Sifurahishwi na Wachina kujenga sanamu ya baba wa Taifa

Sifurahishwi na Wachina kujenga sanamu ya baba wa Taifa

Babeli

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2015
Posts
6,702
Reaction score
3,272
JF

Nimeona tangazo la Mh.Waziri kuhusiana na Sanamu ya baba wa Taifa ambayo wamesema watajitolea kugharamia na ambayo itawekwa Makumbusho ya Taifa.

Najiuliza kwa sauti kubwa sana

1. Hivi nchi yetu haiwezi kugharamia hili? how much?

2. Ile ni Sanamu nyeti mno na ni nembo kwa Taifa letu, kwanini tuwape wachina waweke nembo ya baba wa Taifa kwetu, why?

3. Ni lazima vitu vingine tuweke values zetu na tutembee vifua mbele kwamba ni sisi tumetengeneza na hata wao wanaweza kufanya moja ya sehemu ya utalii ya kutembelea. Je, Wanalitengeneza wao itakuwa na thamani gani kwao kuja kuiangalia si wanaijua in/out.

4. Ni lazima tuwe watu wa kutengeneza values zetu..na hata hao wachina na wengine watatuheshimu siku zote..

Nawaza kwa sauti kubwa sana... sifurahishwi wajameni
 
Take it easy mkuu. Sanamu ni sanamu tu, hayana unyeti wa kuzidi.

Relax, acha watengeneze labda litakuwa zuri. Unakumbuka kitu alitengeneza Kigwangala? Ule ndio uwezo wetu sasa
Kwa maneno yako tayari umeshajidharau na kujikataa..jomba uko vizuri..wewe utakuwa teenager hujui hizi habari
 
Nyie watoto hamyajui haya..mnadandia Mambo kwa mbele tu
Kakudanganya nani Mimi mtoto!?..nimefulia majani ya mpapai,milenda,gwanji,sukari guru,ilikua ukiondoka tabora ukarudi miaka 15 baadae hukuti mabadiliko yoyote,nchi haijengeki,foleni za unga,watu kutembea uchi kusini huko kwa kukosa nguo...na mwenyewe alisema ujamaa ulifeli
 
Vipi kuhus Wachina waliokuwa wanavaa uniform kama za shule nchi nzima..hata Korea
 
Vipi kuhus Wachina waliokuwa wanavaa uniform kama za shule nchi nzima..hata Korea
Hao wajamaa,na itakua kipindi Cha Mao,mao alikua kiongozi wa hovyo,aliyeibadili china ni kiongozi wao wa miaka ya 70,nimesahau jina
 
Hao wajamaa,na itakua kipindi Cha Mao,mao alikua kiongozi wa hovyo,aliyeibadili china ni kiongozi wao wa miaka ya 70,nimesahau jina
Aaah jomba miaka hiyo alikuwa Mao..na ndie aliyeweka misingi imara ya Taifa ambalo unaliona sasa
 
Take it easy mkuu. Sanamu ni sanamu tu, hayana unyeti wa kuzidi.

Relax, acha watengeneze labda litakuwa zuri. Unakumbuka kitu alitengeneza Kigwangala? Ule ndio uwezo wetu sasa
Una uhakika gani mkuu kama hiyo sanamu haitabeba siri nyingine nyuma ya pazia?
 
Tulishawapa wazawa ikawa hivi🐒👇

images (80).jpeg
 
Mkuu 'Babeli', labda ungeweka utangulizi au ufafanuzi kidogo wa habari yako ingependeza sana.

Hii habari wewe umeitoa wapi; na kuna maelezo yoyote juu yake kwa nini waChina wame"pendekeza/omba/wanamsukumo wa kufanya kazi hiyo?
Ni nani anahusika kwa Tanzania kutoa uamzi kazi itekelezwe?

Maswali ni mengi sana, lakini hayo tuyaache pembeni nijaribu kuungana nawe kwenye baadhi ya uliyoandika hapo juu.

Nami nauliza: hivi kwa mfano, swerkali, au basi tuseme ile Taasisi inayohusiana na maswala ya Mwalimu chini ya (nani yule Butiku?), wangesema wanao mpango wa kutoa heshima hiyo kwa Mwalimu, na wakawaambia waTanzania wenyewe kuchangia kazi hiyo, hata Tsh 500/ tu kwa wenye uwezo ndani ya nchi hii na hiyo mia tano, kweli ingeshindikana kuifanya kazi hiyo?

Anyway, Mwalimu mwenyewe alisema wakati wa uhai wake kwamba hana mpango na masanamu, lakini katika hili hana uamzi juu yake, kwa hiyo waTanzania wangejisikia vizuri zaidi kuwa sehemu ya kumuenzi kiongozi wao aliyewatumikia kwa unyenyekevu mkubwa sana.

Kuhusu viongozi wa leo tulio nao, hii habari yako haina mashiko yoyote kwao, kwa hiyo vyovyote na iwavyo wao hayawahusu. Watajionyesha tu kwa nje kushiriki na kuruhusu mambo lakini kwa ndani hawana chochote kinachowaunganisha na aliyoyasimamia Mwalimu ndani ya nchi hii.

Acha waChina wajenge, kwani wanajua urafiki wa dhati aliowapa Mwalimu wakati wa uhai wake.
Watayafanya haya si kwa kuwapendesha viongozi waliopo, lakini ni shukrani zao za dhati kwa Mwalimu.
 
Nisawa na rafiki yako akwambie anataka mnunulie mkeo mpenzi nguo nzuri sana inayomfit na kumpendezesha..utajisikiaje..
 
Back
Top Bottom