wanasema ukiyajua matatizo yako bàsi unaenda kupona.
Lakini kwangu ni tofauti mimi ni mama wa watoto 2, baba wawili tofauti...
Ninatatizo sijui linatokana na nini na ni hali ambayo kwa sasa nimegundua ninatatizo na najichukia lkn siwezi kujicontrol
2013 niliolewa na kijana mzuri anakazi nzuri lkn tuliishi miez 2 tu nikaondoka na mimba juu ya miez 6.
Tatizo nililonalo mkorofi, yan mbabe ukikaa vibaya mwanaume tunashikana tupigane,, au nichukue kitu nikupige nacho ninamaneno nikianza kuongea shombo hata usiku kucha. Mwanzo sikujua tatizo nn niliishia kuwalaumu wanaume na kujiona ninamkosi lkn seriously mi sio mwanamke wa kuishi na mwanaume aisee ...
Mungu kanibariki sura nzuri nyota ya kupata wanaume wa kuniona wapole na wenye kipato kizuri tu tatizo wanakimbia tabia.
2017 nikapata mume mwingine mpole kaka wa watu japo anakaumalaya lkn nimtu peace sana tumezaa mtoto 1,, kaka anapata tabu huyu jaman.
Tunaweza kaa vizuri tu gafla kuna hali inanitokea ya kuanzisha ugomvi tu ambao haueleweki nitalia usiku kucha.
Nikikuta msg ya mwanamke kwenye cm nitapasua cm yake, vitu ndan navunja ...baada ya muda hali inapotea naanza kujuta nalia.
Nikikaa wiki mbili bila ugomvi gafla from no where natafuta ugomvi tu bila sababu yani nikiwaza tu kwamba tunasiku nyingi hatujagombana kosa la jinai halafu baada ya muda mfupi narudi kwenye hali ya kawaida ya kujuta sana na kushangaa kwann nimefanya haya.
Nimekaa nae nimemwambia tuachane maana naona namtesa kaka wa watu lkn hataki unakuta sipendi kua hivi ananiambia anaimani ipo siku nitabadilika.
Mi naona atachoka tu nayeye hata hivyo kanivumilia sana sijui kwann hataki kukubali kuachana
Inaniuma tumeishi tangu 2017 maisha haya haya bila ndoa lkn cha ajabu anataka tuandikishe ndoa tubariki nashindwa kuelewa yeye hachoki haya maisha? Sio mchoyo, ananipa kilakitu kilichondani ya uwezo wake lkn muda wote nalalamika tu.
yeye weakness yake anapenda wanawake na akiwa nao kwenye mahusiano analalamika namnyanyasa mi roho inaniuma namwambia sababu tulianza 0 kwa sasa tunamafanikio na hiyo inatokana na akili yangu ya maendeleo. Nimemwambia anipe mil 5 tu kama mtaji, nyumba nimwachie na viwanja, mifugo lakini hataki kuachana na mimi anasema wewe ni mke wangu hakuna kwenda popote
Kunakipindi alitembea na rafiki yangu tangu nilipogundua hali ndio ikazidi ya ukorofi ni miez 7 lkn nikikumbuka naanzisha ugomvi as if ndio nimemfumania leo..
Nifanyeje jmn either nikae Sawa au niondoke bàdo mapema maana huyu siku akichoka sijui atanifanya nn.
Akipokea mshahara wote ananipa anachukua ya matumiz yake nyingine ananipa mimi ndio napanga ya kula nyingine naweka akiba...kiufupi namimi mbali na hii tabia, nimwanamke wa maendeleo napambana pia nina akili ya maisha hii imetupelekea kupata maendeleo ndani ya muda mfupi..
Pole kwa changamoto unazopitia. Tatizo unalolielezea linaweza kuhusiana na changamoto za kihisia au afya ya akili, kama vile impulse control disorder, bipolar disorder, au athari za matukio ya awali katika maisha yako (trauma).
Hali hii inaweza kudhibitiwa kwa msaada wa kitaalamu.
1. Tafuta msaada wa kitaalamu
- Therapist au mtaalamu wa afya ya akili: Tafuta mtaalamu ambaye unaweza kuzungumza naye. Atakusaidia kuelewa mizizi ya tabia yako, iwe ni kutokana na trauma, hali ya kihisia, au matatizo ya homoni.
- Mtaalamu wa familia na mahusiano: Ikiwezekana, mwalike mume wako katika mazungumzo haya. Inaweza kusaidia kuboresha mawasiliano kati yenu.
2. Tambua na urekebishe vichochezi vya hasira yako
- Andika kwenye journal au daftari kila mara unapogombana. Tambua kilichokuudhi, ulijisikiaje, na nini kingeweza kufanyika tofauti.
- Mara unapojua vichochezi vyako (trigger points), utaweza kujifunza kuzidhibiti. Mfano, badala ya kuvunja vitu au kuanzisha ugomvi, jaribu kutoka kidogo, kupumua kwa kina, au kujitenga hadi utulie.
3. Jifunze mbinu za kudhibiti hasira
- Deep breathing: Ukiwa na hasira, pumua ndani kwa kina kwa sekunde tano, shikilia pumzi kwa sekunde tano, kisha toa taratibu. Rudia mara tano.
- Zungumza polepole: Jitahidi kuelezea unavyohisi badala ya kufoka au kutumia vitisho. Mfano, badala ya kusema, “Wewe ni malaya,” sema, “Najisikia vibaya nikiona ujumbe kama huu.”
- Jitenga unapohisi unakaribia kulipuka: Kusema, “Naomba muda kidogo nitulie,” kunaweza kuepusha mabishano yasiyo ya lazima.
4. Zungumza na mume wako kwa uwazi
- Elezea jinsi unavyojiona na kujuta baada ya ugomvi. Mwambie unahitaji msaada wake kushinda changamoto zako.
- Mweleze jinsi unavyothamini juhudi zake za kuvumilia, lakini pia uweke mipango ya kubadilika. Mfano, mnaweza kuanzisha safe word ya kutumia ili kusimamisha ugomvi kabla haujawa mkubwa.
5. Jipe muda wa kujitunza (Self-care)
- Pata muda wa kufanya vitu unavyovipenda, kama kusoma vitabu, kufanya mazoezi, au kujiingiza kwenye shughuli zinazokuondolea stress.
- Jifunze kutunza afya yako ya mwili na akili kwa kupata usingizi wa kutosha, kula chakula bora, na kuepuka vinywaji au vyakula vinavyoongeza msisimko wa hasira (kama vile pombe kupita kiasi).
6. Shirikisha familia na rafiki wa karibu
- Ikiwa unaweza, waelezee watu wa karibu kile unachopitia. Wanaweza kukusaidia kwa ushauri au kukuweka kwenye njia sahihi unapokosea.
Mwisho kabisa: Usijichukie.
Hali unayopitia si kwamba wewe ni mbaya, bali ni tatizo ambalo linaweza kushughulikiwa. Unayo nafasi ya kubadilika na kurekebisha mambo.
Jitahidi kujipa moyo na kuamini kuwa hatua unazochukua zitakusaidia kupata amani ya kudumu ndani yako na katika familia yako.
Ova