Mkuu 'Babeli', naona kampeni yako kama kweli upo 'serious'; haina msingi wowote inaposimamia.Pamoja na maneno hayo jomba, tuanze na hili...hatuwezi kuwaachia wajenge..tuanzie hapa...nooooway..
Lakini nakupa tahadhari, usidhani napingana nawe katika hili, la hasha, ni kwamba msimamo huu unaousimamia wewe/mimi, akilini mwa wahusika haupo kabisa!
Sasa ngoja nikwambie jambo: ndiyo, ni aibu kwetu sote kwa ujumla wetu wote kujengewa kumbukumbu ya kiongozi wetu tuliyemheshimu sana kwa kujali maslahi yyetu na nchi yetu, kana kwamba sisi wenyewe hatuwezi kuifanya kazi hiyo. Ndiyo, ni aibu kwetu sote.
Lakini nikukumbushe tu kama umesahau, au nikutaarifu kama hukujua..., ni kiongozi huyo huyo aliyetuasa tuwe makini sana katika kulinda heshima yetu na uhuru wetu kwa kutokubali kujiuza kwa hao wanaotuwekea bei kwenye thamani ya maisha yetu. Leo hii vikampuni kama Symbion, vinapokohoa tu, sote tunapata mafua!
Na kana kwamba hiyo haitoshi, sasa ndiyo tunajitumbukiza kabisa kwenye majanga, waje watujengee hata miundombinu, kama barabara, na watutoze gharama za kuitumia barabara hiyo, kama huwezi, pita unakojuwa mwenyewe! Huu ni mfano mdogo tu wa njama zinazoturudisha kwenye utumwa, ukichochewa na hao wakubwa wa mapesa yao kama Benki ya Dunia, IMF na wengineo. Bila hivyo tunaambiwa hatutapata maendeleo.
Siku moja tu ukikorofishana na mashoga wao, wanatulaza gizani, au wanafunga barabara, utafanya nini! Hapana, usidhani natania; kwani Zimbabwe ya Mugabe huioni hapo?
Wanatuhimiza sana tuingie kwenye utegemezi kwao ili watutawale vizuri.
Halafu unakuja hapa na kukomalia jambo ambalo tunajuwa wachina wanataka kulifanya kwa kujituma kwao, kwa heshima waliyomwekea Mwalimu Nyerere?