Sifurahishwi na Wachina kujenga sanamu ya baba wa Taifa

Pamoja na maneno hayo jomba, tuanze na hili...hatuwezi kuwaachia wajenge..tuanzie hapa...nooooway..
Mkuu 'Babeli', naona kampeni yako kama kweli upo 'serious'; haina msingi wowote inaposimamia.

Lakini nakupa tahadhari, usidhani napingana nawe katika hili, la hasha, ni kwamba msimamo huu unaousimamia wewe/mimi, akilini mwa wahusika haupo kabisa!

Sasa ngoja nikwambie jambo: ndiyo, ni aibu kwetu sote kwa ujumla wetu wote kujengewa kumbukumbu ya kiongozi wetu tuliyemheshimu sana kwa kujali maslahi yyetu na nchi yetu, kana kwamba sisi wenyewe hatuwezi kuifanya kazi hiyo. Ndiyo, ni aibu kwetu sote.

Lakini nikukumbushe tu kama umesahau, au nikutaarifu kama hukujua..., ni kiongozi huyo huyo aliyetuasa tuwe makini sana katika kulinda heshima yetu na uhuru wetu kwa kutokubali kujiuza kwa hao wanaotuwekea bei kwenye thamani ya maisha yetu. Leo hii vikampuni kama Symbion, vinapokohoa tu, sote tunapata mafua!
Na kana kwamba hiyo haitoshi, sasa ndiyo tunajitumbukiza kabisa kwenye majanga, waje watujengee hata miundombinu, kama barabara, na watutoze gharama za kuitumia barabara hiyo, kama huwezi, pita unakojuwa mwenyewe! Huu ni mfano mdogo tu wa njama zinazoturudisha kwenye utumwa, ukichochewa na hao wakubwa wa mapesa yao kama Benki ya Dunia, IMF na wengineo. Bila hivyo tunaambiwa hatutapata maendeleo.

Siku moja tu ukikorofishana na mashoga wao, wanatulaza gizani, au wanafunga barabara, utafanya nini! Hapana, usidhani natania; kwani Zimbabwe ya Mugabe huioni hapo?

Wanatuhimiza sana tuingie kwenye utegemezi kwao ili watutawale vizuri.

Halafu unakuja hapa na kukomalia jambo ambalo tunajuwa wachina wanataka kulifanya kwa kujituma kwao, kwa heshima waliyomwekea Mwalimu Nyerere?
 
Wewe utakuwa ni chizi, kama hata hukumbuki unachoandika mwenyewe, dakika chache tu baada ya kukiandika.
Na inawezekana kabisa bado huelewi kinachozungumziawa hapa!
Halafu najifanya mjuaji, kumbe huna lolote unalojua!
 
Wewe utakuwa ni chizi, kama hata hukumbuki unachoandika mwenyewe, dakika chache tu baada ya kukiandika.

Na inawezekana kabisa bado huelewi kinachozungumziawa hapa!
Halafu najifanya mjuaji, kumbe huna lolote unalojua!
huyo ni mtu alini-quote,Mimi maandishi yangu' yameanzia kwa waziri mkuu...punguani mmoja
 
Unataka watengeneze kama lile la Kigwangara Chato?
 
Ingekuwa wanajenga ya Mao hapo sawa malalamiko yako yangekuwa na mantiki, lakini wanajenga ya Baba yetu wa Taifa? Wacha wajenge shida nini kwani?
 
Take it easy mkuu. Sanamu ni sanamu tu, hayana unyeti wa kuzidi.

Relax, acha watengeneze labda litakuwa zuri. Unakumbuka kitu alitengeneza Kigwangala? Ule ndio uwezo wetu sasa

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]
 
huyo ni mtu alini-quote,Mimi maandishi yangu' yameanzia kwa waziri mkuu...punguani mmoja
Ameku'quote' wapi, hata hujui maana ya ku'quote'?
Huoni hayo ni maneno uliyoandika mwenyewe?

Napoteza muda wangu kujibishana na chizi hapa. Nenda kafilie mbali, 'hoodlum' mkubwa.
 
Kama tukiwapinga wachina tumpe kigwa.
Mbona tunapewa ARV,tunajengewa madarasa tunapewa vitabu nk hatuyaoni hayo?
 
1. Hivi nchi yetu haiwezi kugharamia hili? how much?

Kuna mambo huwezi kuyaelewa ukiwaza kwa kutumia ubongo wa nyama na damu...

Tambua tu kuwa sanamu lolote lile, ni madhabahu kwenye ulimwengu wa kiroho...
 
Bora wachonge na wagharamie, uliiona ile aliyoichonga kigwangala, labda ya babu yake, alafu anatuambia eti baba wa taifa na nilishauri ivunjwe au apeleke nyumbani kwake na asiseme tena eti baba wa taifa! Anawatoto yule anafikiri wanachukuliaje!
 
Nyerere alisafiri uchina mara nyingi zaidi kuliko Nchi yeyote
 
Ameku'quote' wapi, hata hujui maana ya ku'quote'?
Huoni hayo ni maneno uliyoandika mwenyewe?

Napoteza muda wangu kujibishana na chizi hapa. Nenda kafilie mbali, 'hoodlum' mkubwa.
Wewe ni punguani,unalazimisha niwe nimesema hivyo
 
Nyerere alipigania uhuru peke yake mbona wapiganaia uhuru wengine hawatajwi kwenye historia
 
Mbona hata kwao Beijing ipo tena kuibwa sana! Wacha wajenge, sanamu ni sanamu tu, Mwalimu Nyerere yuko kwenye mioyo ya Watanzania na hilo ndio la msingi![emoji119]
 
Kwanini wewe usitengeneze na wao wakatengeneza ?

Baba wa Taifa kutokana na Itikadi zake Wachina wanamuelewa kama wamesema wanagharamia wewe unaona shida gani wakigharamia ? Unataka watu waanze kupiga kelele kwamba sababu la yeye amefanya na wenyewe wafanyiwe hence kuendelea na muendelezo wa kuchezea Kodi zetu ?!!!

Hata wewe haukatazwi chonga sanamu likiwa zuri hata likikosa sehemu ya kuwekwa nina uhakika Mama Maria kule Butiama atalichukua.....
 
Sanamu ya Nyerere aliyoitengeneza Kigwangwala ikazinduliwa na Jiwe uliiona ? ungeweza kulia .

Nadhani hicho ndio kimefanya watafutwe wachina
Kigwa alitafuta wafinyanzi wa vyungu akawapa tenda
Ila hii nchi jamani sijui inaendaje endaje. Masanamu nayo niyanini tena kwa mahela mengi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…