Siikubali CCM kwa namna wanavyoendesha nchi ila Sina Imani na mpinzani wake CHADEMA

Wewe tena lazima upinge maoni yangu kwasababu mlengo wako unajulikana
 
Mimi siwakubali CCM liko wazi lakini nitajie chama kingine unaona kinauwezo na kipo tofauti na CCM karibia kila kitu ni kipi? Na nitajie kwakutoa sababu Tano tu
 
Sijasoma yote. Ila nakujibu tu kijumla waambie serikali waiachie CHADEMA ifanye siasa za haki kama inavyofanya ccm. Iwaachie viongozi wake iliyowaweka ndani bia sababu. Mwambie msajili awe fair asiibughudhi CHADEMA kama anavyofanya sasa bila sababu. Waambie waachie uchaguzi uwe huru na haki hata ½ tu. Hapo ndipo utaikubali na kuilewa CHADEMA. Unafikiri serikali yenu inahangaika kuidhibiti CHADEMA kila kona bure?. Usichokijua CHADEMA ndio wananchi wote
 
Mazur na mabaya ya ccm tayar yameshaonekana ivyo twataman tuone mabaya na mazur ya vyama vingine wenzet uko walipo endelea wameona tama na chungu za kila chama na hata uongoz wa kijeshi
Sawa lakini wasipewe kwa huruma au kwa kuangalia madhaifu ya CCM bali wao wenyewe waoneshe kuwa wanaweza kupitia matendo ya viongozi wao, namna wanavyoendesha vyama vyao, ilani zao kupitia sera na vision vya namna watavyoendesha nchi kuwa ni Bora.
 
Ww mawazo yako inabidi yaungwe mkono maana mlengo wako haufahamiki.
Nakuuliza tu swali nitajie sababu kuu 5 kwanini unaamini Chadema wanastahili kuongoza nchi
 
Hata Chadema wangekuwa ni chama tawala na wapinzani wao ni CCM lazima Mambo kama hayo yangekuwepo na hii hiko kwenye siasa za kiafrika hakuna chama kinamuonea huruma chama pinzani. Kwahiyo Mimi Kama mwananchi nachoangalia maslahi yangu sio ya wanasiasa na ndio maana sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote.Nilichokitoa hapo ni maoni yangu kwa kile ninachofikiri na sio kila mawazo tunatakiwa tufanane wote
 
SIO CCM WALA CHADEMA HAKUNA KITU HAPO...CCM HII INAYOWAAMBIA WANANCHI WAKE IMEWARAHISISHIA HUDUMA YA MATIBABU KWA KUWALETEA HUDUMA YA AFYA KWA WOTE(NHIF), AMBAYO MPAKA SASA HUDUMA HYO NI HEWA..NASEMA UONGO NDUGU ZANGU.. ILE AHADI YA NHIF KWA KAYA YA WATU SITA MPAKA SASA NI HEWA.. WANANCHI WANAZID KUUMIA KWA MATIBABU KUWA NA GHARAMA KUBWA..KWAKWELI TZ INAWENYEWE.
 
Tungekuwa tuna vyama pinzani vizuri Leo CCM wasingekuwa madarakani lakini ndio hivyo we imagine kiongozi wa chama cha upinzani anadai kabisa viongozi wao wananunuliwa na CCM anaongea haya bila aibu
 
Haya mawazo ndio yanayofanya Africa ibaki hivi ilivyo. Ksbb ya mawazo yaliyosimama sehemu moja. Kitu usichokijua hata ukatae vipi kuleta mageuzi bado siasa ndizo inayoendesha maisha yako ya kila siku.
UMASIKINI ULIONAO IWE WA KIMAWAZO,KIELIMU AU KIUCHUMI NI KSBB YA SIASA MBOVU SANA ZINAZOIENDESHA NCHI. JAPO WAPO WAMEBAKI WACHACHE WENYE MAWAZO KAMA YAKO WANAJUA KUHANGAIKA NA UMASIKINI WAO NI KSBB YAO. SIASA MBOVU ZA NCHI HUSIKA KAMA HIZI ZA HILI LICHAMA INAHUSIKA KUWAFUKALISHA WANANCHI WAKE.

Kwa sasa wanatamani asitokee hata mtu mmoja kuwashtua wananchi kuhusiana na upigaji unaendelea ndani ya hii serikali. Na bahati mbaya hakuna wa kuwazuia. CHADEMA ambayo ingesaidia kupigia kelele huo wizi mkubwa unaoendelea ndio hiyo imepigwa pin,na wananchi wa kawaida kama wewe unafurahia bila kujali kwamba huo ufisadi unakwamisha hata maendeleo yako.

Juzi juzi kuna kiongozi alijaribu kukemea ufisadi unaoendelea kupitia mitandao yake. Unajua kilichotokea? Ile post yake ya kukemea imefutwa chap baada ya muda mfupi. Unajua maana yake? Wamebariki ufisadi unaoendelea.
 
Tungekuwa tuna vyama pinzani vizuri Leo CCM wasingekuwa madarakani lakini ndio hivyo we imagine kiongozi wa chama cha upinzani anadai kabisa viongozi wao wananunuliwa na CCM anaongea haya bila aibu
Sasa kama wananunuliwa kweli? Na ccm ndio iliyoko madaraka. Imejineemesha kwa mali zetu. Imewafanya watu wawe masikini wa kipato na elimu pia ni rahisi sana kuwanunua kssb ya hali duni iliyowasababishia
 
Ilipofikia CCM haiwezi kutulrtea kiongozi yeyote mzuri akiwa ndani ya CCM.
Sababu ipo mikononi mwa watu wachache wahuni, wabinafsi, wabadhirifu n.k.
Anaye jiona kiongozi mzuri basi ajitoe CCM akkaunde chama au ajiunge vyama vingine isipokuwa chama cha ubwabwa na ACT.
 

Hao CCM nani aliwaweka madarakani 2025?

Vv
 
Hivi nani kakudanganya kwamba ili uwe mfuatiliaji wa siasa lazima uwe mpenzi au mwanachama wa chama
 
Basi wewe una matatizo. Hujui unachotaka. Haya mambo siyo ya imani. Kwani CCM hufurahii mambo yake kwa sababu ya imani au kwa anachofanya.
 
Sasa kama wananunuliwa kweli? Na ccm ndio iliyoko madaraka. Imejineemesha kwa mali zetu. Imewafanya watu wawe masikini wa kipato na elimu pia ni rahisi sana kuwanunua kssb ya hali duni iliyowasababishia
Kama viongozi wao wananunuliwa ina maana Wana watu wengi wenye njaa na wanaopenda rushwa hii si moja ya sababu yakutuonesha kuwa hawastahili kupewa nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…