidi ya Wasukuma Mitandaoni

Ni kweli, Wasukuma ni kabila lenye watani wengi nchini...!
 
Wasukuma Ni kabila kubwa kila mtanzania anawajua. Wewe jiulize umeshawahi kumuona au kumsikia kabila gani zaidi ya msukuma? Yupo kila sehemu ya Tanzania hii Ni sifa kubwa Sana, kuwatania Ni sawa huwezi kuongelea kitu hujaona Wala kusikia.
Hongereni wasukuma.
 
Mleta mada itakuwa kaanza juzi juzi kutumia Internet na social media! Vumilia utazoea tu na baadae hata wewe utakuja kujikuta unacheka sana ukiona huo unaoita udhalilishaji.

Mimi ni mhehe, kuna kipindi nilikuwaga nakasirika sana nikisikia mtu ananiambia tunakula mbwa,
Baadae nikaja kugundua kumbe ni utani tu ukizingatia sijawahi kumla huyo mbwa nikaanza kuchulia poa. Sasa hivi mimi ndio nakuwa muanzisha mada ya utani wa kula mbwa kwa watu ninaotaniana nao.
 
Wasukuma kutaniwa na haijaanza leo, jana wala juzi na wala huo utani hautawahi kuisha ni kabila kubwa na maarufu zaidi Tanzania kwa hiyo kutaniwa ni lazima cha kufanya wewe kaa kwa kutulia tuu hauna lolote la kufanya kwenye hilo
 
Najivunia kuwa Msukuma, nina marafiki wengi na wananikubali kwa sababu ninajiamini na nina uwezo wa kuishi na watu kwa upendo.
Wasukuma tumegawanyika kulingana na shughuli za uzalishaji mali.
Tuna bidii katika kazi na kujiimalisha kimaisha kwa kutafuta fursa popote inapopatikana. 💪
 
Wasukuma ni wajinga sana.Kwa hiyo mkitaniwa mnalia? Wajinga ninyi.Kale michembe ulale.Bloody sukuma!🫸🫷😝😝😝😝😝😝
 
kama na wewe ngoosha kuwa mpole tu nyie ni washamba sana angalia mnvyojazwa kwenye malori ya mchnga kwenda kumshangilia hangaya as if hamna kazi za kufnya huo nao ni ushamba pia bado sijagusa kwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…