Mkuu 'Babeli', labda ungeweka utangulizi au ufafanuzi kidogo wa habari yako ingependeza sana.
Hii habari wewe umeitoa wapi; na kuna maelezo yoyote juu yake kwa nini waChina wame"pendekeza/omba/wanamsukumo wa kufanya kazi hiyo?
Ni nani anahusika kwa Tanzania kutoa uamzi kazi itekelezwe?
Maswali ni mengi sana, lakini hayo tuyaache pembeni nijaribu kuungana nawe kwenye baadhi ya uliyoandika hapo juu.
Nami nauliza: hivi kwa mfano, swerkali, au basi tuseme ile Taasisi inayohusiana na maswala ya Mwalimu chini ya (nani yule Butiku?), wangesema wanao mpango wa kutoa heshima hiyo kwa Mwalimu, na wakawaambia waTanzania wenyewe kuchangia kazi hiyo, hata Tsh 500/ tu kwa wenye uwezo ndani ya nchi hii na hiyo mia tano, kweli ingeshindikana kuifanya kazi hiyo?
Anyway, Mwalimu mwenyewe alisema wakati wa uhai wake kwamba hana mpango na masanamu, lakini katika hili hana uamzi juu yake, kwa hiyo waTanzania wangejisikia vizuri zaidi kuwa sehemu ya kumuenzi kiongozi wao aliyewatumikia kwa unyenyekevu mkubwa sana.
Kuhusu viongozi wa leo tulio nao, hii habari yako haina mashiko yoyote kwao, kwa hiyo vyovyote na iwavyo wao hayawahusu. Watajionyesha tu kwa nje kushiriki na kuruhusu mambo lakini kwa ndani hawana chochote kinachowaunganisha na aliyoyasimamia Mwalimu ndani ya nchi hii.
Acha waChina wajenge, kwani wanajua urafiki wa dhati aliowapa Mwalimu wakati wa uhai wake.
Watayafanya haya si kwa kuwapendesha viongozi waliopo, lakini ni shukrani zao za dhati kwa Mwalimu.