wastani kwa idadi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 503
- 1,432
Wala siijui formula ya aina ipi ya mwanamke wa kuoa hata huyu nilite naye siijui kesho yetu hivyo nachoweka hapa ni theory tu lakini waweza kupata kitu.
Sikuoa rafiki yangu, nilikuwa na marafiki wengi wa kike hata wa muda mrefu tuliowahi kuwa kwenye uchumba lakini haikuwahi kunijia akilini kuoa rafiki wa kike.
Nimemuoa akiwa na miaka 19, cha kuzingatia zaidi nimemzidi miaka, tupo rika tofauti, kwa makadirio yangu nadhani binti wa miaka 18 hadi 23 ana experience ndogo kwenye mapenzi kuliko mwanamke mwenye umri mkubwa, pia itakuwa binti mdogo ni rahisi kumfinyanga kwa jinsi ulivyo kuliko mwanamke mkubwa
Nimeoa kwenye jamii ambayo ndugu wa karibu na wa mbali hawaingilii sana maisha ya mwanamke akiolewa, sijajua kama imetoka kwenye ukoo au kabila lake, Katokea Iringa ila baada ya mkoa kugawanywa itakuwa ni Njombe, Wazazi wake tunawatembelea na kuwajulia hali lakini wao hapa kwetu mama yake amewahi kuja mara chache, Ndugu zake wakija huwa ni kwa shughuli zao, alipojifungua na alipowahi kuumwa ndugu walikuja mumpa msaada alipopona wakakaa kidogo wakarudi makwao .
Haendekezi mambo ya dini, Siku ya kwenda ibada ni moja shughuli imeishia hapo ni mpaka wiki lijalo, kwa mawazo yangu huwa naona labda wanawake wakianza kushinda sana sehemu za ibada, dorminance ya mwanaume wake inahamia kwa wachungaji.
Ana elimu ya kawaida, si jambo la kufurahia lakini naweza kuweka iwe moja ya factors, kaishia form 4 ana division 3 yake, Nimekuwa nikisikia baadhi ya wanaume waliooa wanawake wasomi wakilalamika lakini kwa utafiti mdogo niliofanya kuna namna vyuo huchangia, mwanafunzi wa sekondari akiingia chuo kuna ule uhuru wa ghafla tena akiwa mbali na kwao bila usimamizi, tuliosoma vyuoni tumejionea live jinsi mabinti wanavyobadilika kwa kasi ya radi ndani ya muda mfupi, hii inawathiri hata wakimaliza chuo, kuna mtindo wa maisha, marafiki waliowazunguka na vitu walivyojifunza vinavyoweza kuleta changamoto ndani ya ndoa.
Nilimjaribu kabla hatujaingia kwenye ndoa, vijana wengi siku hizi wanavuta jiko ndani bila kujua uimara wake, sio mtaalam sana wa kupima vigezo lakini binafsi nilimpima kwa kunifulia nguo, kunipikia, usafi wa chumba enzi hizo nimepanga vyumba viwili, n.k. so tulipoingia kwenye ndoa nilishajipatia uhakika haya mambo anaweza,
Meza jeuri yako pale unapoona umekosea au umemkosea mke wako, usihamishe lawama ama kutafuta visingizio, ni ngumu kwa mwanaume kusema samahani lakini waweza konyesha kwa vitendo na yeye atajua,